Wanaume gani watakubali kuingia na wanawake wao kwenye chumba cha kujifungulia?

Wanaume gani watakubali kuingia na wanawake wao kwenye chumba cha kujifungulia?

Nimemsikia raisi wetu SSH jana akiwa hospital ya CCBRT akisema kuna vyumba ambavyo vitatumika wakati wa mke akiwa kwenye kujifungua mume awe hapo akimtia moyo,akiona shughuli wanawake wanapitia[emoji3][emoji3] ili wapange uzazi,atoe mahitaji na vinavyofanana na hivyo.

Mimi sipingi ni jambo zuri lakini tuwe makini wajameni, haya mambo yana athari gani chanya na hasi.
Nimewahi kuwa karibu na labour siku nilimpeleka mke wa rafikiyangu hospital moja Mwanza kujifungua nikasikia kinachoendelea kule ndani, mwingine alikuwa anatukana mfululizo, anataja jina la mwanamme na kushushia na tusi, mara sikupi tena, nimekoma mimi, mara nesi nataka kunya. Jamani jamani leo ndio mwanaume uwe hapo pembeni na mke awe wale wanachukia mwanaume wake hataki hata kumuona kipindi cha ujauzito si itakuwa Ukraine ndogo?

Lakini kuna point nyingine nimewahi kuisikia kwenye dini ya ndugu zangu kuwa mume hupaswi kuutazama utupu wa mke wako[emoji3][emoji3]. Sasa tufikiri kweli mume uko hapo unaona lile tukio mwanzo mwisho kweli mh?
Nauliza kwa ambao wamewahi kuwa na wake zao kwa kipindi hicho mpaka wanajifungua,ivi baada ya hapo inatokea nini? Kumbukumbu inakuwa vizuri kabisa na hamna shida? Wanawake wa JF mnaonaje hili lilivyokaa?

Naamini ni kipindi ambacho wanaume tunapaswa sana kuombea wake kipindi choche cha ujauzito kwa kuzidi sana kipindi hiki, kuwatia moyo, kuwajali na kuonyesha upendo mara dufu na staha ya hali ya juu.

Lakini pale ndani kuwepo kwakweli usisikie sio mchezo. Mtakaokuwa mnaenda kila la kheri lakini mkumbuke kuleta mrejesho pia na wanawake mlete ushauri mapema tujue la kufanya kwa hekima.
Wanawake na wao waende makazin mbele ya wanaume zao wakiwatazama namna wanavyohangaika kutafuta chochote kitu
 
Ni vizuri wakajionee ambavyo kitendo cha kuleta binadamu duniani ni nusu uhai nusu kifo....
Nilimwambia nesi "huwezi kufanya namna yoyote kwa huyo mtoto ili mke wangu apone?" Aliniangalia, akatabasamu, akaendelea na kazi yake. Mtoto amezaliwa sikuwa na habari nae,wife kazimia.
Mwaka wa 12 huu sitaki kusikia kuhusu kuzaa mtoto.
Mke ni rafiki yangu, mtoto ni mama yangu wa pekee... Nawapenda sana.
 
Siez kwenda kule itaniathiri kisaikolojia , ntakuja kushindwa hata kumfokea huyo mwanamke akinizingua huko mbele, maana mda wote ntakuwa namuonea huruma
 
Nilimwambia nesi "huwezi kufanya namna yoyote kwa huyo mtoto ili mke wangu apone?" Aliniangalia, akatabasamu, akaendelea na kazi yake. Mtoto amezaliwa sikuwa na habari nae,wife kazimia.
Mwaka wa 12 huu sitaki kusikia kuhusu kuzaa mtoto.
Mke ni rafiki yangu, mtoto ni mama yangu wa pekee... Nawapenda sana.
ooh pole, ndio ukashindwa kumuongezea mwenzie.... Mungu ni mwema ongeza mwingine 😃
 
Mwanamke atazaa kwa uchungu na mwanaume atakula kwa jasho
Imeshapangwa hivyo na itakuwa ivyo hata nikiangalia haisaidii chochote siku akizingua ni makwenzi tu
 
Mimi ndio ilikuwa dream yangu! na nilikuwa nishaanza kuomba hilo kwa madoctor katika moja ya hospital hapa mjini! Nadhani mama sasa kani rahisishia kabisa direct ntaenda hapo mda ukifika!
 
Mmh mamaee hapana yaani nione kichwa kinatoka mkuma unapanuka midamu na mimaji mimaji ya uzazi


Ile picha itanata kwenye ubongo yaani unaweza kupoteza hisia nae

Hata kwa bunduki siingii
Sio kwamba unakaa upande ule ili uone kila kiungo chake wakati wa kujifungua, unakaa kichwani huku, unamshika mkono na kummasaji kichwani ili qjisikie amani.
 
Sio kwamba unakaa upande ule ili uone kila kiungo chake wakati wa kujifungua, unakaa kichwani huku, unamshika mkono na kummasaji kichwani ili qjisikie amani.
UjiGA du[emoji849]
 
[emoji23][emoji23]Sasa wee si ndo mhusika si mnasemaga hebu tujazie jazie miguu ya mtoto[emoji1787][emoji1787]
we acha kabisa kuna jamaa jirani alikuwa anajifanya ana mambo ya kizungu akaenda kushuhudia, alikata moto wakamlaza alika mwaka ndo akaja kumgusa mke wake. Mpaka leo amekoma.
 
kuliko kwenda leba bora uende kwenye mishe mishe zako ili ataekuja akukute umetoka kupambana ili ajue chaka aliloingia ni mapambano
 
Mh ila kwenda kushuhudia inataka moyo. Nakumbuka mwanangu wa kwanza nimepelekwa bugando, naingia tu pale nikakutana na mama anajifungua nilipagawa na uchungu ukaisha mpka wiki mbili mbele ndo nikaja kujifungua mpka leo ile picha ipo akilini na ni zaidi ya miaka tisa sasa sijui kwa mwanaume itakuaje
 
Back
Top Bottom