Wakati tukisubiri vita kubwa sana kati ya Iran na Marekani

Uwongo...
Watu wengine ukiwaambia ni Wajinga wanakasirika wakati wanajua kabisa hawajui kitu chochote!!

Hapo umeambiwa watu walioisaidia Iran kutengeneza hayo makombola wewe unasema uongo sasa si useme ukweli wako?
 
Iran badala ya kusonga mbele, inazidi kudidimia kuelekea shimoni:

Mwaka 1972 Iran GDP ilikuwa


Ni kweli, sehemu kubwa ya alichoandika mleta mada ni uwongo.
Ulipoandika wewe ndio uongo... Iran imetengeneza hypersonic kabla ya North Korea na wanawasaidia kutengeneza hypersonic..

GDP za kitu gani? uchumi wa kwenye stocks, uchumi wa kitapeli huo...
Angalia PPP sio GDP.. angalia purchasing power kiongozi, Iran mafuta liter moja ni around 100 Tshs... wewe mwenye GDP kubwa mfano Israel mafuta litamoja ni around 5500...

GDP ni ujinga tu..
 
Watu wengine ukiwaambia ni Wajinga wanakasirika wakati wanajua kabisa hawajui kitu chochote!!

Hapo umeambiwa watu walioisaidia Iran kutengeneza hayo makombola wewe unasema uongo sasa si useme ukweli wako?
Unaelewa Iran ndio inaisaidia North Korea kutengeneza hypersonic, au na hilo hufahamu?
 
Watu wasio na uelewa wanaipaisha Iran kwa sifa ambazo ni uwongo mtupu.

UKweli ni kwamba, wakati mataifa menggi yanasonga mbele, Iran inazidi kudidimia siku hadi siku, kuelekea shimoni. Iran ya leo ni duni kuliko Iran ya 1979.

Fikiria GDP ya Iran ya mwaka 2012 ilikuwa dola bilion 644, halafu GDP ya 2025 ni dola bilion 341. Yaani watu wanaongezeka, thamani ya pesa, ikiwemo dola, imeshuka thamani, halafu pato la Iran ni karibia nusu ya pato lake la la miaka 13 iliyopita. Lakini wajinga na wanafiki wanasema Iran inasonga mbele. Iran isingependa kuibembeleza Marekani wakae waongee, lakini hali ngumu ndiyo inayoifanya kuinyenyekea Marekani.
Kuhusu anguko la uchumi wa Iran, soma hapa:
The total GDP of Iran has experienced significant volatility and a long-term decline in global standing from 1972 to 2025, driven by the 1979 revolution, the Iran-Iraq war, and decades of international sanctions. From being a rapidly growing economy in the early 1970s, Iran has seen its global economic ranking drop from around 18th in the 1970s to 44th by 2025.

Iran's nominal GDP in 2012 was $644 billion

Iran's nominal GDP in 2025 is projected to be approximately $341 billion to $375.6 billion USD, according to 2025 International Monetary Fund (IMF) and other estimates. The economy faces a significant slowdown, with growth rates expected to be nearly zero.
 
Usitufanye wote humu ni wajinga kama wewe hebu angalia hapa chini uone harafu uje hapa Ubwabwa Je vizuri
 

Attachments

  • IMG_4918.jpeg
    168.1 KB · Views: 20


Unapoonekana umekosa akili na maarifa ni pale unapoona watu wote Duniani hawana akili usipokuwa wewe tu. Hicho mara nyingi ni kipimo cha ukichaa. Vichaa wengi huwa wanajiona wana akili kuzidi watu wote. Wataalam wote wa Ulimwengu huu wanakubaliana kuwa kipimo cha maendeleo ndani ya nchi ni nominal GDP. Unapopima maendeleo ya watu, na kufanya ulinganifu na Taifa jingine, unaangalia GDP per capita au PPP.

Ndani ya nchi, GDP inaposhuka, GDP per capita inashuka na PPP nayo inashuka.

Kushuka kwa GDP ya Iran, ndiyo kumesababisha kushuka kwa PPP ya watu wake, mpaka kuamua kuamdamana, halafu wewe uliyejificha huko madongokuinama unajifanya unajua ustawi wa Wairan kuliko Wairan wenyewe. Iran kwa sasa kuna watu wengi ambao hawawezi hata kupata milo mitatu kwa siku kwa sababu hawana uwezo wa kifedha.

Based on reports and estimates from 2024 and late 2025, a significant portion of Iran's population faces severe food insecurity, with millions struggling to secure adequate daily nutrition.

  • Extreme Poverty (Food Poverty): Approximately 4 to 5 million Iranians are trapped in extreme poverty, meaning their income is insufficient to cover basic daily food needs.
  • Food Insecurity Rates: Some studies have estimated that nearly 41% of Iranians suffer from moderate to severe food insecurity, with 36 million people unable to afford a healthy, nutritious diet.
 
Aksante sana kwa kutoa shule ya Bure!!!!
 
Ana miaka 86 sasa Khamenei, atatokea Khamenei mwingine...
Khamenei mwenyewe kajikatia tamaa kaanza na kutoa Wosia nani atachukua kiti chake pindi atakapoondolewa madarakani.

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ameripotiwa kuandaa mipango ya dharura iwapo atauawa wakati wa shambulio linalowezekana la Marekani au Israeli, kulingana na ripoti ya New York Times. Mipango hiyo inajumuisha amri za urithi zilizopangwa na minyororo ya amri ya dharura ili kuhakikisha uhai wa utawala huo.

Ripoti hiyo inasema Ali Larijani, ambaye ni mwaminifu kwa muda mrefu, amepandishwa cheo hadi nafasi kuu ya utawala, akisimamia usimamizi wa migogoro, diplomasia ya nyuklia na mipango ya wakati wa vita huku Iran ikiweka jeshi lake katika tahadhari kubwa huku mvutano wa kikanda ukiongezeka.
 

Attachments

  • IMG_4920.jpeg
    92.4 KB · Views: 25
Kaka,kushindwa kwa mifumo ya ulinzi haimaanidhi kuwa haifanyikazi tatizo ni kuzidiwa.

Ukweli ubakie kuwa ukweli Muhajemi ana akili na nguvu kushindwa huyo Marekani(Marekani pia kawatumia sana waisrael na wagiriki kutawala huu ulimwengu).
 
Kaka,kushindwa kwa mifumo ya ulinzi haimaanidhi kuwa haifanyikazi tatizo ni kuzidiwa.

Ukweli ubakie kuwa ukweli Muhajemi ana akili na nguvu kushindwa huyo Marekani(Marekani pia kawatumia sana waisrael na wagiriki kutawala huu ulimwengu).
Kuwadanganye wajinga wenzako tu Kwani kuzidiwa maana yake nini?
 
Haimaanishi ubovu,ni uchovu wa Mfumo wa kudungulia hayo mabomu.

Iron Dome ilizidiwa je,ile ni tenolojia ya Muhajemi?
Ujinga mtupu unakusumbua Kwani uchovu wa mifumo maana yake nini?

Iron dome ilizidiwa nani aliyekudanganya? Iron dome ni teknolojia ya nani? Hebu rudi a tena nikusikie!!!!!!!
 
Nikikumbuka kibri cha Sadam Hussein kipindi kile namwonea huruma Iran!! Sadam alivimba hivi hivi nakujigamba kwamba anakombora za Scad, Kwamba akivamiwa atajibu kwa kuzifuta nchi zote zitakazomsaidia U. S. A. Akapewa mda ajitafakari na kuchukua uamuzi sahihi akavimba kwa kujiona mkubwa, mda ulipoisha alichapika hadi kurusha hizo Scad hakuweza.
 
Korea kusini hawana silaha za nyuklia.
 
UKweli ni kwamba, wakati mataifa menggi yanasonga mbele, Iran inazidi kudidimia siku hadi siku, kuelekea shimoni. Iran ya leo ni duni kuliko Iran ya 1979.
Hapana.
Weka ushabiki wa aina ile nyingine pembeni na tazama uhalisia katika hali ya uwazi.

Maneno haya uliyoandika hapa na kule kwingine yanakufanya mshabiki wa upande mmoja kwa sababu zisizohusiana kabisa na maswala yaliyopo kujadiliwa..

Sikubaliani na maswala mengi ya kiutawala na kitamaduni ya nchi hiyo; lakini natambuwa wazi uwezo mkubwa wa taifa hilo na watu wake.

Hizi 'propaganda' tunazolishwa na hawa tunaowasujudia kiasi hata cha kujitoa ufahamu kabisa hazifai.

Tuwe watu huru, na wakweli wa kujuwa yapi ni sahihi na yapi ni uongo tunapolishwa propaganda hizo.

Sasa tuseme hiyo Iran sasa hivi inataka kupigwa kwa vile GDP yake imekuwa mbaya zaidi ya 1979; au kuna sababu zingine za msingi zaidi, ambazo tukizijuwa pengine hatutakubaliana na hao wanaotulisha hizi prpaganda za kutupotosha?
 
Ndiyo tyranny ya elimu mpachiko hii, haimpi mtu hekima!
Hata kama tukikubaliana nawe kuwa uchumi wa Iran umesinyaa... ni kwa sababu gani? Kwani hujui Marekani inafanya kila kitu, hadi hata kumwekea vikwazo anayenunua kwa anayenunua bidhaa za Iran (three~tier sanctions: yaani kama wewe ukinunua simu Tanzania iliyotengenezwa na Iran, wewe pia unawekewa vikwazo!) haijawahi kutokea wala haitawahi kwa nchi yoyote nyingine! Hata katika kilele cha uadui wa America na Soviet walikuwa wanauziana ngano!
Kiasi dunia nzima ina woga wa kukaribia products za Iran, licha kununua....halafu waandika upuuzi kana kwamba uchumi umeanguka kwa sababu ya corruption! Vikwazo vya kishetani ilivyowekewa Iran, kama ni nchi yoyote duniani ingekuwa kwenye magoti, hata Uingereza na miye nimeishi Uingereza. Halafu unakuja....
Cha ajabu Marekani kufanya haya ni illegal katika sheria za UN, World Trade nk. Lakini inafannya.
Sasa kama ukitaka elimu; wala uchumi wa Iran si $375 billion (ambao hata hivyo ni zaidi ya Tanzania, Kenya na Ethiopia pamoja), hii inaitwa 'currency manipulation' kwamba sarafu ya nchi inakuwa degraded makusudi ili kuwakatisha tamaa wafanyibiashara waone haina thamani. Zote hizi ni mbinu za kuisakama Iran. Swali la kujiuliza, ni kwa sababu gani uadui kama huu. Iran haina uadui huo kwa Marekani wala haina sababu. Pia Marekani haipati faida yoyote kwa kufanya hivi, bali yapata hasara.
Nikuachie uje na jibu, kwa nini Marekani ikawa na uadui usio na kifano kama huu?
 
Iran hakuwahi kuwa Chaguo la kwanza kabla ya Israel.

Ni kweli alikuwa na interest ila sio kwa kiasi hicho.
Basi hujui au ulikuwa mtoto. Tangu miaka ya 60 hadi mapinduzi ya Kiislamu Iran ilikuwa ya kwanza kupata ndege mpya za kivita za Marekani, kama ilivyo Israel hivi sasa, hata kabla ya allies wa karibu kama Uingereza, Ujerumani nk. Iran ilipata F 14, state of the art wakati huo, kabla ya mshenzi yeyote. Hivyo ndivyo ilivyokuwa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…