Wassira: Mkapa alikopa trillion 23, Jakaya alikopa trillion 20, Magufuli alikopa trillion 29

Wassira: Mkapa alikopa trillion 23, Jakaya alikopa trillion 20, Magufuli alikopa trillion 29

kuna picha ya wasira yupo na Nyerere nadhani ni miaka ya 70 ile,yani hawa wazee wapumzike tu,sasa imagine mtu alikuwa anapiga stories na Nyerere alafu bado tutegemee maoni yake leo
wamefanya kazi kubwa sana wakati wao,sasa watuachie vijana,ndio mambo ya kina Ndugai ni mkubwa sana yule mzee
Kwamba huyu Mzee ni age mate wa Charles Njonjo aliyechomwa moto 4 days ago at 101? Hata hivyo maoni yake yaheshimiwe; pinga hoja zake badala ya character assassin.
 
Lilikopa kwa kificho likadai nchi yetu ni tajiri tutembee kifua mbele kumbe linakopa hovyo tena mikopo umiza maana ujeuri ulimfanya asiwe na mahusiano mazuri kupata mikopo nafuu!!!
Bora katoka ofisini asee loh!

Tudai katiba mpya jamani tuachege ujinga tutaumia hadi lini??
Kati ya maamuzi yake ya kushangaza ni kukataa mikopo nafuu na misaada akakimbilia mikopo ya kibiashara! Kiuchumi alikuwa bonge la sifuri; total failure.

Kwa mfano kulikuwa na fedha za millennium challenge account jamaa kwa kiburi akazikataa akakimbilia standard chartered! Akili matope?
 
Ndiyo maana tuliingia uchumi wa kati
Kama Magufuli angetawala miaka 10 angelikopa Trilioni 58!

Hakika hii nchi ingepigwa mnada mchana kweupe na tungeanza kuuza eneo alilozikwa
 
Kwahiyo huyu mzee anataka kukonklude kwambaa!???
 
Na angekuwa mpenda-mikopo, zile bilion dollars za corona 2020 mwaka juzi asingeziacha. Ndiye Rais pekee Afrika aliyependekeza nchi maskini zifutiwe madeni badala ya kukopeshwa tena na kuwaongezea mzigo mzito wananchi.
Hii hawataisema hata siku moja...
 
JPM pesa alizokopa zilitumika kama ifuatavyo
1. Kununua wapinzani waliofika bei ( Waitara, yule WA Liwale, Gekuli, Meya wa Arusha) Mnyeti zingine kununua madiwani na Nassary huko arumeru akina Silinde)

Walionunuliwa Kila mtu alikula pesa yaani dalali na anaenunuliwa

2. Kuijenga chato - huko pesa kibao ilipelekwa bila utaratibu

3. Kufadhiri kikundi Cha wasiojulikana. Kwa taarifa TU Hawa walitumia pesa nyingi sana huwezi kuziediti.

4. Sukuma gang hao walitumia pesa kutoa taarifa kokote Ili kulinda utawala wa jiwe
5 Sabaya na kundi lake Hawa mbali na kumhujumu mbowe kule hai lkn alitumika pakubwa kusimamia kundi LA wasiojulikana Kanda ya kaskazini

5. Ununuzi wa ndege bila kufuata taratibu za manunuzi

6. Ujenzi holela wa miradi

Maovu mengi alifanya yalitumia pesa nyingi hovyo.

Prof. Assad anaweza kutusaidia kufanya ouditing.
 
Kwa hiyo Magufuli alitupiga sana kwenye mikopo?
Aliwapigaje na Flyover mnaziona, barabara za Mwendokasi,Barabara 8 Kimara-Kibaha, Midege...

Hebu acheni kufuru kwa aliyoyafanya Magufuli yangefanywa na utawala wa Jakaya nahisi deni ambalo wangekopa lingefikia trillion 50 au zaidi na bado miradi ingekuwa haikukamilika! Kwa ufisadi wa hali ya juu tulioshuhudia katika awamu ya 4 trillion was wasted alot tofauti na ambavyo ilitakiwa itumike.
 
Aliwapigaje na Flyover mnaziona, barabara za Mwendokasi,Barabara 8 Kimara-Kibaha, Midege...

Hebu acheni kufuru kwa aliyoyafanya Magufuli yangefanywa na utawala wa Jakaya nahisi deni ambalo wangekopa lingefikia trillion 50 au zaidi! Kwa ufisadi wa hali ya juu tulioshuhudia katika awamu ya 4 trillion was wasted alot tofauti na ambavyo ilitakiwa itumike.
JPM alijua:

1. Kubana matumizi
2. Kuelekeza pesa kwenye miradi muhimu na mikubwa yenye tija kwa wananchi wote kwa muda mrefu
3. Kuzuia ufisadi wa pesa na mali za umma
4. Kuepuka mikopo isiyo ya lazima (lika corona etc)
5. Kuwatapisha pesa wapiga-dili na mafisadi
 
Kwani issue ni kukopa au matumizi ya mikopo imewanufaisha nini watanzania? Katika hao maraisi JP ndio raisi ambaye mikopo aliyochukua imeleta faida kubwa kea wananchi kwa kuwakikisha inaenda kwenye miradi iliyopangwa kwa wakati sambamba na kudhibiti ufisadi na Rushwa.
Faida zipi hizo?
Unakopa unaenda kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa Chato, hizi ndiyo faida??
 
Kwamba jiwe alikuwa anakopa ili tuingie kwenye uchumi wa kati... hatari sana ila ndio ivyo tena hakuna namna tupambane tukope mpaka 100tril, then tuanze kulipa au tupige nchi mnada.
Juzi gavana as BOT anasema kigezo cha kukopa ni Rasilimali watu.... kwamba tukufika 100mil mkopo inabidi iongezwe tena
 
Mzee Wasira yupo Star TV Hivi sasa katika kipindi cha the Big Agenda anasema kwa miaka 10 kila mmoja cha Mkapa na Jakaya walikopa trillion 23 na 20 mtawalia.

Magufuli kwa miaka 5 alikopa trillion 29.
 
Attachments

  • IMG_1419.MP4
    532.2 KB
Mzee Wasira yupo Star TV Hivi sasa katika kipindi cha the Big Agenda anasema kwa miaka 10 kila mmoja cha Mkapa na Jakaya walikopa trillion 23 na 20 mtawalia.

Magufuli kwa miaka 5 alikopa trillion 29.
Ukijumlisha mikopo ya watatu hao ni sh. trilioni 72; swali rahisi, mikopo ya Mkapa na Kikwete haina riba? Maana katika hizo trilioni 29 za JPM kuna riba za watangulizi wake, hivyo uhalisia deni alilokopa JPM ni chini ya hizo zinazotajwa.
 
Kila mwaka tunalipa trillion 10 kupunguza deni lakini tangu Magufuli alipoingia madarakani deni limekuwa likipaa!
 
Kwanza kabla sijaendelea ni #Wasira upi? The Chimps?
Kama ni huyo ngoja nikakate gogo
 
Kwamba jiwe alikuwa anakopa ili tuingie kwenye uchumi wa kati... hatari sana ila ndio ivyo tena hakuna namna tupambane tukope mpaka 100tril, then tuanze kulipa au tupige nchi mnada.
Juzi gavana as BOT anasema kigezo cha kukopa ni Rasilimali watu.... kwamba tukufika 100mil mkopo inabidi iongezwe tena
Tutakufaaa!
 
Ukiona mradi gani ulio simama?

Mambo yalikuwa yanaenda mchakamchaka hujawahi ona?
Mfano mradi wa DRT, mbagala ulisimama kabisa, na mwaka huu ulikuwa ukabidhiwe, yule DC wa tmk, Gondwe alikuwa kila mala anakwenda anapigwa mkwara wapi eti mbona kazi haiendi, wao wanasema pesa hakuna, waki issue certificate, hakuna pesa, nenda sasa hivi ukaone kazi inavyokimbia, hiyo sgr kawaulize ma sub contractor walikuwa na hali gani, hadi ma bank yaliwakataa!!kulikuwa na kampuni la kireno pale, kaulizie lilienda wapi?hiyo barabara ya morogoro,
USA, mwenyewe anazingatia bajeti , wewe KIDUDU MTU, hutaki kufuata utaratibu kwa kuendesha nchi, unaendesha kwa mizuka tu, lazima u fail tu, Cha ajabu jana Ndugai ndio ana kili kuwa serikali ilikuwa inaendeshwa ki ugumu sana, kwani pesa iliyotengwa huku inapelekwa kule, mwaka wa fedha unaisha wizara imepata 16% ya bajeti yake iliyotengwa, halafu unakuja kumlaumu waziri!!kutokana na kila leo kuja na mambo ambayo hayako kwenye bajeti.
 
Kwani issue ni kukopa au matumizi ya mikopo imewanufaisha nini watanzania? Katika hao maraisi JP ndio raisi ambaye mikopo aliyochukua imeleta faida kubwa kea wananchi kwa kuwakikisha inaenda kwenye miradi iliyopangwa kwa wakati sambamba na kudhibiti ufisadi na Rushwa.
Na kuthibitisha hilo, kwa kipindi cha miezi 10 tangu afe serikali imekopa tr 10 na hela hazieleweki zimeenda wapi.
 
Kwa hiyo Magufuli alitupiga sana kwenye mikopo?
Samia kakopa Trillion 10, wanachoangalia ni upandaji mpaka unatoka! Linaangaliwa deni sio kiasi ulichochukua hivo basi katika deni kuna riba na riba inapanda inategemea ulikopaje! Kwaiyo kupanda kwa deni ndani yake kuna riba humo
 
Back
Top Bottom