Wasukuma punguzeni huu ulaji wa chakula kingi namna hii


Rekaga kuyomba ma mihayo ga basaji. Bebe utanyaga? Jaga ukanye ukuje nhumbi urye,
 
Aisee hadi mimi nilishangaa kuona binti mdogo tu ameshusha mzigo mithiri ya gogo asee😂😂
 
Mtoa thread hapo kuna mambo mawili unatakiwa utambue
1. Anaishi kijijini au mjini
2. Hali ya kiuchumi ikoje

Tuchambue sasa kwa kifupi
1. A. Kijijini maranying watu wanakula milo miwili yaani mchana na jioni alafu wanafanya kazi ngumu kwahyo mwili unahitaji chakula kingi ili kukizi mahitaji ya mwili
B. Mjini maranyingi hawafanyi kazi ngumu na milo ambayo wanakula ni zaidi ya tatu tena ambayo haina mipangilio ndio maana wanaota vitambi 😄😆. Kwahyo ukipiga hesabu unakuta wa mjini anakula chakula kingi kuliko yule msukuma wa simiyu
2. Hali ya kiuchumi kwa watu wengi waishio mjini ni mbaya sana hata kama anakula milo yote mitatu lakini ni kwa shida sana.
Unakuta familia ya watu watano asubuhi wanakula mihogo ya mia tano na chai nusu kikombe
Mchana wanakula nusu kilo ya unga
Usiku wanakula nusu kilo ya mchele kwa idadi ileile ya watu na siku imeishia hapo. Huyo mtu akienda usukumani walimaji anakuta ndonga ya watu watano wanaokula huko mjini inapigwa na watu wawili lazima ashangae na kuona kitu cha ajabu sana

Ngoja nikale kwanza nitakuja kuendelea.......
 
kabisa mkuu, usukuman wanawake wenye vitambi kama uchagan hakuna na watu wanakula chakula cha asili wana nguvu nyingi na ni imara hata akizeeka, nimewahi kukaa na wasukuma nakuunga mkono uliyosema ni ya kweli.
 
Maisha ni zaidi ya kula, wabongo tujaribu kuwa na imaginations pana zaidi ya kuzaa na kushiba tu.
 
Ni jamii ya wafugaji wote ni walaji wazuri. Juzi nilienda umasaini kwa jamaa mmoja kununua ng'ombe.

Ilibidi niende asubuhi kabla ng'ombe hazijaenda machungani. Nimemkuta mke wa jamaa amesonga ugali wa dona mkubwa sana. Cha ajabu yule mama alauacha ugali uungue jikoni kwa muda mrefu hadi ukabadilika rangi. Then akawaletea jamaa waule
Ule ugali ni mwingi sana na jamaa walikula wakiwa nyama huku na maziwa mgando lita 1 kila mmoja.
 
Maisha ni zaidi ya kula, wabongo tujaribu kuwa na imaginations pana zaidi ya kuzaa na kushiba tu.
Soma Biblia, Ibrahim Baba wa Imani alikuwa na Watoto wangapi?

Mfalme Suleiman alikuwa na Watoto wangapi

Mtume Mohamed SWS, alikuwa na Watoto wangapi

Maisha yafaa nini kama hatuli na kuzalisha ili Koo zetu ziendelee
 
Soma Biblia, Ibrahim Baba wa Imani alikuwa na Watoto wangapi?

Mfalme Suleiman alikuwa na Watoto wangapi

Mtume Mohamed SWS, alikuwa na Watoto wangapi

Maisha yafaa nini kama hatuli na kuzalisha ili Koo zetu ziendelee
Hatuishi tena zama za Biblia au karne ya 7 enzi za Muhammad.
 
hiyo ilikuwa ni misingi tuliyoachiwa na Mitume wetu, ni lazima tuifate
Sio lazima muifuate, mnaamua wenyewe kuifuata au kutoifuata kwa kuangalia uhalisia, pia itafika wakati nyakati na hali halisi zitawafanya mshindwe kabisa kuifuata.
 
Watu awajui kuwa injini ya tractor ni tofauti na injini ya IST
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…