HOJA Wataalamu wa kipengele cha uhamisho ndani ya ESS naombeni msaada mnivushe hapa

HOJA Wataalamu wa kipengele cha uhamisho ndani ya ESS naombeni msaada mnivushe hapa

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Vacancy ilipita auto na hiyo ndo shida kama una anza michakato hakikisha kule unapo kwenda wapitishee
Hapa kwene Auto sema watu pia tunachanganya ombi likifika destination Organisation haliendi kwa Accounting officer moja kwa moja lina anzia kwa Mkuu wa idara ya utumishi katika taasisi husika yeye ndo anatoa maoni then analituma kwa mkuu wa taasisi (Accounting officer) Sasa huyu Afisa utumishi asipo ligusa ombi lako halitoki kwa njia ya auto hata likae mwaka. Ili ombi liende auto lazima kwa HR alipitishe kwakwe nayeye hana uwezo wa ku re-reject ko sasa Ishu ya auto nazani kule utumishi kama ombi lilipita auto watakua wanazingatia pia na Comments za HR kipindi analituma ombi kwenda kwa Acounting officer.
 
HR wa destination anao uwezo wa kureject
 
Uhamisho ni changa moto sana asa kwa tusio na connection
Wanakaza maana wanajua huko Halmashauri ndio kuna watumishi wengi na wanahudumia Watanzania wengi, mkitaka kuhamia wengi kwenye Taasisi huko hakutakuwa na watu.

Lakini Fuatilia hotuba yake Naibu Waziri wa Utumishi, kazidi kupiga spana kuwa hawapokei uhamisho wa makaratasi pia kasema AUTO VACANCY ipo na inaendelea 😁
Japo inaendelea kula vichwa vya watu
 
Auto vacancy nahisi lengo lake ni kupunguza foleni so inakwenda Kisha unapigwa za uso ukajipange
 
Ila hata comments sio kigezo Cha kupata nafasi unaweza wekewa comments nzuri sana na Ikawa Rejected so wakati wa Mungu ni sahihi Mimi now namwachia Mungu
 
NAIBU WAZIRI QWARAY ASISITIZA MATUMIZI YA MFUMO WA E-UHAMISHO
Na Veronica Mwafisi-Lindi na Mtama
Tarehe 23 Oktoba, 2026

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray amesema Serikali imeendelea kuimarisha mifumo ya kidijitali ili kuongeza uwazi, uwajibikaji, ufanisi na ubora wa huduma hiyo hivyo, Watumishi wa Umma wahakikishe katika maombi yao wanatumia Mfumo wa e-Uhamisho badala ya kuendelea kutegemea taratibu zinazoweza kusababisha urasimu na ucheleweshaji.

Naibu Waziri Qwaray amesema hayo leo katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Umma wa maeneo hayo wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kusikiliza changamoto zinazowakabili Watumishi hao na kujadili namna bora ya kuimarisha utendaji.

Mhe. Qwaray amesema kuwa, maombi ya nakala ngumu yanayotumwa kwa Katibu Mkuu (UTUMISHI) hayatapokelewa badala yake njia sahihi ni kutumia mfumo huo wa e-Uhamisho.

Ameongeza kuwa, waajiri na wasimamizi wapitie maombi na kutoa maoni kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa ili kufanyia kazi kwa wakati kwani, maombi ya uhamisho kwa njia ya mfumo yana muda wa kukaa katika ofisi na yasipopitishwa ndani ya muda husika maombi hayo yataenda katika hatua inayofuata.

”Nitoe wito kwa waajiri na wasimamizi kupitia maombi na kutoa maoni kwa wakati kwani uhamisho kwa njia ya mfumo yana muda wake, kwa mkuu wa Taasisi ni siku 10, kwa msimamizi ni siku 4 na kwa mkuu wa Idara ni siku 3 yasipopitishwa kwa muda husika maombi haya yataenda katika hatua nyingine”, amesema Mhe. Qwaray

Akihitimisha hotuba yake Mhe, Qwaray amewataka Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kufanya kazi kwa bidii, kusimamia maadili na kuzingatia maslahi ya umma kwa lengo la kujenga imani ya Wananchi katika taasisi husika kwa ustawi wa Taifa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Mhe. Qwaray amesema Wilaya ya Lindi inamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha nyingi ambazo zimesaidia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali jambo ambalo linawapa ari Watumishi wa Umma ya kufanya kazi kwa moyo, upendo na kujituma.

Naye, Katibu Tawala Msaidizi, Utawala na Rasilimaliwatu-Lindi, Bw. Natalis Linuma amemshukuru Naibu Waziri, Mhe. Regina Qwaray kwa kufanya ziara katika Mkoa huo na kuahidi watatekeleza na kufanyia kazi maelekezo yote ambayo yametolewa kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi.
 
Back
Top Bottom