Wanawake kwa hizi akili, Mna haki ya kupigwa matukio

Matukioa gani mkuu , mtu ana degree nne unataka uje umfuge kama mtumwa au mfanyakazi nyumbani kwako? Kwanini usitafute aliyeishia la 7 halafu hawa wasomi wenye akili ukatuachia sisi?
Naunga mkono hoja wengi hawakumuelewa walifikiri ameshauri wanawake wasiwe wanawafulia wanaume zao boxer wakati kauli yake hiko hivi Wanawake wasiishie pekee kufua boxer wafanye zaidi ya hapo unajua kiswahili ni kigumu kwa waliowengi neno "pekee" lipo kwenye sentensi yake alafu wakachanyikiwa na alivyosema ana degree nne wao wakaona kama ni kiburi, anajisikia bila kumsikiliza context ya yeye kusema hivyo ni Nini? Katumia kusema hivyo kumaanisha Wazazi wake wamesomesha mpaka kuwa na hizo degree si tu awe mama wa nyumbani Bali awe ni msaada wa familia yake na atayoitengeneza kiuchumi huwa wabongo wanaokotesha maneno machache bila kuelewa ujumbe mzima mhusika aliolenga kwa kisimi tunaita Extensive Reading
 
Wanaume wengi wanapenda kunyanyasa na kumuendesha mwanamke!!! Utaona anamfanyia vituko vya kila aina na majigambo juu kuwa "ataenda wapi???"
 
Nilimuelewa vizuri tu, ila jiulize:

1. Unajua kwanini wanaume wengi tunapendelea mabinti zetu wasome, wawe na fedha na wasimtegemee mwanaume ila tunataka wake zetu watutegemee?

2. Unajua kwanini mwanaume ni rahisi kumtamani mwanamke wa mwanaume mwingine ila akiachika interest kwa huyo mwanamke inapotea?

3. Unajua kwanini mwanaume atatoa hata wanawake 20 bikira halafu atataka aoe bikira kisha baada ya kuoa anaendelea kutafuna bikira zingine hata za mabinti nusu ya umri wake?

4. Unajua kwanini single mothers kwa kijana wake ni HERO ila kwa kijana wa mwingine hafai kuwa mke?

Majibu ya haya maswali ndo yanatufanya tumshambulie huyo dada.
 

Mkuu wewe na huyo mwanamke kwenye hiyo video na huyu mwamba unayemuunga mkono wote mna tatizo hilohilo la uelewa mdogo mnalotuhumu wengine kuwa nalo. Matatizo ya umma (public issues)yanazungumzwa kwa wingi na kwa ujumla. Sasa hebu niambie ni wanawake wasomi asilimia ngapi wanazuiwa na waume zao na wanashindwa kabisaa kujitafutia riziki? Narudia tena ni wachache sana sana. Ktk ulimwengu wa sasa hakuna mwanaume anaweza mzuia mwanamke kujitafutia riziki. Isitoshe majority ya wanaume wanapenda mwanamke mwenye uwezo wa kuchangia garama za familia. Sasa ni nini msingi wa hizi tuhuma?
 
Kazusha, by implication, kwamba ndoa ni kizuizi cha maendeleo kwa mwanamke wa kitanzania. That's not true anymore. I called her an idiot because she seems to truly believe her nonsense.
Wapi huyo mama amesema ndoa ni kizuizi cha maendeleo?
 
ujumbe upo very clear ni vile wabongo hatupendi kusikiliza kwa makini mtu kasema kabisa "Wanawake wasiishie pekee kufua boxer wafanye zaidi ya hapo" hivi kweli hapa unahitaji uwe na degree ndio uelewe au neno boxer na ndio limechanganya watu? Wakafikiri eti wasifuliwe boxer au kusema yeye ana degree nne waka term kama ni anajisifu au kiburi bila kuelewa mantiki ya hoja nzima na kaeleza kwa kina yeye kasomeshwa mpaka kufika level hiyo ya kuwa na degree nne si tu awe mama wa nyumbani pekee Bali awe msaada kwa familia yake kiujumla na si kumtegemea hivi hapa unashindwa vipi kuelewa au vile stress zinatusumbua
 
Vitu gani hivyo mkuu ambavyo mtoto wako wa kike anapaswa kufundishwa.
Mahusiano ni asili labda tuanzishe ya kisasa kama vile ambavyo kila kitu ni cha kisasa. Swali tunalopaswa kujiuliza Je mahusiano yatadumu na kuwa yenye afya au ndio yatakumbwa na saratani?.
 
Kwa kweli sijaelewa hoja yako
 
Msingi wa hoja upo kwasababu wapo wawakawe wengi wakiolewa wanaambiwa na Wanaume zao waache kazi wabaki kuwa mama wa nyumbani hao ndio Pasta kawalenga
 
Wanaume wengi wanapenda kunyanyasa na kumuendesha mwanamke!!! Utaona anamfanyia vituko vya kila aina na majigambo juu kuwa "ataenda wapi???"
Hapo wewe uliyeamua kuolewa na Mwanaume wa hivyo ndio hujitambui na hujui unachokitaka kwenye maisha yako. Kila mtu awajibike kwa uchaguzi wake!
 
Kwanini upige mimba umuache? Ni vyema kumuacha bila kumgusa kabisa.

Kumbe mnaitumia mimba kama adhabu, haya tumefahamu.
Huu upuuzi siupendi watu kama hawa ndio wanaotuzalishia single mother's wanazalisha alafu jukumu la ulezi anamwachia mzazi mwenzake kama kumkomoa ajui kuwa kile kiumbe kilichozaliwa ni chake alafu Sasa huyo mtoto akija kuwa mwenye maendeleo baba anaanza kujipendekeza
 
Wapi huyo mama amesema ndoa ni kizuizi cha maendeleo?
Kwahiyo hapo anapozungumzia madhara ya mwanamke msomi kuwa mama wa nyumbani anayepika na kufua boxer anazungumzia mahusiano ya kaka na dada? Halafu alivyo mjinga hajui kwamba kuna wanawake wasomi na ni mama wa nyumbani na hakuna kitu wanapungukiwa. Halafu anatafsiri usomi kwa idadi ya degrees.
 
Hoja yako ina ujazo wa juu kabisa uzingatiwe
 
Hii vita ni kali sana lugha aliyotumia tu ni kuonesha ana kiburi cha elimu na kipato nani ataishi na mwanamke mwenye ego kiasi hicho
 
Namnukuu Wanawake wasiishie pekee kufua boxer wafanye zaidi ya hapo kama haujaelewa hapo utakuwa una shida zako binafsi
 
Kwa kweli sijaelewa hoja yako
Nahisi kamaanisha kuwa mzazi hamsomeshi mtoto wa kike kuja kuwa kiburi na ego ya kujitegemea bali hufanya hivyo kutimiza wajibu lakini likitokea suala la kuolewa credit ni zilezile za miaka yote hazijawahi kubadirika hata wewe huwezi weka dume jike ndani mwako eti ukamuita mke
 
Wanaume tumelishwa mentality ya kuwa control hawa viumbe ila tunakoelekea haiwezekani
Kwako wewe ndio haiwezekani, kiasili ndio tumeumbwa hivyo wala sio mentality. Ww unaweza kufanya kazi za mwanamke kama kufua kidek, kupika, kuosha vyombo au kuandaa watoto ilihali mkeo yupo hapo? Kama mkeo yuko juu yake hautaweza tena kumsimamia.
 
We should Know this and know peace, Wanaume asilimia baadhi hawapendi watoto, Idea yao ya kuzalisha ni kutaka kumcage mwanamke.
 
Namnukuu Wanawake wasiishie pekee kufua boxer wafanye zaidi ya hapo kama haujaelewa hapo utakuwa una shida zako binafsi
Ni mwanamke yupi kaishia kufua boxer kwa kulazimishwa na akawa hana namna kuondokana na ulazima wa kufua boxer? Yeyote anayeamini hivi ana changamoto ya kufikiri.
 
Nimeangalia chapisho lake mtandaoni kuhusu PhD yake haliko wazi maana yake ni ya magumashi ndiyo maana anaongea ujingaujina.Mwenye PhD iliyoshiba huwa ni faida kwa jamii na siyo kubomoa jamii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…