HOJA Wataalamu wa kipengele cha uhamisho ndani ya ESS naombeni msaada mnivushe hapa

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Wakuu ivi KM utumishi akikuandikia kibali ,ni lazma kipitishwe kwa RAS Kisha kiende wa mwajiri wako(mkurugenzi) ndo ukipate au kinatoka Moja kwa Moja bila kupitia kwa RAS ??

Kibali cha KM kimekua addressed kwako kupitia kwa (KK) mwajiri wako. Sasa RAS anahusikaje hapo? Labda kama ni kibali kutoka kwa KM TAMISEMI, hapo sina uzoefu ila na penyewe sidhani kama lazima kipite kwa RAS.​
 
Kweli aise
 
Na iwe hivyo mkuu.
 
Anaweza kuwa sahihi tu, kwa maana yeye hataki hayo makaratasi. Kwa mantiki hiyo unatakiwa uanze uhamisho kupitia dirisha la Vacancy ndio mbadala wa hiyo barua.
Sijui umeelewa hapo..?
Nimekuelewa boss,asante
 
Chief kwema?!
Hongera kwa hatua, kikubwa tu kama IKAMA ipo aawa kwa mwaka husika tegemea kuula
Kikubwa ni taasisi wakikibali utumishi ni kuangalia tu ikama
Hongera
 
Hii Week inaenda kuisha.. Utumishi wanaongoza Bado 5 - 0 Wasubiri vibali Tena wamechoka😁

UTUMISHI 5 - 0 WASUBIRI VIBALI
halafu ni mechi isiyokuwa na muda/dakika maalum na mechi inaendelea
 
Kupitisha haimaanishi umekubaliwa, alichoandika Mkurugenzi wako huwezi kukiona. Kiufupi hawezi kukuruhusu kuhama ili hali unaruhusa ya masomo. Endelea tu na shule, huwezi kypata uhamisbo.
 
Kupitisha haimaanishi umekubaliwa, alichoandika Mkurugenzi wako huwezi kukiona. Kiufupi hawezi kukuruhusu kuhama ili hali unaruhusa ya masomo. Endelea tu na shule, huwezi kypata uhamisbo.
Mkuu mbona unakatisha tamaa Wapambanaji..!!
 
Kuna mmoja kazini kwetu alituma maombi na yakafika Utumishi June, kalamba asali juzi (26/08/2026).

Tuendelee na Dua na sala.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Mkuu hv kibali wanatuma kwa ess au kwenye taasisi husika
Kwenye ESS unakutana tu na status.
Kama ni "Granted" basi unasubiri kibali, na HR wako akikipokea na Mkurugenzi akisaini basi yeye HR ana ki-attach kwenye ESS na huko unakoenda wanakipokea kwa mfumo.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…