Wanawake, kama huwezi mtunza mtoto pelekeni kwa Baba zao. Msisumbue watu kwa upuuzi wenu

Wanawake, kama huwezi mtunza mtoto pelekeni kwa Baba zao. Msisumbue watu kwa upuuzi wenu

We nae hujui nyamaza bwana u showing the height of ur ignorance here, nature ni mwanaume kutafta ale kwa jasho, mke azae kwa uchungu ni vile sahivi most of u mmekua wavivu ndo mana upo hapa kulialia njaa ungekua unaenenda na nature usingeandika vitu virahisi hivi pia kubali kukosolewa na kufundishika, huna haja ya kumwambia mtu hata mnyama anamshinda thats a point of weakness unalazimisha kushindana na kushindwa, baki kwenye hoja ya msingi acha maneno ya hovyo

😂😂😂
Sasa maneno ya hovyo ni vile mtu anavyoyaona. Mfano maneno uliyoyatoa kunihusu Mimi sio kwamba yanaonyesha Mimi nikoje isipokuwa vile unavyoniona. Yaani ishu ya akili yako inavyofanya kazi.
Ukiniita mjinga haimaanishi Mimi ni mjinga Ila vile unavyoniona Kwa akili yako.

Huyo nilikuwa namjibu kulingana na nature.
Nawe umeeeleza vizuri kuwa jukumu la kutunza Familia na kutafuta ni lamwanaume na ndio maana mwanaume ndiye mmiliki wa familia na watoto. Ndicho nilichoeleza.
Yeye kasema Watoto ni wawote Mimi nikamuambia watoto wanakuwa ni wawote kama Wote mnatafuta na kulisha familia Kwa kiwango kinachofanana au kukaribiana.

Lakini kama mmoja ndiye jukumu lake ndio la kutafuta na kulisha familia Basi watoto wanakuwa WA huyo mwenye Hilo jukumu, hiyo ndio nature ilivyo.

Kwa wanyama Sio kila mnyama dume ndiye mtafutaji na kulisha familia, wanyama majike wengi ndio wenye jukumu Hilo hivyo wao ndio wamiliki halali wa watoto hao.
Jaribu hata kufuga kuku au Mbuzi au NG'OMBE au nenda katalii mbugani utaelewa mwenye watoto Kwa wanyama waliowengi ni Jike au dume.

Umiliki unatokana na Huduma na wajibu wa kutunza, na si vinginevyo.
 
WANAWAKE KAMA HUWEZI KUMTUNZA MTOTO PELEKENI KWA BABA ZAO. MSISUMBUE WATU KWA UPUUZI WENU!

Anaandika, Robert Heriel

Unang'ang'ania kuishi na mtoto alafu huna uwezo wa kumtunza huo si upuuzi.

Kama huwezi kumtunza Mtoto na unapenda kuishi naye basi kuwa na adabu, kuwa humble Kwa Baba WA mtoto, hakuna mwanaume ambaye ni mkorofi Kwa mwanamke mwenye adabu au mnyenyekevu. Sijawahi kuona mwanaume wa hivyo. Sisi wanaume tunaupendo mara elfu zaidi kuliko ninyi wanawake, tunajali na kuthamini lakini kama heshima yetu itazingatiwa. Lakini Sisi ni makatili, washenzi, wakora Kwa watu wasiotuheshimu.

Linapokuja suala la heshima kwetu tupo tayari kupoteza vyote ikiwezekana uhai. Tupo Radhi kufukuza Mke, watoto na wote ambao hawatuheshimu. Ndivyo tulivyo. Hiyo ni kanuni yetu ya Asili Aliyotupa Muumba.

Eleweni kuwa Mtoto akiishi na Mama Mkorofi asiye na adabu tunamchukulia Kama mwanampotevu, yaani yupo nje ya Mfumo hata Kama ni mtoto wetu.

Eleweni kuwa kadiri mnavyokuwa Wakorofi na wajeuri ndivyo tunavyozidi kuwapuuza ninyi na watoto wenu.
Kumbuka, Mama Mpumbavu ni mzigo mwa Mwanaye Kama ilivyo mwana Mpumbavu alivyomzigo Kwa Mamaye.

Wanaume tunafalsafa zinazotuongoza, mojawapo ni hii, Mwanamke asipotuheshimu na akitudharau tunaamini kuwa hata mitoto yake aliyoizaa Asilimia kubwa haitatuheshimu na itatudharau.

Hatuoni shida kutelekeza Mama jeuri na mitoto yake hata Kama watoto hawana kosa. Lakini kitendo cha kulelewa na Mama jeuri na korofi tunaamini hilo toto litafuata tabia za Mama yake.

Vijana, msiogope kufanya maamuzi magumu Kama Mwanamke hakuheshimu, anakudharau na ni korofi. Ninaongea nikiwa ninauhakika na kile nikisemacho. Ninaushahidi wa kutosha dhidi ya wanaume wanaoteswa na watoto wao kisa kulelewa na mimama ya hovyo.

Mwanaume wewe ndiye mungu hapa Duniani. Wewe ndiye unayeamua mtoto gani umbariki na yupi usimbariki kulingana na tabia za watoto na Mama zao. Zingatia mara nyingi tabia za watoto huendekezwa na Wamama.

Kama vile Mungu anavyotubariki bila USAWA ndivyo hivyohivyo usibariki watoto Kwa USAWA ilihali hawapo Sawa.

Mitoto mijeuri ipe ujeuri wao.
Wamama wajeuri wape kulingana na ujeuri wao.
Watoto wema wape mambo Mema
Wamama wema walipe Mema.
Hiyo ndio maana ya kuitwa Mwanaume, Mtawala wa Dunia.

Wanawake eleweni kuwa Mwanaume hapendelei isipokuwa anafanya Kwa Haki. Na haki ya mwanaume inahesabiwa Kwa kuangalia usikivu na utii wa mtoto au wa mkewe.

Kadiri usivyomtii na kumsikiliza Mwanaume ndivyo unavyojiweka Mbali naye. Hiyo ndio kanuni ya BABA.

Sio ajabu Baba akatoa Urithi na baraka kwa Mke mdogo au watoto wa nje zaidi kuliko watoto wa ndani kutokana na vile wanavyomheshimu na kumsikiliza.

Au sio ajabu mwanaume akatoa zaidi Huduma nje ikiwezekana Kwa MICHEPUKO yake Kwa sababu ndani ya familia yake hakuna anayemsikiliza na kumtii. Hachukuliwi Kama Mwanaume.

Wanawake ukitaka uzipige pesa za mwanaume basi itakupasa uwe mwanamke halisi, umheshimu na kumtii huyo mwanaume. Hiyo ndio Siri. Hii itamfanya mwanaume awe na deni kwako.

Kumzalia mwanaume hakumfanyi awe na deni kwako. Hata CHIZI anaweza kuzaa naye. Wanaume tunajiona wenye wajibu wa kutunza wanawake na watoto wote wanaotuheshimu na kututii hata Kama sio Wake zetu au watoto wetu WA kuwazaa.

Wanaume hatuoni wajibu na hatuna msukumo kutoka ndani kutunza majitu yasiyotuheshimu na kututii hata Kama ndoa hiyo ingefungishwa na Malaika wa mbinguni.

Hakuna mzigo mzito Kwa mwanaume Kama kulitunza limwanamke lisilo na heshima au litoto lisilo Mheshimu Baba yake. Taikon anaonelea ni Bora mwanaume huyo akafungwe jela kuliko kuhudumia watoto wasiomheshimu.

Wanawake eleweni kuwa, hakuna suala la Haki Sawa baina ya mtoto wa karibu na mtoto wa Mbali. Mtoto wa Mbali atapata Haki za Mbali. Mtoto wa karibu atapata Haki za karibu.

Ni Kama vile hakuna haki Sawa Baina ya Diaspora na mtu aliyepo nchini. Kuna mambo aliyeponchini atapata Favour huku aliyembali hatazipata.

Ukitaka Mtoto wako apate HAKi Sawa Kwa Baba yake basi mpeleke Kwa Baba yake akae na watoto wenzake.

Vijana msiwe laini kiasi cha kukubali kuvunjiwa heshima yenu Kama wanaume Kwa kisingizio chochote kile.

Chagua shule Lipa Ada, mtoto asome. Mwanamke asikuendeshe na akili za kijinga. Kama anataka shule nzuri na hauna uwezo nayo mwambie wazi hutolipia hata Mia moja.

Tafuta muda uwe unaongea na mwanao kumsaili na kupiga Stori za hapa na pale. Kama mama yake anazuia Jambo Hilo kisa hujafuata mfumo wake, piga wote chini. Usiogope. Zingatia watoto wanaakili, hasa watoto wa siku hizi. Hivyo wanauwezo wa kuchambua mbivu na mbichi.

Kamwe usiseme maneno mabaya yanayomhusu Mama Kwa mtoto. Eleza mazuri tuu ya mama Kwa mtoto wako, hayo mabaya ayaone yeye mwenyewe Kwa macho yake.

Wapo wanawake wanajibebesha mimba Kwa waume za Watu makusudically ili wapate unafuu wa Maisha.
Wanawake mlio kwenye ndoa mkiona mwanamke wa hivyo anakuingilia ndoani mwako wala asikupe presha, piga Spanner za kutosha iwe fundisho Kwa wengine.

Dhibiti uchumi wa Mwanaume/mumeo mpaka akose za kutuma nje. Alafu mwambie awalete watoto hao wa nje ulee wewe. Kama hataki mwambie hutaruhusu pesa yoyote itoke nje ya Familia.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kuna uzi umefunguliwa wa.kudai ada halafu wewe unafungua uzi huu + - =

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
We nae hujui nyamaza bwana u showing the height of ur ignorance here, nature ni mwanaume kutafta ale kwa jasho, mke azae kwa uchungu ni vile sahivi most of u mmekua wavivu ndo mana upo hapa kulialia njaa ungekua unaenenda na nature usingeandika vitu virahisi hivi pia kubali kukosolewa na kufundishika, huna haja ya kumwambia mtu hata mnyama anamshinda thats a point of weakness unalazimisha kushindana na kushindwa, baki kwenye hoja ya msingi acha maneno ya hovyo
Mkuu huwezi pingana na nature hata siku moja ipo hivyo na itakuwa hivyo mwanamke ana majukumu yake ya kiasili ambayo hata afanye nini hawezi kuyakwepa ndivyo hivyo kwa mwanaume pia.Kwa bahati mbaya naweza sema wanawake wengi wanafanya machaguo ya kuwa na wavulana sio wanaume hizo sifa ulizo sema ni sifa za mvulana sio mwanaume.mwaume hawezi kuwa mvivu wa kutafuta kwa ajili ya mwanamke wake na familia yake.

To the woman he said,
“I will greatly multiply your pain in childbirth.
In pain you will bear children.
Your desire will be for your husband,
and he will rule over you.”

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mimi ni mtu wa saikolojia ilikua ni lazima nione mwonekano wako kujiridhisha fikra zangu juu yako pasipo kukuonea mkuu

Mimi ni mwalimu wa Saikolojia. Hivyo naelewa ilikuwa lazima Kwa mwanafunzi WA saikolojia anavyofikiria.

Kama ungekuwa Mwabasaikolojia wala isingekulazima kuhangaika kiwango hicho.

Kajifunze Semantic na pragmatic itakusaidia kupata maana katika Yale uyasomayo, na uyaonayo na kuyasikia
 
Mimi ni mwalimu wa Saikolojia. Hivyo naelewa ilikuwa lazima Kwa mwanafunzi WA saikolojia anavyofikiria.

Kama ungekuwa Mwabasaikolojia wala isingekulazima kuhangaika kiwango hicho.

Kajifunze Semantic na pragmatic itakusaidia kupata maana katika Yale uyasomayo, na uyaonayo na kuyasikia
Sawa mkuu ni kweli wewe mwalimu wa saikolojia kwa mwonekano tu yani...refer to pragmatic...
 
Hahahaha naona Ile siredi ya mjumbe kutaka kumpeleka mzazi mwenzie mahakamani kisa ada imekuchefua
 
Nakiri kuwa kumekuwa na changamoto za malezi baada ya wazazi kutengana lakini utatuzi kila upande unastahili lawama......na hatuwezi kulitatua hili kwa kuangalia au kuegemea upande mmoja bali tunatakiwa kubalance kila upande ili tupate muafaka.......

Wapo wanawake wanaotumia watoto kama kitega uchumi Cha kuendesha maisha......pia wapo wanaume wanaotumia gharama za matunzo kama fimbo ya kumchapia mzazi mwenzie baada ya kutengana.........

Kwa vyovyote vile kama juhudi za kuwafanyia waishi pamoja wanandoa au wazazi zimeshindikana basi kwa manufaa ya watoto wazazi na walezi wakae wajadiliane namna nzuri ya kuwahudumia watoto wao na kuhakikisha wanapata mahitaji yao ya kimsingi kama watoto wngine......

Si uungwana wala ubinadamu kuwaunganisha watoto kwenye ugomvi wa wazazi au walezi.......

Masuala haya yanatakiwa busara na hekima kuyatatua sio jazba.....
Umemaliza Mkuu.
 
Shukrani sana mkuu,neno lako limenipa faraja,Mimi mwenyewe tumezinguana na wife na amerudi kwao,kisa namuambia mara kwa mara kuwa sufuria ya kupikia chakula inabidi ioshwe pia chini uvunguni,

Lakini yeye ataki kusikiliza, anakuwa mbishi, eti masufuria hayaoshwagi chini hasa Kwa sisi tunaotumia Kuni kupikia

Anaacha masufuria yanakuwa na masizi mpaka basi..,ukimuambia anaona unampelekesha

Ukishika tu sufuria mikono inajaa masizi.., nikaona huu ni upuuzi Sasa

Mwanaume aheshimiwe,hata kama kakuambia kitu ukaona akiwezekani wewe fanya Ili tuone kama kweli haliwezekani kuliko kuleta dharau
Ungemuonyesha mfano wa kusugua.
 
Mleta mada wewe jinsia gani ? Kutwa kuleta habari za wanawake wakati jina lako ni la mtoto wa kiume

Ndugu wa mleta mada hebu kaeni naye

Muongee naye kuna shida au ana Genes za kike au shoga labda?
Google him mkuu utapata majibu yote uliouliza ...
 
Mimi nimelelewa na mama na wadogo zangu, ila kila likizo tulikuwa tunaenda kwa baba,mama yangu ni mtata mno ukichanganya alikuwa askar ndioo balaa

Yaan hiyo likizo ilikuwa na ratiba yake siku tatu kwa baba siku zilizobak kwa bibi mzaa baba...km mzee anataka tukae kwake likizo mwezi mzima ilikuwa sharti bibi mzaa baba aje tukae nae kwa baba au ndugu upande wa baba hasa ma aunt( hapa dogo alikuwa anamiaka 3,mwingine 6 mimi 9) hilo sharti lilikuwa kipaumbele cha bmkubwa ikitokea akijua tulikaa wenyew kw dingi na maza mdogo bila ndugu kuwepo bac inaweza pita miaka hata miwili bila kwenda kwa mzee( watoa taarifa ni madogo na ma aunt coz alikuwa ana bond nao kubwa mpaka sasa. kwamba tulikaa wenyew)

Bimkubwa wangu alikuwa mtata sana ila sijawahi sikia wanagombana masuala ya matunzo wala ada,mzee alimwachia nyumba bmkubwa alafu sijawahi sikia wakipondeana.. japo bmkubwa alikuwa anajifanya nunda anakomaa kutulipia ada mwenyew na huku tukitoka likizo tunafedha za mzee...yaan mashindano yao kiukweli sisi watoto tulifaidika mno(tulikuwa tunanunuliwa makolokolo mengi)

Mzee alikuwa anatuma hela kwenye acc ya bimkubwa,uzuri bmkubwa alikuwa anasema baba yenu kawatumia hela zenu( kwetu shangwe) zikiwa nyingi alikuwa anatununulia mashamba( sasa hivi ni viwanja kisasa mbuyuni-Dodoma na ilazo dodoma kila mtu now anavyo viwili viliwi)

Ila kuanzia kidato cha tatu bmkubwa ndio aliacha kutufuatilia tukiwa kwa Mzee akawa ananiambia waongoze wadogo zako huko kwa mama yenu mdogo ushajua baya na zur hata mkiwa wenyew bila bibi yenu..

Japo mzee amefariki sasa ishapita miaka mitatu ila kutengana na bmkubwa toka 1997 ila walikuwa wanaheshimiana sn,faza mtu wa stor na vituko sana..walikuwa wanapiga stor na kushauriana mambo mengi yaan mpaka tumekuwa watu wazima hatujawahi ona wakifokeana zaid ya kupewa taarifa tu nimeongea na baba yenu leo au nliongea na mama yenu..

Bimkubwa yeye baada ya kuachana aliishi mwenyew mpaka sasa..mzee alioa na kubahatika kupata watoto wawili kwa maza mdogo..

Maza mdogo tunaishi nae vizur tu,tunashirikiana mambo mengi,hata ivyo mzee alimwachia msingi mzur...ila na yeye pia ni mpganaji km bimkubwa ...(urithi haujasumbua maana mzee aligawaga urithi akiwa hai yaan kila familia ilijua vitu vyake mpaka ukoo wa mzee ulishirikishwa )
 
Femissts mpo? Singles! Naona mapovu machache kuliko nikivyotarajia.
Anaye pingana na ukweli anajisumbua Tu.
 
Mimi nashikilia hapo kwenye ujeuri wanawake wengi aisee ni wajeuri sanaa ninawaona wengine ninawashuhudia yani kwanza anavyoongea na baba mtoto ni full matusi hapo anataka kuomba ada anasema ngoja nimpigie huyo mbwa hajui ni muda wa ada? Mtoto akimuudhi atamtukana matusi yote anamwambia ww ni mbwa kama baba yako, mbona kuna wengine wanaishi vzr na malezi yanaenda ila siungi mkono kwenye matusi hasa kumtukana mzazi mwenzio tena unamtukana na mtoto matusi makali as if alikuwepo wakati unaenda geto kwa huyo baba ake. Mkiachana achaneni kwa amani mtunze watoto wenu kwa heshima na baba hakikisha kama ulihaidi kulipq ada lipa kwa wakati kuna kukosa sometyms shirikishaneni muone mta solve vipi. Ila wamama kwa midomo hatujambo.
 
Mimi nashikilia hapo kwenye ujeuri wanawake wengi aisee ni wajeuri sanaa ninawaona wengine ninawashuhudia yani kwanza anavyoongea na baba mtoto ni full matusi hapo anataka kuomba ada anasema ngoja nimpigie huyo mbwa hajui ni muda wa ada? Mtoto akimuudhi atamtukana matusi yote anamwambia ww ni mbwa kama baba yako, mbona kuna wengine wanaishi vzr na malezi yanaenda ila siungi mkono kwenye matusi hasa kumtukana mzazi mwenzio tena unamtukana na mtoto matusi makali as if alikuwepo wakati unaenda geto kwa huyo baba ake. Mkiachana achaneni kwa amani mtunze watoto wenu kwa heshima na baba hakikisha kama ulihaidi kulipq ada lipa kwa wakati kuna kukosa sometyms shirikishaneni muone mta solve vipi. Ila wamama kwa midomo hatujambo.

Alafu wengu wanapenda kuvuruga familia za watu.

Anajipachika mimba makusudi na mume WA mtu Kwa lengo la Kula pesa za Mwanaume.
Akitumiwa za mtoto tuu anasema ndogo Kwa maana anapiga na mahitaji yake Kama Kodi na bills zingine.

Au mtu mmeachana anataka bado umhudumie Kama zamani, yaani kuna mambo yanachekesha sana
 
Back
Top Bottom