View attachment 3095829
Natumaini mu wazima humu, ni siku nyingine tukiwa bado tunasubiri muafaka wa mchezaji Kagoma kama atabaki Simba au atarudi Yanga, Mzee wetu magoma na yeye ni mpaka kieleweke !!,
Anyway tukirudi kwenye kichwa cha habari, Ujerumani imekubali kuwapokea Wakenya 250,000 na kuwapa nafasi za kufanya kazi nchini humo.
Makubaliano hayo yamefikiwa kati ya Rais William Ruto na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz.
Tayari madereva Watano toka Kenya wamefika kwenye mji wa Flensburg Ujerumani kupitia mpango huu. (Maderva hulipwa wastani wa euro 14 / shilingi elf 42 kwa saa)
Faida..
- Fursa za kujiongeza kielimu na kupata kazi zenye mishahara ya kizungu (Mwalimu analipwa milioni 8 kwa mwezi)
- Kupunguza tatizo la wahitimu wengi wasio na ajira Kenya
- Kupata connections za biashara za kimataifa, Mfano kununua maparachichi Tanzania kwa mia mbili, kuyauza ujerumani kwa elf 5.
- Diaspora inazidi kupanuka, baadhi ya sehemu kunakuwa na vijiji / mitaa iliyojaa wakenya
- Inakuwa rahisi kwa wakenya kuingia ujerumani wakiwa na ndugu, marafiki na jamaa waliojaa nchini humo.
- Wakenya kupata fursa za kutumia vipaji kupata pesa zaidi, Kuna vijana wadogo ujerumani wanacheza mpira wanakunja milioni 200 kila wiki.
- n.k.
View: https://x.com/visegrad24/status/1834677580542193790