amu
JF-Expert Member
- Aug 8, 2012
- 16,132
- 31,149
Sasa mwanaume mwenye kipato kidogo wa nini jamani????Oohh kwahiyo hata mwanaume awe na kipato kidogo kuliko mkewe bado atatakiwa kusimamia majukumu yake yote like kulipa bills na kumhudumia mkewe na watoto wake? Na asiulize kabisa kipato cha mke wake kinaenda wapi right?
Wanaume wote waliojaaa wenye hela na kujielewa jamani.
Chaiiiii mwanamke utalipaje bills jamani???kuhudumia nyumba na watoto ni jukumu la mwanaume.
Kamwe usichukue majukumu yake.
Mwache apambane alete chakula mezani.
Jukumu la mwanaume kuhakikisha mke na watoto wanakula, kulala na kupata mahitaji muhimu ikiwemo elimu bora kwa watoto.
Mwanamke kulipa bills na kusimamia majukumu hii inamuondolea confidence mwanaume na ndo chanzo cha migogoro kama ndoa ya mleta mada.
Kazi ya kipato cha mwanamke ni moja tu kusaidia kuwa msaidizi yaani kujazilia sehemu ndogo sana, kuweka akiba pale mume siku akibanwa unampiga tafu, kuwa huru na kipato chako pia nikiamua kuwatoa out including mume ninatoka nae nalipa bills vizuri tu tunaenjoy maisha. Yeye pia ni binadamu iko siku atakwama, anaweza ugua au kupata matatizo mda mrefu kipato changu na akiba nilizoweka zitatusaidia tusongeshe gurudumu la maisha.
Kwanza kwa kumbukumbu zangu wanaume wasiokuwa na hela wana shida sana,mleta mada ni mmojawapo alizidiwa elimu na kipato na mke wake, ikamuondolea uanaume wake na kupelekea maugomvi na talaka.
Wadogo zangu waepukeni wanaume wasio na kipato hawana jema hata kidogo atakunyanyasa kwa kipato chako, atakudhalilisha kwa kipato chako yaani atapambana kuhakikisha unakuwa chini kama yeye kiuchumi na kifikra.