Wananchi wa wilaya ya Mlimba, Morogoro wachoma magari na vifaa vya wapima ardhi

Ningekuwa katika kamati ya kushughulikia hilo tatizo ningeweka ndani wanakijiji wote waliohusika pamoja na hao wapimaji ardhi ili ijulikane mbivu na mbichi

Kwa nini walienda kufanya kazi siku isiyo ya kazi?

Uharibifu huu umechangiwa na pande zote mbili waswekwe ndani wote
 
Huwezijua,mambo ya mulungula hayo,wapimaji watakuwa walisimama kwa mwenye nacho.
Watu wakichoka na uonevu ndio haya ya;
Mulimba
Tunduru

Hata mwaka 2018 kule Dodoma watafiti wa sijui kilimo kwanza walipoteza maisha
 
wananchi ndiyo wenye nchi.
Uchunguzi hapo uwe makini.
Mbunge wa zamani na wasasa walisimamia upande UPI
Pili Mbunge wa zamani yupo selo.
Tume iwe huru kuchunguza hiyo issue.
Wakitumia nguvu watashindwa kujua kiini pia uhasama utakuwa mkubwa zaidi
 
Uzoefu wangu. Mara nyingine katika issue kama hizi watu wawe makini sana.
Huwa inatokea: Wale wavamizi halisi bila kupepesa macho ndio wanakuwa wachochezi wakuu, halafu mambo yakipamba moto, haooo!!! Wanaenda sehemu na kusikilizia! Halafu..…."kichekoooo!!!"
 
Hapana, hawakuwa wa SUA bali walikuwa wa kituo cha utafiti Kilimo Selian Arusha. Hawa jamaa wa Melela ni wakorofi tu maana hata viongozi wa kijiji walikuwapo nao wamechezea mfueni!
 
Qubbake tatizo nini mpaka kufikia hatua hiyo?
 
Hakuna Mkuu wa Wilaya huko kuwajulisha hali halisi? Au kama kawaida yao waliamua kudharau malalamiko ya Wananchi!? Nawaunga mkono Wananchi dhuluma na udhalimu vyote vinakithiri kwa kasi ya kutisha. Sasa watakamatwa hovyo hovyo na kupewa mkong’oto wa kufa mtu kisha kabambikiwa kesi hata ambao hawakuhusika.
Kosa kubwa sana hili, inaonekana walichukulia poa au hawakuwa wanajua hali halisi.
 
Sehemu yenye mgogoro ilikuaje hao wapima ardhi kwenda bila ya kua na ulinzi?
Wanajikutaga miungu hao watu hasa ukikuta wanataka kufanya dhuluma kwa wananchi, wana majibu ya hovyo, adi wanatukana na unakuta ardhi ni ya wananchi kihalali kabisa kuna mahali nilisumbuana nao miaka 3 adi haki ikatendeka yaan hao wananchi naelewa hasira zao wangetoka na ulemavu kabisa wanakera mnoo
 
Hizo hasira wangezielekeza kwenye kudai katiba mpya wangefanya la maana sana
 
Waende na silaha kwa wananchi?

Halafu unajiita Dr ?
Sasa mkuu hilo si eneo la mgogoro? Unajua migogoro ya ardhi kati ya wawekezaji na wananchi inavyokuaga na balaa...?
Ni muhimu kujihami na ulinzi ili waweze kufanya kazi yao kwa amani kama wataalamu. Unajua kwenye hili tukio walikwepo hadi viongozi wa kijiji ila na wao walidundwa vile vile na hao wananchi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…