Watanzania tujiulize Maswali muhimu ya Kibiashara kuhusu bandari zetu kwa dunia ya leo

Ww utakua umeolewa huko uarabuni, maana unawahusudu sana hao masultan
Tuwe na lugha za kuheshimiana kwenye huu mjafaa mkitaka lugha za kuoana kuna jukwaa la mahusiano, hata mimi nimetangaza huko, jionee:

 

Kasome kwanza MoU ndiyo uje kuandika hapa. Hakuna watu ambao hawaipendi DP World. Yaliyomo kwenye hiyo MoU ndiyo baadhi ya watu wanaona yana ukakasi.
 
Sasa hata hayo unayotaka tuyazungumzie hayana nafasi kwasasa maana hatuyajui mkataba unasemaje.
Upo sahihi kabisa, tusubiri mikataba. Maana ni mikataba mingi sana ijayo, bandari inahusisha mabao mengi sana.

Hapa ndiyo kama hivyo tunaelemishana, labda kwanza ulifikiri mkataba upo, sasa itakuwa umeelewa kuwa kinachosubiriwa ni mikataba.

Kwa kuwa hii ni biashara kubwa na inawagusa wengi ambao wanafaidika na hali, kwa hiyo lazima fitina zinakuwa kubwa.

Wengi wanapinga lakini ukiwauliza unachokipinga nini, kimya. Au wanajibu "ukakasi", sasa kama kuna ukakasi si waweke chumvi. Swali moja tu lipo post namba moja na nimelirudia humu mara chungu nzima, hakuna anaelijibu. Mpaka najiuliza, kwanini?
 
Mi ninavyojua huyo mwarabu katangulizwa na mmarekani ila cc akili ndogo tunafikiri tumewin
 
Pantosha

Mbona unaniwekea maneno yako kwenye post zangu? Tafadhali zifanyie editing.
 
Mi ninavyojua huyo mwarabu katangulizwa na mmarekani ila cc akili ndogo tunafikiri tumewin
Upo huru na fikra zako. Hakuna kisichowezekana.

Kikwete aliwahi kusema "kula uliwe".
 
Kumbe hoja yako si bandari bali kina Samia. Umeeleweka.


Kazi ya Mungu haina makosa.
 
Bandari za tanganyika hatuwezi kukubali ziuzwe au zikodishwe na wazanzibar!
Kama ni hivyo basi ni vizuri sana kwani hata makubaliano yalikuwa ni baina ya Serikali ya Tanzania na Falme ya Dubai. Siyo Tanganyika.

Hivi Tanganyika iko wapi? Mimi sijaiona tokea mwaka 1964. Si Nyerere alimkatalia Mzee Jumbe alivyotaka kuwe na Tanganyika mpka akamtowa kwenye Urais wa Zanzibar?

Sisi tunafahamu chadema kizingiti chao ni kura za Zanzibar, ndiyo maana hawaitaki kabisa Zanzibar. Kama wewe ni chadema nakushauri muwahini Ali Karume, mtakuwa mmeshamaliza kazi. Lakini hapa kwenye bandari hata Mmarekani mwenye hisa zake Dubai hatokubali. Na hivi alivyofurahi kampuni ya Kichina kuondolewa pale banarini, ndiyo kabisa.

Na G55 kama unawakumbuka, si walizimishwa madai yao ya Tanganyika na Nyerere au ulikuwa bado siku hizo?

Kuirudisha Tanganyika ni mpaka wakubali walioruhusu ifutwe kwenye uso wa dunia. Mmarekani na Muingereza.
 
Lione swali lililoulizwa, unalo jibu au una swali lako tulijadili? Au mawazo yako tuyajadili. Hao wanaoona "haya" achana nao.
Hebu tupe kidogo ukomo wa makubaliano yaliyofikiwa. Ni kile kipengele kinachosema mpaka shughuli za bandari zikome? Halafu una justify vipi kukodisha bandari zote nchini? Hii wewe unaona sawa? Mikataba yeyote midogo itakayokuja lazima iwe ina comply na.makubaliano mama.
Jambo jengine, unadhani mkataba kama huu kwa maslahi na mustakbali wa nchi, ukizingatia uwekezaji uliofanywa, kwamba ujadiliwe tu bungeni na kuridhiwa ndani ya siku moja? Kulikuwa na uharaka gani? Unatafakari vitu kama hivi?
Eti kwamba tuuridhie kwanza halafu ndo tutumie nguvu kubwa kutoa ufafanuzi kwa hoja mbalimbali za.wananchi? Kwa maslahi ya nani?
 
Waulize wao serikali wameshindwa nn kuiboresha hii bandari kama Mombasa wameweza?.
Hata Mombasa kwa sasa wanaendesha kusogeza siku, wanajenga kwa mkataba bandari mpya kubwa zaidi huko Lamu.

Dunia ya biashara ya bandari imebadilika sana. Ina ushindani mkubwa sana. Kama hauna mitaji mikubwa hufiki popote, utabaki kuambulia vimizigo uchwara tu. Tanzania leo unaweza kuagiza mali kutoka Ulaya basi ukaipata baada ya miezzi minne. Wakati inatakiwa ndani ya 14 ikichelewa sana mwezi mmoja tu uwe umeshapata mzigo wako. Unafahamu sababu zake?
 
Kwanza hakuna mtu hata mmoja mpaka sasa niliyemsikia akipinga uwekezaji wa DPW kwenye bandari zetu, kinachopingwa ni baadhi ya vipengele vinavyompa muwekezaji mamlaka makubwa kuliko wenye mali huku faida hazijawekwa wazi.
 
Huwezi ukajadili jambo na mtu aliyetanguliza chuki,hii issue wengi wanaendeshwa na chuki tu na ubaguzi,

Subiri uone wakakavyokuja na matusi badala ya kujikita kwenye hoja.

Naona wameshaanza maneno maneno, ndio maana wanaDP WORLD wamewafungia kukomenti kwenye page yao, si unawajua watanzania mkuu, wengi wao nimefuatilia komenti zao wanatukana wanadhani ile page ni ya udaku.


Asanteni sana dp world kuwablock
 
Acha UONGO!! Dubai Expo 2020 imefanyika 2021 kwa sababu ya Corona.
 
Kwanza Faiza huwezi endesha mjadala huu maana msimamo wako unajulikana unaunga mkono kutwaliwa milele kwa bandari kwa kivuli cha uwekezaji. Pili wale wanaoupinga tayari wametishiwa maisha yao, na tayari moja ameponea chupuchupu kwenye jaribio la utekeji. Hivyo kuweka hoja hapa za kupinga utwaliwaji milele wa Bandari kwa malipo yasiyojulikana ni kujihatarishia uhai. Tatu waziri wa mambo ya ndani ameonya wale wanaotumia lugha za matusi kwenye mjadala huu. Ukweli watu wazima wanajua ni kawaida CCM wakizidiwa hoja utaona waziri wa mambo ya ndani anaibuka na kuonya dhidi ya matusi, UKWELI HAKUNA MATUSI YOYOTE ni kutengeneza njia ya kuwakamata na kuwababimbikia kesi wakosoaji. Mwisho hoja za kina kitenge, Steve Nyerere, Manara, Zembwele za kuunga hoja za utwaliaji milele kwa malipo yasiyojulikana tumezisikia, DHIDI ya Hoja za Proffesa Shivji, Lissu, Mbowe, Tibaijuka, Mawakili, Maaskofu nk.
Sentesi ya mwisho ni ya muhimu zaidi unless ni mwathirika wa CCM mentality ya kuunga mkono kila kitu bila ya kutumia neema ya akili uliyojaliwa na Mola wako.
 
Waziri mkuu alisema, TICTS haikuwa na ufanisi unaoridhisha, Kwa maana hiyo DPW wamekuja kuwa mbadala wa TICTS, na TICTS mkataba wao ulikuwa na ukomo, Je DPW world ukomo wake ni miaka mingapi? wakiunderperform kama TICTS itakuaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…