Wana ndoa wengi siku hizi wanaishi kama maadui. Tatizo ni nini?

Wana ndoa wengi siku hizi wanaishi kama maadui. Tatizo ni nini?

Kifaru86

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2017
Posts
1,734
Reaction score
3,822
Japo sio wote ila wana ndoa wengi siku hizi wanaishi kama maadui tatizo ni nini lakini yaani. Kuna watu wapo ndani ya ndoa lakini wakiwa ndani hawaongeleshani

Kuna watu wapo ndani ya ndoa kila siku ugomvi vikao vya kifamilia vya usuluhishi haviiishi. Kuna watu wapo ndani ya ndoa wanaona bora kuchelewa kurudi nyumbani ili akose tuu muda wa kuongea na mwenzie

Kuna watu wapo ndani ya ndoa wameshafika hatua hadi kupelekana mahakamani. Wengine wapo ndani ya ndoa kila siku ligi hakuna anayekubali kushidwa kila mmoja anajiona sahihi kuliko mwenzie

Wengine wapo ndani ya ndoa hata kushare kitu chake na mwenzake hataki kama ni gali hataki kabisa mwenza wake akitumia gali lake. Wengine wapo ndani ya ndoa hata tendo la ndoa hawashiriki tena usishangae wanalala vyumba tofauti tofauti ili mradi amnyime mwenzie

Je, katika haya yote shida ni nini lakini?
 
Kwamba kwenye pesa hakuna matatizo!?!..


Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
Kwenye pesa hakuna matatizo Kuna changamoto ndogo ndogo na penyewe zikitokea mna kwea pipa mpaka Dubai date moja mnarudi nyumbani mna vibe penzi linaendelea .....!

Sasa wewe unakaa chumba kimoja tandale kwa tumbo ,joto Kali mpaka ndani ,kutoka tu out ni mtihani ,daily unakula wali mbegu ...unataka mwanamke akuvumilie [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Unachosema ni kweli mm nimekua kwenye familia yenye migogoro nipo chuo ila naishi home niseme tu wazazi wangu upendo kati yao ulishakufaaaaa kitambooo sanaaaaa tangu niko primary mpaka sasa nipo chuo yani ugomvi daily ingekua ni amri yangu basi ningevunja ndoa ya wazazi wangu maana ni wanaishi tu siku ziende kuna kipindi walizinguana mama akaondoka nyumbani kama mwezi mzee akalazimisha arudi nikamwambia si kila mtu aendelee na maisha yake maana unachofanya ni Kuangalia movie ya titanic mara ya pili na kutegemea meli isizame itazamaa tu


Mama akarudi nyumbani amani ilirudi kwa wiki mbili tu afu vita ikaendelea kama kawa dah jau sana na Leo tu asubuhi wamezinguana tena,mzee wangu anataka kufurahisha jamii ione yupo Kwenye ndoa kumbe ndani hamna amani.nashukuru hii migogoro yao haijani affect kisaikolojia na wala siwazi mambo yao Niko busy na mambo yangu ila nawachora tu wanavohangaika na ndoa yao naombea tu wadogo zangu wasiathirike Maana ni wadogo wako primary.


Wazazi wangu wasije wakakaa wategemee eti siku nitaleta mchumba nyumbani kumtambulisha eti nikae kabisa baba,mama huyu hapa mchumba nimemleta mumtambie maviii ya kuku na wakiona kimya wasije wakaniuliza eti mafian cartel unaoa lini haha Nitakachojibu watanyamaza wasiulize tena.

Ndugu zangu mliopo Kwenye ndoa maji yakizidi unga achaneni tu mtakufa bure

Hapa naskilizia ugomvi wa wazazi wangu baadae utaendaje maana asubuhi wamezinguana na ugomvi haujausha bado

NDOA NDOANO!!
 
Japo sio wote ila wana ndoa wengi siku hizi wanaishi kama maadui tatizo ni nini lakini yaani

Kuna watu wapo ndani ya ndoa lakini wakiwa ndani hawaongeleshani

Kuna watu wapo ndani ya ndoa kila siku ugomvi vikao vya kifamilia vya usuluhishi haviiishi

Kuna watu wapo ndani ya ndoa wanaona bora kuchelewa kurudi nyumbani ili akose tuu muda wa kuongea na mwenzie

Kuna watu wapo ndani ya ndoa wameshafika hatua hadi kupelekana mahakamani

Wengine wapo ndani ya ndoa kila siku ligi hakuna anayekubali kushidwa kila mmoja anajiona sahihi kuliko mwenzie

Wengine wapo ndani ya ndoa hata kushare kitu chake na mwenzake hataki kama ni gali hataki kabisa mwenza wake akitumia gali lake

Wengine wapo ndani ya ndoa hata tendo la ndoa hawashiriki tena usishangae wanalala vyumba tofauti tofauti ili mradi amnyime mwenzie

Je katika haya yote shida ni nini lakini
Tatizo ni porn.
 
Kwenye pesa hakuna matatizo Kuna changamoto ndogo ndogo na penyewe zikitokea mna kwea pipa mpaka Dubai date moja mnarudi nyumbani mna vibe penzi linaendelea .....!

Sasa wewe unakaa chumba kimoja tandale kwa tumbo ,joto Kali mpaka ndani ,kutoka tu out ni mtihani ,daily unakula wali mbegu ...unataka mwanamke akuvumilie [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Kwa karne hii Hakuna watu ambao mapenzi yanawatesa kama wenye pesa.
 
Back
Top Bottom