[emoji23][emoji23][emoji23]
Dah mkuu umetoa povu mno.
Muheshimu mama yako huyo licha ya mapungufu yake yote.
Mimi nimekulia maisha ambayo wazazi wote wawili wanatafuta na mama anacontribute kwa kiwango kikubwa..yaani kuna muda unakuta mzee hana basi mama ndiye anaendesha familia na kusomesha watoto.
Alitoa kwa moyo na hakuwahi kuona kama anaonewa.
Kazi zilifanywa kwa kusaidiana...baba anaamka anakamua maziwa na kufagia uwanja,mama anafanya usafi wa ndani,anaandaa chai na chakula.
Wote wanaenda kazini.
Hata ikifika jioni mzee akiwahi,basi mtakuta amewasha moto,mama anakuja kuendelea.
Baba alifanya kwa moyo na hakuwahi kuona kama ni adhabu.
Kipindi mama amesafiri tukiwa wadogo basi mzee alikuwa anatupikia.
Sasa ninashangaa huu utaratibu ambao watu wamejiwekea wa kutaka kukaa tu kama walemavu.
Kiufupi sikuwa na wazazi wavivu.