Wanawake wanawahi kuchoka, Mwanaume unatoa wapi ujasiri wa kuoa mwanamke mnayelingana umri?

Wanawake wanawahi kuchoka, Mwanaume unatoa wapi ujasiri wa kuoa mwanamke mnayelingana umri?

Wanawake vijana wote wanazaa? Kwanini uzae uzeeni na sio ujanani? Nani atalea watoto wako?
tunazaa kama viumbe hai wengine, habari za kufikiria kulea ni habari za kufikirika hasi. Niache kuza kisa eti watoto watalelewa na nani? Mi mwenyewe nitawalea nikiwa hai na nikiwa mzee sana sina nguvu mama yao kijana atawalea, na mpaka mama yao azeeke kiasi cha kushindwa kuwahudumi watoto watakuwa wameshakuwa wakubwa kujihudumia wenyewe
 
Mwanaume kama unakula vizuri na unafanya mazoezi ya hapa na pale moto unapeleka mpaka uzeeni tatizo wengi huwa wanajisahau mtu unaendekeza kitimoto na bia wakati uko abv 40
Sasa unazani wanawake nao wamechoka sana? Kuna mwingine akikwambia ana 45 utakataa kabisa wapo warembo kabisa, sema wanaume wanawafuja na kuwapa stress zakutosha
 
Bado mnajiuliza ni kwa nini babu zetu walikua wanaoa mke zaidi ya mmoja, majibu yake ndio hayo, huyo aliyefikisha 40 unampandisha cheo, then unamtafutia msaidizi mwenye 30 years, mmoja anakuwa manager mwingine CEO familia inastawi vyema kabisa
Vijana wanadanganyana tu....hawajui mzizi wa fitna zote ni kuoa wake zaidi ya mmoja.....

Yaani uoe kamwanamke kamoja na useme tunaendana nae....waaapiiiiii??
 
Mwanamke mkilingana, hata stories zenu zinafanana. Marafiki wanakuwa agemates, mnakumbushiana habari za Amina Chifupa alipokuwa Clouds FM au Akina Daz Baba wakati anasoma Azania. Sasa wewe ulizaliwa 1985 unaona dada wa 2001 utapiga naye story gani wakati wa usiku??
Usiku siyo muda wa stori, ni muda wa kula kitumbua.
 
Bado mnajiuliza ni kwa nini babu zetu walikua wanaoa mke zaidi ya mmoja, majibu yake ndio hayo, huyo aliyefikisha 40 unampandisha cheo, then unamtafutia msaidizi mwenye 30 years, mmoja anakuwa manager mwingine CEO familia inastawi vyema kabisa
Au unaoa mnaelingana huyo anakua ndio CEO wa familia anasimamia kila kitu. Halafu huko nje we unakua unajichapia tu vitoto vya 18 - 24 kadri unavyopenda no strings attached.
 
Mimi naona mwanaume anatakiwa amzid mwanamkewake hekima busara na maarifa ya kuendesha familia kunawatu wazee kweli lakin kichwani empty😀Kuna vijana wako vizuri sana mnalingana umri lakini unaona kabisa huyu kanizid kilakitu
Umri namba tu
 
Nitoe mfano, majina yakiwa ya kutunga.

Mwaka 2008 Fred akiwa na miaka 26 alifunga ndoa na Recho mwenye miaka 25. Wote walikuwa bado ni vijana wabichi kabisa wanavutia.

Kufikia Leo Fredi ana miaka 41 huku Recho ana 40, unaweza kuhisi Fred alioa dada yake.

Fred ni rafiki yangu, anakiri kwamba alikosea kufanya huo uamuzi hasa ukizingatia yeye bado kijana ambae huvutiwa bado na mabinti wenye muonekano wa ujana bila make up, ambao wengi ni chini ya miaka 32.

Muda huu ni ngumu hata kwa Recho kuzaa na kuzaa akiwa na miaka 41 na kuanza kulea watoto, ule umri mzuri wa kuzaa ushampita, hivyo inakuwa kizuizi hata kwa Fred.

Pia wote kwa pamoja wapo katika hatari ya magonjwa nyemelezi ya miaka ya 40 kama kisukari, homa ya ini, presha, n.k.
Wanaume Wenye akili na hekima huoa wanawake wanaolingana umri (balanced age) hapa mtabalance kwenye mambo mengi na kushabihiana ila wale wanaume wapumbavu huoa mabinti waliowazidi sana umri na hujikuta kwenye majuto na kujifia mapema.
 
Back
Top Bottom