Ndugu zangu watanzania,
sauti za mamilioni ya Watanzania ni kiu Yao ya kuhitaji utumishi wa Rais Samia mpaka 2030, watanzania wengi wameguswa na uchapakazi wa Rais Samia, wametekwa mioyo Yao na kazi za Rais Samia ambazo zimeleta Tabasamu na Taswira mpya ya kimaendeleo katika Taifa letu.
watanzania kwa wingi wao hawaoni sababu ya kupoteza mamilioni ya Fedha kwa ajili ya kuchapisha karatasi za nafasi ya Urais wakati utendaji kazi wa Rais Samia umejibu maswali ya Watanzania na kukata kiu Yao ya muda mrefu ya kuhitaji Rais mchapa kazi, mzalendo, msikivu, Jasiri, imara, madhubuti, shupavu, mwenye maono Sera na ajenda za kugusa maisha Yao.
Watanzania wanajiuliza wamtoe na kumnyima Rais Samia kura ili wampe Nani? Aje afanye nini kipya ambacho hajafanya Rais Samia? Aje na ajenda na Sera zipi ambazo Rais Samia hajazigusa katika maisha Yao?
Wanajiuliza kipi ambacho Rais Samia hajatekeleza ama kukigusa katika yote waliyoyahitaji watanzania?
Wanajiuliza kwanini wasimpe muhula wa pili Rais Samia ili aendeleze kazi njema aliyoianza ya kuijenga nchi yetu? Kwanini wamnyime Kura zao wakati muda wote amekuwa akizungumza ajenda zao?
watanzania wanamuona Rais Samia Kama mkombozi wao katika kuwakwamua kiuchumi,wanamuona Rais Samia Kama kiongozi mwenye uthubutu mkubwa Sana na ujasiri wa Hali ya juu katika kusimamia maslahi ya Taifa letu,wanaona namna Rais Samia alivyojitoa na kujitolea kulitumikia Taifa letu kwa moyo wa uzalendo, wanaona juhudi za Rais Samia katika kujenga uchumi jumuishi unaomgusa kila mtanzania pasipo kumwacha yeyote nyumaa,wanaona namna alivyotuvusha katika nyakati ngumu mpaka hapa alipotufikisha ambapo kila mtanzania Anayo matumaini makubwa Moyoni mwake ya kutimiza Ndoto zake.
Ndio sababu ya Watanzania kumhitaji Rais Samia Kuendelea kuwaongoza, Watanzania wanahitaji Rais Samia abakie ikulu Kama Rais wao na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama,wanahitaji kuona Rais Samia akiendelea kuwatumikia na hawaoni sababu ya kuona Rais Samia akizunguka mikoani kuomba kura wakati kazi zake kupitia miradi mbalimbali inaonekana kwa kila mtanzania, Hivyo wanaona muda wa kampeni abakie ikulu akichapa kazi na kuwahudumia watanzania kwa kuwapelekea maendeleo yanayogusa maisha yao.
Kazi Iendeleee , mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi ga ihumicevuruwake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania na sauti
KumbaLucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627