Wanaume gani watakubali kuingia na wanawake wao kwenye chumba cha kujifungulia?

Wanawake na wao waende makazin mbele ya wanaume zao wakiwatazama namna wanavyohangaika kutafuta chochote kitu
 
Ni vizuri wakajionee ambavyo kitendo cha kuleta binadamu duniani ni nusu uhai nusu kifo....
Nilimwambia nesi "huwezi kufanya namna yoyote kwa huyo mtoto ili mke wangu apone?" Aliniangalia, akatabasamu, akaendelea na kazi yake. Mtoto amezaliwa sikuwa na habari nae,wife kazimia.
Mwaka wa 12 huu sitaki kusikia kuhusu kuzaa mtoto.
Mke ni rafiki yangu, mtoto ni mama yangu wa pekee... Nawapenda sana.
 
Siez kwenda kule itaniathiri kisaikolojia , ntakuja kushindwa hata kumfokea huyo mwanamke akinizingua huko mbele, maana mda wote ntakuwa namuonea huruma
 
ooh pole, ndio ukashindwa kumuongezea mwenzie.... Mungu ni mwema ongeza mwingine 😃
 
Mwanamke atazaa kwa uchungu na mwanaume atakula kwa jasho
Imeshapangwa hivyo na itakuwa ivyo hata nikiangalia haisaidii chochote siku akizingua ni makwenzi tu
 
Mimi ndio ilikuwa dream yangu! na nilikuwa nishaanza kuomba hilo kwa madoctor katika moja ya hospital hapa mjini! Nadhani mama sasa kani rahisishia kabisa direct ntaenda hapo mda ukifika!
 
Mmh mamaee hapana yaani nione kichwa kinatoka mkuma unapanuka midamu na mimaji mimaji ya uzazi


Ile picha itanata kwenye ubongo yaani unaweza kupoteza hisia nae

Hata kwa bunduki siingii
Sio kwamba unakaa upande ule ili uone kila kiungo chake wakati wa kujifungua, unakaa kichwani huku, unamshika mkono na kummasaji kichwani ili qjisikie amani.
 
Sio kwamba unakaa upande ule ili uone kila kiungo chake wakati wa kujifungua, unakaa kichwani huku, unamshika mkono na kummasaji kichwani ili qjisikie amani.
UjiGA du[emoji849]
 
[emoji23][emoji23]Sasa wee si ndo mhusika si mnasemaga hebu tujazie jazie miguu ya mtoto[emoji1787][emoji1787]
we acha kabisa kuna jamaa jirani alikuwa anajifanya ana mambo ya kizungu akaenda kushuhudia, alikata moto wakamlaza alika mwaka ndo akaja kumgusa mke wake. Mpaka leo amekoma.
 
kuliko kwenda leba bora uende kwenye mishe mishe zako ili ataekuja akukute umetoka kupambana ili ajue chaka aliloingia ni mapambano
 
Mh ila kwenda kushuhudia inataka moyo. Nakumbuka mwanangu wa kwanza nimepelekwa bugando, naingia tu pale nikakutana na mama anajifungua nilipagawa na uchungu ukaisha mpka wiki mbili mbele ndo nikaja kujifungua mpka leo ile picha ipo akilini na ni zaidi ya miaka tisa sasa sijui kwa mwanaume itakuaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…