Ningekuuliza ni Wayahudi wa aina gani hao wasio na mashaka, na ni yapi yamhusuyo Yesu ambayo hawana mashaka nayo... hata hivyo, najua huwezi kuwa na jibu la hilo swali, hivyo niseme tu 'Unachekesha sana aisee..."
Yaani Wayahudi wangeamini Yesu alikufa na kufufuka unadhani wangeacha kumwamini?!
Mara kwa mara nimekuwa nikitumia maneno "Wayahudi kwa IMANI" na "Wayahudi kwa ASILI"... inaelekea hufahamu tofauti ya hizo dhana!!
Yesu ni Myahudi kwa ASILI... hawa ni wale waliotokana na kizazi cha Yakobo!!
Hawa Wayahudi kwa ASILI wana IMANI TOFAUTI kwa sababu, kabla ya Yesu hajaja duniani kuitangaza Injili, kuna wengine walimtangulia, and the most notable one ni Mussa ambae alikuja na Torati, bila kuisahau Zaburi ya King David.
Na kizazi hiki cha Yakobo (theoritically)kilicho Israel bado wanaamini katika Tanakh ambayo ndani yake kuna Torat, Manabii, na Maandiko... AGANO LA KALE!!
Kwahiyo Yesu alikuja duniani akiwakuta ndugu zake kwa asili (Ethnic Jews) wakiwa tayari wameshatopewa na Torati ya Mussa ambayo ni moja ya vitabu vinavyopatikana kwenye Tanakh!!
Yesu alishindwa kuwashawishi ndugu zake kuikubali Injili kwa sababu Wayahudi hawa walitabiriwa na Kumbumbu la Torat 18:18-19 kwamba:-
Wayahudi walitumia vigezo gani... I don't know lakini wakaona Yesu ha-fit kwenye utabiri huo, na kwahiyo WAKAMKATAA, na Injili aliyokuwa anaihubiri, WAKAIKATAA na wakendelea na ku-stick kwenye Torat, na bado wanamsubiria huyo Messiah hadi ninapoandika haya!
Hawa wanaoamini katika Uyahudi, HAWAAMINI CHOCHOTE wanachokiamini Wakristo kuhusu Yesu!! Hawaamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka, wala hawaamini katika Utatu Mtakatifu... HAWAAMINI CHOCHOTE!!
Ni kama ambavyo nilikuambia mwanzoni kabisa kwamba, Wayahudi (kwa imani) wanauchukulia Ukristo sawa na ambavyo Wakristo wanavyouchukulia Uislamu!
Mambo ya KIIMANI kuhusu Yesu yanaaminiwa na Wayahudi ambao ni Wakristo na sio Wayahudi wanaoamini katika Uyahudi(Judaism).
Na kwa taarifa yako, Wakristo nchini Israel ni WACHACHE sana...hawafiki hata 5%. Ni kwamba, Waislamu ni WENGI Israel kuliko Wakristo. Na zaidi ya 75% ya Wakristo wa Israel ni WAARABU kama ilivyo kwa Waislamu!! Simply meaning, Ukristo upo nje ya Israel na sio Israel wenyewe...
Unlike Uislamu ambao ulikuwa promoted na Waarabu wenyewe ambako ndo chimbuko la Uislamu, Ukristo ulikuwa promoted duniani na watu ambao kwa asili, sio "ndugu" wa Yesu!!
Na ndo maana HQ za Madhehebu YOTE makubwa ya Kikristo yapo nje ya Israel kwa sababu Wayahudi walimkana Yesu na Maandiko yake, na ndo maana Quran isiyoremba remba maneno inawataja wazi Wayahudi kwamba ni WAKAIDI, NA WATU WASIOAMINI! Quran inawasema vibaya sana Wayahudi na sio Wakristo!!