Kwa ufupi mfumo wa ESS unahitaji maboresho mengi sana madogo madogo ambayo yasipoangaliwa kwa jicho huru na makini yatawasababishia watumishi magonjwa ya sonona na mengineyo kama hayo.
Mfano hai: kuna mdau alikuwa anafanya kazi taasisi X kwa miaka zaidi ya 12 alipambana sana kuhama wakati ule wa kuhama kwa taratibu za barua za hardcopy, ila unajua tena zamani maofisini mambo yalivyokuwa magumu kuruhusu uhamisho.
Kwa bahati nzuri au mbaya likatoka tangazo Wizara imeiunganisha ile taasisi X kwenda taasisi nyingine kubwa Y, Hivyo wafanyakazi wote wakawa wanasoma taasisi Y na kwenye mfumo barua ikawekwa wamehamishwa. Tatizo linakuja kilichobadilika kwao ni jina ila mazingira ya kazi wapo kituo kile kile na kila wakijaribu kuomba kuhama hata kama taasisi Y imeruhusu wao kuondoka katika Mfumo ESS unawakataa ukiandika hawajamaliza miaka mi3 katika taasisi waliyopo sasa.
Hii inamaanisha wamepoteza haki zao za kuhama japo wameweza kutumikia pale kwa miaka zaidi ya 12 na wapo mazingira yale yale kilichobadirika ni namba ya mwajiri tuu.