WANAWAKE KAMA HUWEZI KUMTUNZA MTOTO PELEKENI KWA BABA ZAO. MSISUMBUE WATU KWA UPUUZI WENU!
Anaandika, Robert Heriel
Unang'ang'ania kuishi na mtoto alafu huna uwezo wa kumtunza huo si upuuzi.
Kama huwezi kumtunza Mtoto na unapenda kuishi naye basi kuwa na adabu, kuwa humble Kwa Baba WA mtoto, hakuna mwanaume ambaye ni mkorofi Kwa mwanamke mwenye adabu au mnyenyekevu. Sijawahi kuona mwanaume wa hivyo. Sisi wanaume tunaupendo mara elfu zaidi kuliko ninyi wanawake, tunajali na kuthamini lakini kama heshima yetu itazingatiwa. Lakini Sisi ni makatili, washenzi, wakora Kwa watu wasiotuheshimu.
Linapokuja suala la heshima kwetu tupo tayari kupoteza vyote ikiwezekana uhai. Tupo Radhi kufukuza Mke, watoto na wote ambao hawatuheshimu. Ndivyo tulivyo. Hiyo ni kanuni yetu ya Asili Aliyotupa Muumba.
Eleweni kuwa Mtoto akiishi na Mama Mkorofi asiye na adabu tunamchukulia Kama mwanampotevu, yaani yupo nje ya Mfumo hata Kama ni mtoto wetu.
Eleweni kuwa kadiri mnavyokuwa Wakorofi na wajeuri ndivyo tunavyozidi kuwapuuza ninyi na watoto wenu.
Kumbuka, Mama Mpumbavu ni mzigo mwa Mwanaye Kama ilivyo mwana Mpumbavu alivyomzigo Kwa Mamaye.
Wanaume tunafalsafa zinazotuongoza, mojawapo ni hii, Mwanamke asipotuheshimu na akitudharau tunaamini kuwa hata mitoto yake aliyoizaa Asilimia kubwa haitatuheshimu na itatudharau.
Hatuoni shida kutelekeza Mama jeuri na mitoto yake hata Kama watoto hawana kosa. Lakini kitendo cha kulelewa na Mama jeuri na korofi tunaamini hilo toto litafuata tabia za Mama yake.
Vijana, msiogope kufanya maamuzi magumu Kama Mwanamke hakuheshimu, anakudharau na ni korofi. Ninaongea nikiwa ninauhakika na kile nikisemacho. Ninaushahidi wa kutosha dhidi ya wanaume wanaoteswa na watoto wao kisa kulelewa na mimama ya hovyo.
Mwanaume wewe ndiye mungu hapa Duniani. Wewe ndiye unayeamua mtoto gani umbariki na yupi usimbariki kulingana na tabia za watoto na Mama zao. Zingatia mara nyingi tabia za watoto huendekezwa na Wamama.
Kama vile Mungu anavyotubariki bila USAWA ndivyo hivyohivyo usibariki watoto Kwa USAWA ilihali hawapo Sawa.
Mitoto mijeuri ipe ujeuri wao.
Wamama wajeuri wape kulingana na ujeuri wao.
Watoto wema wape mambo Mema
Wamama wema walipe Mema.
Hiyo ndio maana ya kuitwa Mwanaume, Mtawala wa Dunia.
Wanawake eleweni kuwa Mwanaume hapendelei isipokuwa anafanya Kwa Haki. Na haki ya mwanaume inahesabiwa Kwa kuangalia usikivu na utii wa mtoto au wa mkewe.
Kadiri usivyomtii na kumsikiliza Mwanaume ndivyo unavyojiweka Mbali naye. Hiyo ndio kanuni ya BABA.
Sio ajabu Baba akatoa Urithi na baraka kwa Mke mdogo au watoto wa nje zaidi kuliko watoto wa ndani kutokana na vile wanavyomheshimu na kumsikiliza.
Au sio ajabu mwanaume akatoa zaidi Huduma nje ikiwezekana Kwa MICHEPUKO yake Kwa sababu ndani ya familia yake hakuna anayemsikiliza na kumtii. Hachukuliwi Kama Mwanaume.
Wanawake ukitaka uzipige pesa za mwanaume basi itakupasa uwe mwanamke halisi, umheshimu na kumtii huyo mwanaume. Hiyo ndio Siri. Hii itamfanya mwanaume awe na deni kwako.
Kumzalia mwanaume hakumfanyi awe na deni kwako. Hata CHIZI anaweza kuzaa naye. Wanaume tunajiona wenye wajibu wa kutunza wanawake na watoto wote wanaotuheshimu na kututii hata Kama sio Wake zetu au watoto wetu WA kuwazaa.
Wanaume hatuoni wajibu na hatuna msukumo kutoka ndani kutunza majitu yasiyotuheshimu na kututii hata Kama ndoa hiyo ingefungishwa na Malaika wa mbinguni.
Hakuna mzigo mzito Kwa mwanaume Kama kulitunza limwanamke lisilo na heshima au litoto lisilo Mheshimu Baba yake. Taikon anaonelea ni Bora mwanaume huyo akafungwe jela kuliko kuhudumia watoto wasiomheshimu.
Wanawake eleweni kuwa, hakuna suala la Haki Sawa baina ya mtoto wa karibu na mtoto wa Mbali. Mtoto wa Mbali atapata Haki za Mbali. Mtoto wa karibu atapata Haki za karibu.
Ni Kama vile hakuna haki Sawa Baina ya Diaspora na mtu aliyepo nchini. Kuna mambo aliyeponchini atapata Favour huku aliyembali hatazipata.
Ukitaka Mtoto wako apate HAKi Sawa Kwa Baba yake basi mpeleke Kwa Baba yake akae na watoto wenzake.
Vijana msiwe laini kiasi cha kukubali kuvunjiwa heshima yenu Kama wanaume Kwa kisingizio chochote kile.
Chagua shule Lipa Ada, mtoto asome. Mwanamke asikuendeshe na akili za kijinga. Kama anataka shule nzuri na hauna uwezo nayo mwambie wazi hutolipia hata Mia moja.
Tafuta muda uwe unaongea na mwanao kumsaili na kupiga Stori za hapa na pale. Kama mama yake anazuia Jambo Hilo kisa hujafuata mfumo wake, piga wote chini. Usiogope. Zingatia watoto wanaakili, hasa watoto wa siku hizi. Hivyo wanauwezo wa kuchambua mbivu na mbichi.
Kamwe usiseme maneno mabaya yanayomhusu Mama Kwa mtoto. Eleza mazuri tuu ya mama Kwa mtoto wako, hayo mabaya ayaone yeye mwenyewe Kwa macho yake.
Wapo wanawake wanajibebesha mimba Kwa waume za Watu makusudically ili wapate unafuu wa Maisha.
Wanawake mlio kwenye ndoa mkiona mwanamke wa hivyo anakuingilia ndoani mwako wala asikupe presha, piga Spanner za kutosha iwe fundisho Kwa wengine.
Dhibiti uchumi wa Mwanaume/mumeo mpaka akose za kutuma nje. Alafu mwambie awalete watoto hao wa nje ulee wewe. Kama hataki mwambie hutaruhusu pesa yoyote itoke nje ya Familia.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam