Wakuu kuanzia sasa na kuendelea nikiona mtu anapigania usimba na uyanga najitolea kumpeleka Mirembe

Wakuu kuanzia sasa na kuendelea nikiona mtu anapigania usimba na uyanga najitolea kumpeleka Mirembe

Yes, nampeleka mirembe kwa gharama zangu japokuwa mimi sina uwezo mkubwa kifedha lakini niko tayari kuzikopa popote ili nimsaidie mtanzania mwenzangu mwenye ugonjwa wa akili maana nikimwacha anaweza akaanzisha makaazi yake dampo.

Nayasema haya kwa sababu watanzania wengi ukiwasikiliza wakiizungumzia vilabu vya Simba na yanga unaweza ukadhani kuwa labda hawana ubongo bali samadi katika mafuvu yao. Mtu yuko tayari kukiita cheupe cheusi, watu wamejaa biasness na baadhi yao wako humu humu JF.

Hizi ngonjera za Simba na yanga imenikasirisha na najua zimesababishwa na nguvu kubwa ya ushawishi ya viongozi wa Serikali katika soka la Tanzania jambo ambalo binafsi nalichukulia kama ukumanyoko na ningefurahi fifa ingeifungia Tanzania kwa miaka zaidi ya mitano ili tujifunze.

Ngoja nisiendelee.......
Simna na yanga ni mtaji wa ccm kwahiyo tunapaswa kutulia tu
 
Yaani ilitakiwa mpaka karia Atoke kabisa, ikiwezekana Simba na Yanga zvunjwe zitengenezwe timu mpya kabisaaa, yaani tuanze upyaa
Mkuu unakumbuka sakata la FEISAL lilivyoenda?

Japo Mimi naishabikia Simba lakini FEISAL alitakiwa awe anakula sukari hadi leo lakini busara za mama zilimpatia msamaha tu.
 
Kuna mmoja nilikua namsikiiliza Jana kwenye redio Moja hivi ya kipumbavu, anaishukuru serikali.ya awamu ya sita chini ya mama Samia kwa kuwezesha derby kuchezwa
Duh, ila watu wengine wameoza ubongo 😅
 
Binafsi Bongo sina timu, ila zinapokutana Hizi timu mbili huwa naburudika, kwa nini... napenda kuona lile vibe wanalokuwa nalo mashabiki wa hizi timu mbili....ila zinaposhiriki mashindano ya kimataifa huwa nakuwa upande wao

Kilichoharibu soka la bongo ni siasa, mpira na siasa ni vitu viwili tofauti na hii ndio sababu inayonifanya nisiwe na timu
 
Hizi ngonjera za Simba na yanga imenikasirisha na najua zimesababishwa na nguvu kubwa ya ushawishi ya viongozi wa Serikali katika soka la Tanzania jambo ambalo binafsi nalichukulia kama ukumanyoko na ningefurahi fifa ingeifungia Tanzania kwa miaka zaidi ya mitano ili tujifunze.❗❗❗📌📌📌🔨🔨🔨
Naunga mkono hojaa
 
Hizi ngonjera za Simba na yanga imenikasirisha na najua zimesababishwa na nguvu kubwa ya ushawishi ya viongozi wa Serikali katika soka la Tanzania jambo ambalo binafsi nalichukulia kama ukumanyoko na ningefurahi fifa ingeifungia Tanzania kwa miaka zaidi ya mitano ili tujifunze.❗❗❗📌📌📌🔨🔨🔨
😄 🤣 😂
Dini.
Siasa.
Mpira.

Bora nijifungie chumbani nianze kuangalia album yangu ya picha.

Vinaturudisha nyuma sana sisi kama watanganyika.
 
Back
Top Bottom