Waislamu Waafrika waliosoma madrasa wanaweza kuongea lugha ya kiarabu kwa ufasaha na weledi?

Waislamu Waafrika waliosoma madrasa wanaweza kuongea lugha ya kiarabu kwa ufasaha na weledi?

Mkuu, huko Madrasa watoto wanafundishwa kwa mfumo wa lugha kama zilivyo lugha nyingine. Kwa maana ya kwamba a b c d & a e i o u.

Wanafundishwa vyema kabisa, ndio maana mwanafunzi bora anayezingatia mafunzo ana uwezo wa kukifahamu Kiarabu kwa ufasaha.
Wengi wanafundishwa kwa kukariri tu lakini si kwa kuandika kwenye madrasa. Kuna shule wanasoma Arabic kama somo ila sijajua kama wakitoka huko wanaweza kuwa wataalamu wa lugha hiyo. Halafu lugha yoyote ili kuijua vizuri inahitaji kuifanyia mazoezi kwa kwa kuongea, shida inakuja, wanaongea na nani?
 
OK, achana na kujichanganya kwangu, jibu swali; kijana aliyesoma madrasa na akaiva, anaweza kwenda Uarabuni na akaongea Kiarabu vizuri? Or, wewe kama bwana Malaria, unaweza kutumia simu yako hiyo ikiwa kwenye lugha ya Kiarabu?
Asilimia kuwa hawajui. Wamekariri tu Quran.
 
Wengi wanafundishwa kwa kukariri tu lakini si kwa kuandika kwenye madrasa. Kuna shule wanasoma Arabic kama somo ila sijajua kama wakitoka huko wanaweza kuwa wataalamu wa lugha hiyo. Halafu lugha yoyote ili kuijua vizuri inahitaji kuifanyia mazoezi kwa kwa kuongea, shida inakuja, wanaongea na nani?

UNASHANGAA NINI? HUSHANGAI HII
Nchini Tanzania taasisi ya utafiti wa masuala ya elimu Twaweza imetoa ripoti yake inayoonesha kuwa asilimia 44 ya wanafunzi wanaomaliza shule za msingi nchini Tanzania hawajui kusoma vitabu vya Kiingereza vya darasa la pili.

Hata hivyo kwa mujibu wa utafiti huo, asilimia 16 wamebainika kuwa nao hawawezi kusoma vitabu vya Kiswahili vya darasa la pili. Tena utafiti ni shule za makanisa
 
Swali, Biblia ya Wakristo wa Uarabuni imeandikwa kwa kiarabu, sasa kwa nini Wakristo wa Uarabuni hawajui kusoma Qur'an na imeandikwa Kiarabu?
Kwamba kuna watu wanajua Kiarabu fasaha lakini hawawezi kusoma na kuelewa Quran?!
 
Sheikh gani sasa huyo hata kusoma na kuelewa Kiarabu hawezi! Huyo itakuwa sheikh jina tu.
Vijijini huko watu wanajipachika majina ya sheikh kumbe hawajui kitu chochote.
 
Sisi tunafundishwa kusoma Quran ambacho ni kitabu cha Mwenyezi Mungu, kilichoshushwa kwa lugha ya kirabau ambayo ndio lugha ya Mtume wetu SAW.

Tunafundishwa lugha ya kiarabu tunapokuwa madrasa. Ni kama vile shule unapofunzwa kiingereza au kifaransa haina tofauti. ni Lugha tu. inatusaidia kuilewa zaidi Quran kwa sababu Quran haiwezi kubadilishwa kwenda kwenye lugha zingine compeletely, ila inaweza kutafsiriwa kwa lugha yeyote. Lakini inaposomwa inasomwa kwa lugha yake ya asili ambayo ni kiarabu.

Hii imeweza kuifanya Quran kubaki na maneno yale yale bila kubadilishwa kwa miaka 1400 na itabaki hivyo mpaka siku ya mwisho.
 
Kwanini Quran ishushwe imeandikwa kiarabu?
Basi, hata huko mbinguni watakuwa wanazungumza kiarabu pia
Si ilishushwa kwa mtume na watu wanaoongea lugha hiyo. Sasa ulitegemea iwe ya kiswahili. Vitabu vyote vya dini viliandikwa kwa lugha zao . Kilichotakiwa ni viongozi kufanya juhudi za kufundisha Quran kwa lugha zinazotumiwa na watu mbalimbali
 
Hata hapa mjini wengi hawajui. Wamekariri Quran nzima lakini hawajui kusoma.
Kwamba anakuwa amekariri tu surat ila haijui tafsiri au maana yake?!
Ila wengi huwa naona wakinukuu aya ya Quran wanatoa na tafsiri yake kwa Kiswahili.
 
"Na hapana yeyote miongoni mwenu ila ataifikia (Moto wa Jahannam); hilo ni jambo lililokadiriwa na Bwana wako, ni lazima."

Tafsiri na Maelezo:

"Na hapana yeyote miongoni mwenu ila ataifikia": Hii inaeleza kwamba kila mtu atapita au kufikia Jahannam (Moto wa Jehanamu), lakini haimaanishi kwamba kila mtu ataingia ndani yake. Aya hii inatafsiriwa na wanazuoni kuwa kila mmoja atapita juu ya Sirat (daraja lililo juu ya Jahannam) siku ya Kiyama, ili kuonyesha nguvu ya hukumu ya Mungu na haki yake.
Aya inaeleza wazi waislamu wote watakwenda motoni, kwa nini tuhitaji maelezo ya wanazuoni? Au umeshasahau Qur'an ni kitabu kilichokamilika kisicho na shaka yoyote?
 
Basi,nataka hata sisi waislamu wa Tanzania tuongee kiarabu broken ili tuwafunge midomo mahasidi.
Kingereza ni lugha ya kufundishia secondary mpaka chuo kikuu, kwa hiyo ni rahisi watu wengi kukijua. Kiarabu sio. Ila wakristo wanatumia biblia za kiswahili na hata za lugha za makabila mbalimbali. Waislamu badala kujikita kufunisha Quran kwa kiswahili wao wanamezeshwa bila kujua maana yake. Mtu kahifadhi Quran nzima bila kujua maana yake, huyo ana tofauti gani na ambaye hajahifadhi?
Quran inatakiwa ifundishwe na watu waielewe lakini hili halifanyiki.
 
Na hii ndio tofauti ya QURAN NA BIBLIA, Quran imebaki kama ilivyo kwa miaka 1400 na mpaka sasa dunia nzima tuna Quran moja tu. Na ndio maana utaona mashindano ya kusoma Quran yanafanyika Tanzania yanahusisha nchi 40 ambazo hizo nchi zinaongea lugha tofauti. Lakini inapofika kwenye Quran tunayo moja tu dunia nzima.


Lakini kwa wenzetu wakristo wao wana bible zaidi ya 6000 duniani kote, ukiachilia mbali utofauti wa lugha kwa maana kila bible ipo kwenye lugha yake, lakini pia ndani ya lugha moja kuna bible tofauti tofauti kila dhehebu lina bible yao. Hata bible za kiswahili tu zimetofautiana za wasabato zikiwa tofauti na za wakatoliki na walutheri. Na ndio mana kamwe huwezi kuona Wakristo wakifanya mashindano ya kuhifadhi bible kwa sababu kila mtu ana bible yake kwa version yake na kwa lugha yake..

Kwa waislamu hata wakiwa madhehebu tofauti lakini Quran yao ni moja tu popote duniani.
 
Kwamba anakuwa amekariri tu surat ila haijui tafsiri au maana yake?!
Ila wengi huwa naona wakinukuu aya ya Quran wanatoa na tafsiri yake kwa Kiswahili.
Si unamezeshwa vifungu na tafsiri yake. Mwambie akusomee uone kama anaweza. Ni wachache sana wanaweza hususani waliosoma Arabic
 
Vijijini huko watu wanajipachika majina ya sheikh kumbe hawajui kitu chochote.
Tafsiri ya Sheikh ni mzee au mtu anayeheshimika kwenye jamii siyo lazima awe na elimu ya dini.
Ndio maana hata gaidi Osama alikuwa wakimuita Sheikh Osama.
 
Back
Top Bottom