Bila uoga, Wananchi wengi wamejitokeza kuandika comments zenye ujumbe wa 'No Reforms, No Election' chini ya post ya salamu za kheri ya Sikukuu ya Eid al-Adha zilizotolewa na Rais Samia kupitia mitandao ya kijamii.
Your browser is not able to display this video.
Badala ya kusherehekea ujumbe huo wa sikukuu kwa kawaida, baadhi ya wananchi wametumia fursa hiyo kuonesha msimamo wao kuhusu haja ya mabadiliko ya kisiasa na kisheria kabla ya uchaguzi mkuu ujao, wakisisitiza kuwa pasipo mabadiliko, hawatashiriki uchaguzi.
Jambo hili linaonesha kiwango cha ujasiri na kiu ya wananchi kushinikiza mabadiliko ya kidemokrasia nchini.
Oparesheni hii imeenda mbali zaidi kwani imepelekea hata baadhi ya viongozi na TBC kufunga sehemu ya comments.
Wananchi pia wameigia mpaka kwenye page ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson
MOja kwa moja kwenye mada Tabia ya kwanza . Kumekuwa na tabia za wasanii kutumia infuence yao kusifia chama cha kisiasa au kiongozi flani wakati wa kampen (mfano wasanii hulipwa na chama X kuwasifia kwenye majukwaa ya kisiasa na kutumia influnce yao kushawishi mashabiki zao wawapigie kura...
Hapa hatuna namna nyingine zaidi ya mabadiliko tuongozwe na viongozi watakaochaguliwa kama sisiemu akishinda ashinde kwa merits kama wapinzani wakishinda wapewe ushindi wao kadiri wananchi walivyoamua No Reform No Election ni agenda ya wananchi 2025