Siku zote huwa nasema kuwa, Wakristo ni njia nyembamba inayoonwa na kupitwa na wachache, wengi wenu mma majina ya Kikristo au mnaupenda Ukristo au mmerithishwa Ukristo au na Mashabikintu na wapenzi wa Ukristo lakini kamwe si Wakristo na hamjawahi kuwa.
Ni wapi katika Ukristo mliapangiwa au mlifundishwa kiasi cha mahari mnachotakiwa kutoa? Ni wapi mlifundishwa mfanye sherehe kubwa za kufahari?
Ni wapi mlifundishwa kufanya misiba na maziko ya kifahari?
Watu mnajiamulia wenyewe kuishi mifumo yenu ya kimaisha halafu mnasingizia dini.
Mbona Wakristo wa huko Ulaya, Marekani na kwingineko nje ya Afrika hawafanyi mambo ya ndoa na maziko kifahari? Wengine hata mahari hazitolewi?
Mfumo wa ufungishaji ndoa wa bomani ulitumiwa ma wakoloni wakiuleta kutoka huko kwao. Mbona ndoa za Bomani leo hii huwa hatuzioni zikiwa na hizi mbwembwe?
Mkubali tu kwamba wengi huwa mnajidhania kuwa ni Wakristo ila kiuhalisia mpo nje kabisa ya Ukristo.
Ukristo unapaswa uutafute, unakuhitaji ujikane kweli, sasa dini inayokutaka ujikane na uichague yenyewe dhidi ya mali itakufundishaje kuishi maisha ya kifahari? Kwa uwezo na mali zipi ulizo nazo?