HOJA Wataalamu wa kipengele cha uhamisho ndani ya ESS naombeni msaada mnivushe hapa

HOJA Wataalamu wa kipengele cha uhamisho ndani ya ESS naombeni msaada mnivushe hapa

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Wewe kwakuwa Bado hujatimiza miaka mitatu kazini, piga kazi huko Halmashauri uliko huu Uzi utakutia wenge tuachie wenye mapambano yetu😂​

Jamaa anaweza kutoka huko mapema kabla yako na barua yake ikaanza na “ Kutokana na umuhimu wa kazi na kwa mamlaka niliyonayo chini ya Kifungu cha…”

Utabaki unashangaa hapo. Be humble mshua, mtumba ni kwa watumishi wote.​
 
We

Kwahiyo wewe unaona sijawa humble, inawezekana wewe ni mgeni wa huu Uzi, sisi humu hatujawahi kuwa na makasiriko tushazoea maisha yetu hasa kwenye huu Uzi, kutaniana, kupongezana, kupeana pole pale mtu anavyopata rejected na masikhara ni kawaida kwani inatupunguzia stress zinazotokana na hizi issue za Transfer na Castr tupo wote hapa toka yeye ameanza kufuatilia Uzi na ali-declare kuwa bado hajatimiza miaka 3.
Fuatilia huu Uzi utaelewa na kujua ni akina nani ni waasisi wa huu uzi.
 
....
 
Baada ya hapo inakaa siku ngapi ili ifike utumishi?

Kufika utumishi hata siku ya pili inawezekana kutokana na jitihada zako kwa mabosi wako, kwanzia supervisor, mkuu wa idara na Mkurugenzi kama wanakupitishia chap inaenda Utumishi kiongozi ila kama hufatilii inakaa siku hata 20 kwa level ya chini
 
Kuwa bembeleza
 
Hahaha!
Mkuu, kuweka medical reasons labda uwe unataka kuhama kutoka machaka kwenda town kwenye Taasisi hiyo hiyo ndo uhamisho utakuwa na afya.

Imagine unatoka LGA unataka kwenda taasisi ya umate umate halafu unawawekea ripoti yako ya ugonjwa “wa leo ama kesho 😁” Wao wanahitaji nguvu kazi mkuu. Utumishi kwa kukusaidia watakutoa huko machaka wakusogeze eneo lenye huduma nzuri kwa matibabu kulingana na afya yako. (Chini ya LGA hiyo hiyo😁).

Pursue new challenges ndiyo mpango mzima.
Hahaha sure aisee umesema kweli. Basi huenda ndio maana hata vacancy naiona hapa leo imepita auto 😂.
 
Wakuu ee this time ombi langu limepita auto, hivi hakuna ushuhuda hata mmoja wa aliepata uhamisho kwa auto kabla sijawithdraw?
Maana wale jamaa ukiomba transfer kwa auto umewarahisishia kukureject.
 
Wakuu ee this time ombi langu limepita auto, hivi hakuna ushuhuda hata mmoja wa aliepata uhamisho kwa auto kabla sijawithdraw?
Maana wale jamaa ukiomba transfer kwa auto umewarahisishia kukureject.
Auto maana yake ata kama auna sifa umepita,mm naomba this time Mungu asaidie lisipite auto
 
Ndio maana yake, coz sio HR wala DG/CEO wameangalia CV yako na kuona sifa zako. Ndio maana Huwa ukituma Vacancy, CV lazima uwekeili Mwajiri mpya akaone sifa zako na kujiridhisha kuwa unafiti kwenye Taasisi hiyo na cheo hivyo.

Kwa kweli AUTO sio kitu Cha kukiaacha ni issue ya ku-withdraw mapema kuliko kupoteza muda
Auto n mbaya sana,maana kw hali ya kawaida lazima waangalie cv Yako na waweke maoni kama wanakuhitaji au hapana,Mimi namshauri afanye jambo moja tu ku with draw na kuanza upya au kutafuta sehemu nyingine
 
Mfumo hufanya kazi hivyo kwa baadhi ya kada. Kwa mfano, Taasisi A inapokuwa na uhitaji wa Tutorial Assistant (TA) au Mwalimu wa Fizikia mwenye kiwango cha elimu ya Shahada, mfumo unaweza kumruhusu mtu yeyote kuomba nafasi hiyo bila kujali kama ana Diploma ya Arts, Shahada ya Arts au hata GPA iliyo chini ya 3.5 kwa nafasi ya TA.

Hivyo, kukubaliwa kwa maombi na mfumo hakumaanishi moja kwa moja kwamba mwombaji anakidhi vigezo vya nafasi husika. Ni jukumu la Taasisi Lengwa (Destination Institution) kupitia maombi, kuchambua sifa za waombaji na kuthibitisha kama wanaendana na mahitaji ya nafasi waliyoitangaza. Kwa maana hiyo, uamuzi wa mwisho unapaswa kuzingatia sifa na vigezo vya mwombaji, siyo tu kukubaliwa kwa maombi na mfumo.
 
Back
Top Bottom