kipenseli2021
JF-Expert Member
- Jul 17, 2021
- 2,181
- 1,988
Wapo Fair KakaHow?
#YNWA
#YANGA_BINGWA
Wapo Fair KakaHow?
#YNWA
#YANGA_BINGWA
NAIBU WAZIRI QWARAY ASISITIZA MATUMIZI YA MFUMO WA E-UHAMISHO
Na Veronica Mwafisi-Lindi na Mtama
Tarehe 23 Oktoba, 2026
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray amesema Serikali imeendelea kuimarisha mifumo ya kidijitali ili kuongeza uwazi, uwajibikaji, ufanisi na ubora wa huduma hiyo hivyo, Watumishi wa Umma wahakikishe katika maombi yao wanatumia Mfumo wa e-Uhamisho badala ya kuendelea kutegemea taratibu zinazoweza kusababisha urasimu na ucheleweshaji.
Naibu Waziri Qwaray amesema hayo leo katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Umma wa maeneo hayo wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kusikiliza changamoto zinazowakabili Watumishi hao na kujadili namna bora ya kuimarisha utendaji.
Mhe. Qwaray amesema kuwa, maombi ya nakala ngumu yanayotumwa kwa Katibu Mkuu (UTUMISHI) hayatapokelewa badala yake njia sahihi ni kutumia mfumo huo wa e-Uhamisho.
Ameongeza kuwa, waajiri na wasimamizi wapitie maombi na kutoa maoni kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa ili kufanyia kazi kwa wakati kwani, maombi ya uhamisho kwa njia ya mfumo yana muda wa kukaa katika ofisi na yasipopitishwa ndani ya muda husika maombi hayo yataenda katika hatua inayofuata.
”Nitoe wito kwa waajiri na wasimamizi kupitia maombi na kutoa maoni kwa wakati kwani uhamisho kwa njia ya mfumo yana muda wake, kwa mkuu wa Taasisi ni siku 10, kwa msimamizi ni siku 4 na kwa mkuu wa Idara ni siku 3 yasipopitishwa kwa muda husika maombi haya yataenda katika hatua nyingine”, amesema Mhe. Qwaray
Akihitimisha hotuba yake Mhe, Qwaray amewataka Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kufanya kazi kwa bidii, kusimamia maadili na kuzingatia maslahi ya umma kwa lengo la kujenga imani ya Wananchi katika taasisi husika kwa ustawi wa Taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Mhe. Qwaray amesema Wilaya ya Lindi inamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha nyingi ambazo zimesaidia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali jambo ambalo linawapa ari Watumishi wa Umma ya kufanya kazi kwa moyo, upendo na kujituma.
Naye, Katibu Tawala Msaidizi, Utawala na Rasilimaliwatu-Lindi, Bw. Natalis Linuma amemshukuru Naibu Waziri, Mhe. Regina Qwaray kwa kufanya ziara katika Mkoa huo na kuahidi watatekeleza na kufanyia kazi maelekezo yote ambayo yametolewa kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi.
Wanakaza maana wanajua huko Halmashauri ndio kuna watumishi wengi na wanahudumia Watanzania wengi, mkitaka kuhamia wengi kwenye Taasisi huko hakutakuwa na watu.
Lakini Fuatilia hotuba yake Naibu Waziri wa Utumishi, kazidi kupiga spana kuwa hawapokei uhamisho wa makaratasi pia kasema AUTO VACANCY ipo na inaendelea 😁
Japo inaendelea kula vichwa vya watu
I kamaAuto sio tiketi ya kukosa na comments za mkuu wa taasisi sio tiketi ya kupata!! IKAMA ya unakotoka na maoni ya mwajiri wako ndo kusema!!
KabisaWale mnaosubiri vibali naona tarehe za vibali zimewadia, Sikilizie kuanzia kesho 26 - 30 Oct
Hii ni weekend ya maajabu, E-Transfer inafunga Jumamosi na Jumapili🤔Ila mfumo una funguka
Ukiona ivyo hakuna vibaliHii ni weekend ya maajabu, E-Transfer inafunga Jumamosi na Jumapili🤔
HawasomekiUkiona ivyo hakuna viba
Hakuna nafasi zilizo tangazwaHabari za wakati huu, ndugu zangu.
Naomba ufafanuzi kuhusu mfumo wa Utumishi. Je, nafasi zilizotangazwa zikishajaa, mfumo huzuia waombaji wengine kwa kuonyesha ujumbe wa “Vacancy Filled”, au kuna utaratibu mwingine unaotumika kudhibiti maombi?
Nitashukuru kupata ufafanuzi kutoka kwa mwenye uelewa kuhusu jambo hili. Asanteni.
Nakubaliana na wewe. Na mimi baada ya miezi 8 ya kusubiri nimekula Rejected. Hakuna uthibitisho wa nafasi wazi. Japo nilipambana sana. Nafasi nilipewa. Kule nilipotaka kuhamia wanashangaa.Endeleeni na illusion huo mfumo umekuja kuzuia uhamisho ila mnajitoa ufahamu,wake up mnapotezewa muda.
Poleni.
Duh Sasa miezi nane yoteNakubaliana na wewe. Na mimi baada ya miezi 8 ya kusubiri nimekula Rejected. Hakuna uthibitisho wa nafasi wazi. Japo nilipambana sana. Nafasi nilipewa. Kule nilipotaka kuhamia wanashangaa.
Pia Bora ss wengine tuchague taasisi za kawaidaNakubaliana na wewe. Na mimi baada ya miezi 8 ya kusubiri nimekula Rejected. Hakuna uthibitisho wa nafasi wazi. Japo nilipambana sana. Nafasi nilipewa. Kule nilipotaka kuhamia wanashangaa.
Mimi taasisi ya kawaida tu nilitaka career Development na kuhama mkoa. Pay 1.5M. No posho posho.Pia Bora ss wengine tuchague taasisi za kawaida
Aisee so umekuwa rejectedMimi taasisi ya kawaida tu nilitaka career Development na kuhama mkoa. Pay 1.5M. No posho posho.
Rejected.Aisee so umekuwa rejected
Pole but don't give up, ili kuwa auto auRejected.
Normal transfer.. Nilipata barua ya nafasi wazi nikaweza kwenye mfumo na vielelezo vyote.. Ila ndiyo hivyo.Naachana nayo. Kama kupambana nilipambana sana.Pole but don't give up, ili kuwa auto au