HOJA Wataalamu wa kipengele cha uhamisho ndani ya ESS naombeni msaada mnivushe hapa

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Hili swala la kuhama na kama mwakani nina panda daraja Kuna uwezekano wa kutopanda daraja kwasababu ya kukosa asilimia za pepmis ni la kweli ?
 
Hapa shida basi ni mfumo ,watu wapo busy bora wangeondoa auto features tu
Kuna jamaa angu limemtokea hili…

Aliomba nafasi mwezi wa tano mwaka huu akapata(kwenye taasisi)

Mwezi wa sita maombi yakafika utumishi..mwezi wa nane akawa rejected comment ni “Bajeti ya nafasi imeshapita”

So pia hii ni changamoto kwa wengine..ni lazima pia tuangalie timing ya kutuma maombi
 
Aisee ni Kuomba Mungu tu
 
Samahani naomba kama kuna aliyeona nafasi ya kuhamia kwa kada ya ict officer II anishitue kwenye huu mkeka ipo moja singida lakini kwenye ess haipo kabisa.
 
Samahani naomba kuuliza hivi unaweza kuomba nafasi kwenye taasisi mbili Kwa wakati mmoja ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…