Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Wale tuliokosea kuoa tukutane hapa

Khaa kwahiyo ukiwa Mbeya hiyo hela huwezi kutuma? Ndiyo muone raha ya kulazimisha mtu afanye majukumu yake hata kama haiwezekani kwa muda huo yaani that is exactly how women feel pale mumeo anapokuambia "mimi hata kama unafanya kazi na unarudi usiku majukumu yako lazima ufanye"!
Majukumu ni vitu basic ina maana kwako watu hawatakula? Mtaishi katika nyumba chafu? Kutiwa hutatiwa nimeoa mke wa kazi gani?

Mbona vitu vingine ni basic sana yani mi ntapiga makofi mpaka urudi kwenu ukajifunze adabu sipendi mwanamke mjuaji kabisa na jueri! Ombea upate mwanaume nyoro nyoro tu.

Kuumwa ni emergency hamna anayepanga kwamba badae ntaumwa niweke elfu 50 kwa ajili ya matibabu. Inaweza tokea mtu yuko kijijini saa 8 za usiku hamna access ya kutuma pesa. Utaacha mtoto afe?
 
Hamna cha ubinafsi mama zetu walifanya mambo yote kwenye familia bila kulalamika. They did the needful usafi wa mazingira na upishi bila kusahau kulea na still kazini walienda.

Nimeishi na mama wa kambo nikaona wanawake wajinga jinsi walivyo hovyo. Mama ni mchafu, usafi anaojua ni kuamka kupiga mswaki na kuoga tu. Kudeki mpaka mzee amkodishe mtu aje kufanya usafi jumba lina mavumbi pazia toka maza afariki 20 yrs ago mpaka last year mzee ndo kafanya renovation ya nyumba akaweka pazia mpya [emoji28] on top of all mama ni msomiless na mshirikina sana. Kupika anataka apike ila vyombo aoshewe hahahah atalalamika balaa completely useless woman ni vile mzee ndio alijichanganya tu tunaheshimu uamuzi wake ila umetugharimu sana.

Sasa unapoongea unayoongea unazidi kuntia nyongo tu sababu naona ndio wale wale tu.
Hivi kwanini huwa mnapenda kuwatolea mifano bibi zetu je mnajua walivyokuwa wanajisikia mioyoni mwao kufanyishwa kazi zote hizo na kubeba majukumu yote hayo mnafikiri walikuwa wanapenda? Ni vile tu hawakuwa na sauti kwa sababu mila na desturi zetu zote zilikuwa zinatungwa na wanaume hivyo waliamua kujipendelea kwenye masuala ya majukumu!

Kwahiyo kumbe ninyi hamjali mwanamke anajisikiaje mnachotaka ninyi ni mambo yaende tu yaani kwamba kwenye ndoa furaha ya mwanamke haina umuhimu akifurahi mwanaume inatosha? Huo kama siyo ubinafsi ni nini?
 
Ndio maana nikasema hilo lilifanya kazi kwa babayako ila ukiolewa utaratibu unaokwenda kuufuata ni wa kwa mume wako sio wa ulipotoka.

Ndio maana huwa mnapewa sifa ya kupelekesha sana wanaume huko kanda ya green city.
Wewe jamaa mbinafsi sana! Kwa hali hiyo hata wanawake mtawaona wabinafsi tu ningekuwa mimi natimiza majukumu yangu yote sitataka uguse hata kijiko ila haki ya nani hutakaa uione hata mia yangu yaani shida yoyote ikitokea ndani ya nyumba utapigiwa simu hata kama uko hospitali umelazwa!
 
Hivi kwanini huwa mnapenda kuwatolea mifano bibi zetu je mnajua walivyokuwa wanajisikia mioyoni mwao kufanyishwa kazi zote hizo na kubeba majukumu yote hayo mnafikiri walikuwa wanapenda? Ni vile tu hawakuwa na sauti kwa sababu mila na desturi zetu zote zilikuwa zinatungwa na wanaume hivyo waliamua kujipendelea kwenye masuala ya majukumu!

Kwahiyo kumbe ninyi hamjali mwanamke anajisikiaje mnachotaka ninyi ni mambo yaende tu yaani kwamba kwenye ndoa furaha ya mwanamke haina umuhimu akifurahi mwanaume inatosha? Huo kama siyo ubinafsi ni nini?
Tatizo wamama wamelega lega kwenye kuwapa mafundisho sana watoto wa kike wa kileo. Bibi zenu waliambiwa kabisa wanakoelekea na majukumu yao unyagoni yaliainishwa.

Kumbe furaha yake ni kuona mumewe anadeki na kupika au sio 😅? Jiulize tu mwanao wa kumzaa ukakuta anapelekeshwa kama gari bovu na kupigishwa deki na kukaripiwa kama msukule utajiskia raha sababu mwanamke wake anafurahia kuona mumewe akifanya hayo.

Nafikiri kuna haja ya kurudisha tamaduni za unyago tumepotoka sana kama taifa.
 
Kufanywa kwa upendo sio swala kabisa hata mie nikiguswa nakupiga tuff ila ikishageuka malumbano ya hoja tabu inaanzia hapo!

Mfano tuna mtt mdogo nafanya kumbeba nambembeleza wewe unafanya majukumu mengine nini mbaya hapo? If i do it kwa mguso binafsi sio swala ila ondoeni ile notion eti kama mie nakusaidia hela ukikwama kwanini usikoke kuni upike?

Huo ni upumbavu na ukosefu wa adabu na kwangu makofi utakula.
Khaa siyo ukosefu wa adabu wala upumbavu bali ni mgawanyo wa majukumu tu kwani wewe mimi pesa yangu ya nini? Hata mimi niache nitoe pale nitakapoguswa tu asee!
 
Wewe jamaa mbinafsi sana! Kwa hali hiyo hata wanawake mtawaona wabinafsi tu ningekuwa mimi natimiza majukumu yangu yote sitataka uguse hata kijiko ila haki ya nani hutakaa uione hata mia yangu yaani shida yoyote ikitokea ndani ya nyumba utapigiwa simu hata kama uko hospitali umelazwa!
Heheheheh nikwambie kitu karma, naomba don’t ever think of getting married please wala kuzaa naomba usizae sio kwa ubaya bali tu itakusaidia sana. Una mentality ngumu sana sababu hutakaa kwenye ndoa for more than a year hata ukiamua tu kuolewa incase utapata mwanaume shababi! Unless una joke ila kama haya unayoandika yanatoka rohoni nakuonea imani sana.

Ndoa itakayodumu kwako ni ya kumlea mwanaume kama ben 10 au kama shilole anavyolelea wanaume vile. I doubt kama hilo utaliweza ndio maana nasema bora usihangaike na mambo ya ndoa.

Just nenda kwa vituo vya watoto yatima fata taratibu get a child anza kumtunza kama mwanao don’t waste nguvu zako ama mayai ya mwanaume kuzaa mtoto ambaye mtakuja kumpa shida tu.
 
Khaa siyo ukosefu wa adabu wala upumbavu bali ni mgawanyo wa majukumu tu kwani wewe mimi pesa yangu ya nini? Hata mimi niache nitoe pale nitakapoguswa tu asee!
Wewe unapenda ligi! Ishi mwenyewe tu kwa usalama wako na afya yako maana ukipata mume mwenye calibre ya Magufuli atakutoa meno mapema sana.
 
Majukumu ni vitu basic ina maana kwako watu hawatakula? Mtaishi katika nyumba chafu? Kutiwa hutatiwa nimeoa mke wa kazi gani?

Mbona vitu vingine ni basic sana yani mi ntapiga makofi mpaka urudi kwenu ukajifunze adabu sipendi mwanamke mjuaji kabisa na jueri! Ombea upate mwanaume nyoro nyoro tu.

Kuumwa ni emergency hamna anayepanga kwamba badae ntaumwa niweke elfu 50 kwa ajili ya matibabu. Inaweza tokea mtu yuko kijijini saa 8 za usiku hamna access ya kutuma pesa. Utaacha mtoto afe?
Hivi mke aliyeajiriwa full time anayeenda kazini asubuhi na kurudi usiku anapika saa ngapi, anafua saa ngapi, anaosha vyombo saa ngapi na anasafisha nyumba saa ngapi? Unavyoongea hivyo utadhani option ya housegirl haipo!
 
Negotiation za jinsi utakavyo handle majukumu yako na housegirl hazi involve mume! Mie najua mke wangu lazma anipikie, ahakikishe usafi wa mazingira, afue na kunyoosha na mengineyo. Kama mtagawana kazi na housegirl kwangu sio ishu ila nataka kila kitu kiwe sawa.

Mie kazi yangu kuhakikisha familia imekula na utilities zinapatikana maji, umeme, ving’amuzi na kadhalika.
 
Tatizo wamama wamelega lega kwenye kuwapa mafundisho sana watoto wa kike wa kileo. Bibi zenu waliambiwa kabisa wanakoelekea na majukumu yao unyagoni yaliainishwa.

Kumbe furaha yake ni kuona mumewe anadeki na kupika au sio [emoji28]? Jiulize tu mwanao wa kumzaa ukakuta anapelekeshwa kama gari bovu na kupigishwa deki na kukaripiwa kama msukule utajiskia raha sababu mwanamke wake anafurahia kuona mumewe akifanya hayo.

Nafikiri kuna haja ya kurudisha tamaduni za unyago tumepotoka sana kama taifa.
Hebu acha kuropoka vitu ambavyo havipo unakwama wapi? Kwahiyo wewe kumsaidia mkeo hizo kazi ni hadi akukaripie au kwanini useme unapigishwa deki na siyo unapiga deki?

Furaha ya mwanamke ni kuona kila mtu anatimiza majukumu yake bila kuingiliana! Ila inapotokea wewe unataka yako akusiadie na yeye lazima atahitaji msaada toka kwako!

Ila wanaume mnataka mkeo afanye majukumu yake yote na yako akusaidie ila wewe yake kufanya unasingizia eti 'anakupigisha deki'! Sasa hapo hiyo furaha yake inatoka wapi?
 
Heheheheh nikwambie kitu karma, naomba don’t ever think of getting married please wala kuzaa naomba usizae sio kwa ubaya bali tu itakusaidia sana. Una mentality ngumu sana sababu hutakaa kwenye ndoa for more than a year hata ukiamua tu kuolewa incase utapata mwanaume shababi! Unless una joke ila kama haya unayoandika yanatoka rohoni nakuonea imani sana.

Ndoa itakayodumu kwako ni ya kumlea mwanaume kama ben 10 au kama shilole anavyolelea wanaume vile. I doubt kama hilo utaliweza ndio maana nasema bora usihangaike na mambo ya ndoa.

Just nenda kwa vituo vya watoto yatima fata taratibu get a child anza kumtunza kama mwanao don’t waste nguvu zako ama mayai ya mwanaume kuzaa mtoto ambaye mtakuja kumpa shida tu.
Haha kuishi na mwanaume naweza vizuri tu mradi kila mtu anatimiza majukumu yake ipasavyo! Inapokuja kwenye suala la watoto wangu nitagharamia ila siyo wewe mume kama mume au chochote kinachohusu nyumba hapo hapana!
 
Hebu acha kuropoka vitu ambavyo havipo unakwama wapi? Kwahiyo wewe kumsaidia mkeo hizo kazi ni hadi akukaripie au kwanini useme unapigishwa deki na siyo unapiga deki?

Furaha ya mwanamke ni kuona kila mtu anatimiza majukumu yake bila kuingiliana! Ila inapotokea wewe unataka yako akusiadie na yeye lazima atahitaji msaada toka kwako!

Ila wanaume mnataka mkeo afanye majukumu yake yote na yako akusaidie ila wewe yake kufanya unasingizia eti 'anakupigisha deki'! Sasa hapo hiyo furaha yake inatoka wapi?
Huo ni upumbavu wewe ila ipo siku utanikumbuka na kuona dunia kumbe sivyo ambavyo ilivyo kichwani mwako!

Mwanamke anayejitambua hawezi ruhusu eti mumewe aanze kufanya mambo ya kike kike eti sababu anamsaidia. Nashukuru mungu mtu niliye naye anaweza hata kulipa ada ya mtoto na still akaendelea kuniheshimu kama mume. She feel responsible kama mwanamke na mama wa mtoto. Hata siku moja hawezi kuniambia eti deki au osha vyombo.

Huwa nashangaa unapoonge vitu ambavyo kama haviwezekani kumbe ni mentality ya kipuuzi tu ulio nayo ndio inakufanya uone kuwa ukifanya kitu lazma na mwanaume naye umhenyeshe tu ili ku correspond kujitoa kwako.
 
Negotiation za jinsi utakavyo handle majukumu yako na housegirl hazi involve mume! Mie najua mke wangu lazma anipikie, ahakikishe usafi wa mazingira, afue na kunyoosha na mengineyo. Kama mtagawana kazi na housegirl kwangu sio ishu ila nataka kila kitu kiwe sawa.

Mie kazi yangu kuhakikisha familia imekula na utilities zinapatikana maji, umeme, ving’amuzi na kadhalika.
Basi ndiyo muache kulalamika pale mnapoona housegirl anafanya! As long as mke anasimamia na kila kitu kinaenda sawa hayo mengine hayawahusu we nenda kafunue tu mahotpot ukale ushibe ukimaliza uende chooni kisha ulale!
 
Unaona ulivyo na tatizo? Kwahio mwanaume akafunue ma hotpot wewe ukiwa jamii forums sio! Aisee mtoto wangu siwezi kubali aoe utopolo wa mwanamke ni lazma alete wachumba niwakague kwa siri na kisha ntamwambia huyo ndie oa.
 
Na kuliko kuolewa na mwanaume mzigo haki ya nani bora niwe single mother hata wa watoto kumi! Na hao watu watakaonisema wahakikishe nao wakifa wanaenda mbinguni!
Kumbe umeshajijua.

Ni vizuri umeshajijua wewe ni wa Aina gani.

All the best
 
Unaona ulivyo na tatizo? Kwahio mwanaume akafunue ma hotpot wewe ukiwa jamii forums sio! Aisee mtoto wangu siwezi kubali aoe utopolo wa mwanamke ni lazma alete wachumba niwakague kwa siri na kisha ntamwambia huyo ndie oa.
Unapoteza muda wako bure hapo.

Hao ndio Aina ya wanawake MKE wako akiwa Ni rafiki Yake lazima familia au ndoa yako ipitoe changamoto
 
Back
Top Bottom