Wana-CCM wajitokeza kuchukua fomu ya kutia nia ya kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la JMT. Yupo Dkt. Tulia na Masele
Huyu Tulia baada ya Statement zake za leo tutegemee Bunge kutokuwa tu a Rubber Stamp bali hio Stamp itakwenda kabisa Ikulu ili wamalize huko huko hakuna haja hata ya ku-consult Bunge
Spika ni Tulia!. Sio mimi, ni sauti!.
P
 
Tulia hatakiwi kugombea, anatakiwa aendeshe mchakato wa kumpata spika.

Sasa anaachia kiti alichopewa kikatiba kugombea kingine bila kuwepo anayekaimu...
Spika ajaye ni Dr. Tulia Akson!.
Sio mimi ni sauti hii...
P
 
Aliyewahi kuwa Makamu wa kwanza wa Rais katika Bunge la Afrika (PAP), Stephen Masele na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson wamechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania...
Dkt Tulia ackson ni Kiongozi mzuri na makini Sana. Anajua vitu vingi na yupo very smart kwenye speech zake. Akiongea unasema kweli kiongozi ameongea.
 
Dr Tulia Ackson.
Ni msomi
Ni mwanasheria
Ana uzoefu sasa wa u spika.

Bungeni sasa si mahali pa kubahatisha.
Tunahitaji mtu anayeweza kuitafsiri katiba na wakati huo huo kuisimsmia serikali.

Wabunge wa CCM msifanye kosa.
 
Dkt Tulia ackson Ni Kiongozi mzuri na makini Sana. Anajua vitu vingi na yupo very smart kwenye speech zake. Akiongea unasema kweli kiongozi ameongea.

Mbona Jana kaongea pumba. Wala Hana uongozi wowote zaidi ya kubebwa.
 
Alitoa ufafanyzi wa executive kadiri ya Katiba yetu,hukusikia au nongwa?

Pili Kazi ya spika sio kufarakana na kuchonganisha mihimili na wananchi

Mimi nashangaa wanaomtetea Tulia. Mimi tangu akubali kuwafuga wale COVID 19 nilimtoa maana.
 
Sio tuu msomi lakini pia ana uzoefu wa kuongoza Bunge na ni mwanasheria.

Ukiacha hilo ni mwanamama ngangari kweli kweli ambae atalinda maslahi ya ccm na wananchi.

Acha kupotosha, Bunge sio taasisi ya chama ambapo speaker anaenda kulinda maslahi ya CCM. Bunge ni chombo Cha kuwakilisha wananchi katika maamuzi ndio maana wabunge wanachaguliwa na wananchi. Hiyo kazi ya kulinda maslahi ya CCM bungeni ni uhuni Kama uhuni mwingine.
 
Acha kupotosha, Bunge sio taasisi ya chama ambapo speaker anaenda kulinda maslahi ya CCM. Bunge ni chombo Cha kuwakilisha wananchi katika maamuzi ndio maana wabunge wanachaguliwa na wananchi. Hiyo kazi ya kulinda maslahi ya CCM bungeni ni uhuni Kama uhuni mwingine.
Kuns watu vichwa vyao vimejaa mlenda sana
 
Aliyewahi kuwa Makamu wa kwanza wa Rais katika Bunge la Afrika (PAP), Stephen Masele na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson wamechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania

Mtu mwingine aliyechukua fomu ni Patrick Nkamaha. Mchakato huu umeanza baada ya CCM kutangaza kutaka muwakilishi kugombea nafasi iliyoachwa na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai

  • Patrick Nkamah
  • Stephen Masele
  • Tulia Ackson Mwansasu
  • Godwin Kunambi
  • Hamidu Ubaidi Chamani
Katika makosa na kosa litakalofanywa na CCM ni kumchagua Tulia kuwa tena spuka. Mihimili ni mitatu miwili inakwenda kubwebwa na wamama na mhimili wa tatu upo hai hai kuchukuliwa na wamamama.
 
Acha kupotosha, Bunge sio taasisi ya chama ambapo speaker anaenda kulinda maslahi ya CCM. Bunge ni chombo Cha kuwakilisha wananchi katika maamuzi ndio maana wabunge wanachaguliwa na wananchi. Hiyo kazi ya kulinda maslahi ya CCM bungeni ni uhuni Kama uhuni mwingine.
Sio taasisi ya chama ila waliomo ndani ni wanachama wa vyama kwa hiyo Wana wajibu wa kulinda interests za chama Chao.
 
Mchungaji na Nabii Komando Mashimo ambaye hupatikana zaidi stendi ya Mbezi kupitia ukurasa wake wa Instagram ametangaza nia yake ya kugombea nafasi ya "sipika" wa Tanzania. Pia aliitag ukurasa wa bunge kuonyesha msisitizo. Kama akishinda itakuwa mara ya kwanza bunge letu kupata spika anayetoka kwenye taasisi za dini.

20220111_112052.jpg
 
Back
Top Bottom