Wachina wamejipiga pini kwenye vita ya ushuru, Soko kubwa dunia nzima lipo Marekani

Wachina wamejipiga pini kwenye vita ya ushuru, Soko kubwa dunia nzima lipo Marekani

Mexico ni soko kubwa la Marekani kuliko china ... Dola Bilion 300 Kwa mwaka ...


Trump alichofanya amepiga Tarrif China halafu kawashushia nchi zingine nusu tariff 20% ... Kiakili anaandaa nchi zingine zipeleke bidhaa Marekani na sio kutoka china.


India naona atatake over...


Acha kulialia muafrica wewe angalia kama fursa ya kupeleke bidhaa Gani china!



Soko lingine analouza kwa kiasi hiko cha $140B ni lipi?. Inaonekana wazi kuwa hata US yenyewe haiko tayari kulikosa hilo soko la Uchina.

Trade deficit kwa US haikwepeki maana industrial power yake haifikii ile ya Uchina.
 
Soko la Africa linampa china Dola bilion 160 tu. Wakati Marekani kama soko Moja tu Kwa china linampa Dola bilion 500.


Nyie waafrica umasikini umewajaa mnaagiza yeboyebo na ndoto za plastic hamna uwezo wa kureplace soko la Marekani Kwa mchina.


Domestic Consumer Spending yaaani soko la ndani la china ( akiuza bidhaa zake ndani ) ni Dola Trilion 6


Wakati soko la ndani la Marekani, Marekani akiuza bidhaa zake ndani ni Dola Trilion 7.


Marekani anaingiza Dola bilion 160 kutoka china Kwa mwaka wakati soko lake Moja la mexico anaingiza Dola bilion 300+


Kumbuka hizo nchi mbili Moja Ina idadi kubwa ya watu china ( milion 900+)

US ni nusu ya hiyo milion 900. Kimahesabu china ndio ana stress. Idadi ya raia milion 900 Kuihudumia sio mchezo. Ajira zilizokuwa zinatolewa na mnyororo wa Makampuni ya Marekani kuwepo china ni Kubwa sana. Nina rafiki mchina hivi ninavyoandika anasema hali ya ajira inaenda kuwa mbaya sana kwao. Anataka ahamie nchi nyingine. Viwanda ni vingi bidhaa hawana pa kuuza
China bado ni mtengenezaji na mtundu wa bidhaa rahisi na wakati mwingine zilizo bora sana na kwa Bei nafuu. Nchi zingine Bei ya bidhaa zao ni ghali sana. Pili, China Ina soko la ndani la watu bilioni 1:4, asilimia karibu 20 ya watu wote duniani iko china., jumlisha na soko la Africa na Asia China Ina soko la asilimia karibu 50 ya watu duniani. Angalau China wana ubavu wa kumkoromea Mmarekani. Sisi wamatumbi wa bongo tungemlamba miguu tu.
a chin
 
Tesla hata Wamarekani wameanza kampeni ya kuzisusa kutokana na ujinga wa Elon Musk.

Ndio muda mzuri wa Kununua hisa Sasa . . Bulls tunazama soko likiwa chini. Siku tariff zikitolewa Tesla inaamia kama Simba aliejeruhiwa
 
Mexico ni soko kubwa la Marekani kuliko china ... Dola Bilion 300 Kwa mwaka ...


Trump alichofanya amepiga Tarrif China halafu kawashushia nchi zingine nusu tariff 20% ... Kiakili anaandaa nchi zingine zipeleke bidhaa Marekani na sio kutoka china.


India naona atatake over...


Acha kulialia muafrica wewe angalia kama fursa ya kupeleke bidhaa Gani china!
Hao na NAFTA yao wanafanya biashara at a gun point huku US ndiye mnufaika mkubwa.

Swali, je US yupo tayari kulikosa hilo soko la Uchina lenye thamani ya $140B nje ya NAFTA?.
 
Marekani kwa hilo kachemsha,China huo upepo walishauona siku nyingi,labda kama na ulaya yote itaamua kumbania,China imeshikilia mpk masoko ya ulaya kwahiyo huo mkwala wa Marekani haumpi pressure...
 
Ndio muda mzuri wa Kununua hisa Sasa . . Bulls tunazama soko likiwa chini. Siku tariff zikitolewa Tesla inaamia kama Simba aliejeruhiwa
Bila taarifa sahihi utashikilia loss sana na vile Bwana mkubwa hatabiriki.
 
Marekani anamtegemea m China kupata cheap labor na cheap products.

Hizo tariffs zikiwa in effect vitu vitapanda bei mara tatu na Marekani watu watashindwa kununua.

Na hata kuhamisha production kutoka China si kitu cha kufanya mara moja.

Wamarekani wakipata arosto ya kukosa bidhaa za bei chee kutoka China kwa mwezi mmoja tu, kutatokea machafuko makubwa Marekani.

Ndiyo maana Stock Markets za Marekani zimeanguka Mpaka Trump kaondoa ujinga wake wa tariffs za ajabu dunia nzima, kabakisha 10% tu na tariff kubwa kabakiza China, na huko China atapunguza mwenyewe.

Ndiyo maana Trump kaanza kuomba kupigiwa simu wayajenge na Mchina.

Wakati Mchina kasema ukimwaga ugali namwaga mboga wala sikupigii simu.
Yes, dow Jones ilishuka Ile mbaya mno from 42000 to 36000 ndani ya muda mchache mno, hapa inaweza ikawa game ya kuwatoa hela na wengine wanachukua Mana hapa Kuna marginal trading account za futures wenye ku swing on the fence waliunguza akaunti.
Ila I can say wachina Wana rise panapo vikwazo. Kikawaida ukibaniwa ama ukifanyiwa figisu lazima upate akili tu, penye hardship champions rise. Pia elewa USA ni jalala la watu tofauti tofauti kutoka Kila pande ya dunia Ila china ana race yake pekee yaani just Chinese genes like Russia Sasa angekuwa anachanganya na kuiba watu wenye akili kubwa duniani unadhani wangekuwa wapi hao watu wawili plus na north Korea. So USA namuona ni Kama ni Malaya hajatulia
 
Trump alichofanya amepiga Tarrif China halafu kawashushia nchi zingine nusu tariff 20% ... Kiakili anaandaa nchi zingine zipeleke bidhaa Marekani na sio kutoka china.


India naona atatake over...
Kwani malengo ya hizi tariffs ni zipi kama si kurudisha viwanda US na kuchochea uwepo wa ajira na export, sasa India achukue mikoba si itakuwa ni nje ya malengo.

Wawekezaji wenyewe hawapo tayari kuondoa viwanda kutoka China, hapo ndipo Trump anapopata ugumu kwenye hii sera yake.
 
Kuna kitu hamkielewi... Laiti mngekielewa basi ingekua ni fursa kwenu

Maisha yanamtaka mtu mwenye macho mengi or mwenye jicho 1 linalozunguka kama dishi la kutazama matrilion ya kilometers
Fursa ipi kwa mtanganyika mlala hoi?
 
Screenshot_20250412-193355~2.png
 
Marekani katuwekea ushuru wa 10% kwenye pamba tunayomuuzia, kwanini tusiipeleke China ambako hatutotozwa ushuru?
Kwa hiyo kuuza pamba ghafi china unaona ni fursa? Kufanya hivyo si unaongeza ajira kwa wachina?

Tukiwauzia pamba yetu, wanai process na kutengeneza boxer ambazo watatuzia mara 1000 ya bei waliyonunulia pamba yetu.

Sasa bwashee hiyo ni fursa kwa mtz au kwa mchina?
 
Kwa hiyo kuuza pamba ghafi china unaona ni fursa? Kufanya hivyo si unaongeza ajira kwa wachina?

Tukiwauzia pamba yetu, wanai process na kutengeneza boxer ambazo watatuzia mara 1000 ya bei waliyonunulia pamba yetu.

Sasa bwashee hiyo ni fursa kwa mtz au kwa mchina?
Sasa kama hamuwezi kuichakata si bora muokoe kidogo kilichokua kinapotelea Marekani?
 
I like this.

Kwa walioona, utawala wa Trump una lugha mbaya sana ya dharau, ubabe na udhalilishaji kwa mataifa mengine na viongozi wao.

Kwa walioshuhudia udhalilishaji aliofanyiwa Zelenskyy pale White House na kejeli zinazoendelea kutolewa na Trump, Musk, Vance na Hegseth dhidi ya EU, Canada, Mexico, na Denmark wataelewa (wakipenda). Dunia imeshuhudia.

Kwa China, Trump ameamsha zimwi la Mao Zedong! Xi aliingia madarakani kuhakikisha China inasimama kama super power, isidharauliwe na Marekani kwa vile tu imekubali uchumi wa soko na biashara huria (free trade).

Xi ni muumin wa Mao kiasi chake. China imeshatahadharisha utawala wa Trump kuwa HAITAKI DHARAU. Trump atasubiri sana simu ya Xi. Xi hana kikwazo cha opinion polls. Wala Hana uchaguzi unaomkabili. Tuone. Who will blink first.
Umeelezea vizuri sana mkuu, Xi amekataa bullying na coercion kutoka kwa Trump mwendawazimu​
 
Makampuni ya Marekani yanatumia China kuzalisha bidhaa.

If they take away manufacturing from China, China itaumia zaidi
Unazani hiyo ni kuhamisha ni kazi ya siku moja?

Hiyo relocation sio projects ya siku moja mzee,inaweza ikawachukua miaka zaidi ya kumi kuandaa hayo mazingira kuanzia miundombinu, resources na kutrain watu na hayupo mfanyabiashara au kampuni itaakayo fanya hivyo.
 
Hii thread inajadiliwa kishabiki sn Wale Pro Arab,Russia,Iran,Hezbollah, Hamas na Hauthi ndio wanaoishabikia China na kuiponda US.. usishangae hao hao kabla ya kulala wanameza ARV ambazo Donor from US..
Kwahio unaumia asee
 
Mbona hizo nchi hazikuuza huko hata kabla ya kuwekewa 10%?
Trump alitegemea china kabla ya leo awe ameomba deal, leo naye kaongeza tariff hadi 125% na kasema baada ya hapa hataongeza tena tariff maana namba kufikia hadi sasa hazimake sense tena ni kama no business at all.
China hataki kupiga magoti maana demands za marekani haziishi. Demand zake zinabadilika.
K
Kila mtu humu ni gwiji wa uchumi, siasa na michezo.
😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom