Wapi mnapata pesa za kujenga wandugu? Mbona kwangu naona chenga tu?

Mi pia naona hii inaelekea kuwa chai,uandishi unaongea...
Sio chai kabisa ni maisha hasili ninayopitia,sasa niandike chai ili iwaje?je nitafute umaarufu na nikishapata huo umaarafu faida yake nitakayo ipata ni ipi??
Toka mwanzo nilisema ni maisha yangu haya sijaongeza wala kupunguza chochote
 


Inaendelea.
Habari zenu wandugu??
Jumapil imetulia vyema,japo umeme wamechukua masnitch tanesco ila hakuna kitakacho haribika.

Kama nilivyosema hapo mwanzo hii ninayoandika ni mimi niliyopitia,nashangaa kuna watu humu wamekuwa daima wanaamini kila uongo wasikiacho au kukisoma,kama unaona nilichokiandika ni chai ni wewe na roho yako kivyako..

Tuachane na hayo..
Twende moja kwa moja baada ya kuchakatua mbususa wa huyo mwanamke wa kinyakyusa,ni kama nilimloga aisee maana kipindi hicho alikuwa anaishi kwa Dada ake.

Akawa anatoroka kwa Dada ake nakuja kwangu maana kwa Dada ake na kwangu sio mbali kivile,demu akanogewa na muhogo kutoka chuga,mda wote anataka nimkune, usiku anatoroka nakuja kwangu nikamwambia aende kwao hataki,dada yake akapeleleza mpaka akajua ni mimi ninayo msababisha kutoroka kwao,basi dada akanifuata nikamuelekeza huwa anakujaga kwangu,nikamwambia asiwe na wasiwasi nipo naye,basi nikapewa uhuru wakuwa Nate.

Binti siaka hamia kwangu manzima,na begi lake la shangazi kaja kipindi anakuja manzima kwangu tayari alishapata ujauzito,basi tukaishi vyema huku nikiparangana na mbishe zangu za library na sokoni.

Kweli nililea ile mimba mpaka kufika WAKATI wa kujifungua,nikajiandaa vyema kumpokea mtoto wangu,kwa sisi wachaga mtoto wa kwanza lazima alelewe na Bibi yake au Dada zako,basi nikampeleka chuga kujifungua.

Basi kweli mwisho wa siku akajifungua mtoto wa kiume,aisee nilifurahi sana maana nilishahapaga lazima Mama yangu hamuone mjuu wake kabla hajafa,basi mzee Baba nikawa natuma pesa za kula uzazi,aisee binti alinenepa na kupendeza sana maana wa Mama wa kichaga wanajua kulea sana wajawazito.

Baada ya miezi kadhaa kuptia mwanamke akaanza vituko kwa Mama mkwe,mama yangu mimi ni mfanya biashara soko kuu la Arusha,huwa ndani anajaza kila kitu mchele,mafuta,unga ,sabuni n.k sasa mwanamke akawa anavigawa kwa majirani,lila akimuuliza mbona vitu vinaisha mapema anajibu vinatumika,hivi kweli mchele kilo 10 unaweza kuisha kwa siku 5??ukicheki nyumbani yupo yeye na Mama tu Dada zangu wameolewa.

Akawa hashindi nyumbani tena mda wote anashinda kwa majirani,afanyi chochote kama kumsaidia mama kuchota maji na usafi,akihamka siku nzima anashinda kwa majirani kazi kupiga umbeya,nikaona Bora nimtumie nauli aje Dar.

Basi toka aje Dar hakuna hata ndugu yake aliyekuja kukucheki,na kumpa hongera kwa kupata mtoto nikasema ishalaah yote DUA basi mzee Baba nikaendelea kumlea vyema bila hata ya tabu yeyote.

Nitajitahidi kuandika kwa kirefu baadaye simu inaisha Charge huku nilipo wamekata umeme toka jana jioni,samahani sana wa ndugu
 
Hmmmm inakuja inakataa enewei lete mambo hayo huwqga wanaandika kwenye notebook ya simu wasave then utakua wakop na kupaste tuh mkuu nusu nusu jau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…