Watoto wa siku hizi wanadekezwa sana

Umeambiwa beba sahani yako beba.
Kama ni mgeni wa kuja na kuondoka utaambiwa, wacha usihangaike, kama ni ngeni wa kufikia hapo ndiyo uuelewe utaratibu wa hapo.
kama huwezi unaacha unaondoka, wacha ujuwaji wa kutaka kuwapangia watu maisha yao.
When in Rome, do as the romans do.

Kwa hili uko sahihi
 
Kuna Nyumba zingine zina majiko ya wazi, yaani sinck la Vyombo linaoneka kutoka dining room!!
Acheni umbea kwenye nyumba za watu wewe mgeni sehemu zako ni 2 tu living room na dining room na kwa kuongezea public toilet

Vingine mwenye nyumba atake yeye kukuonyesha
 
Tatizo sio single mama, tatizo ni mwanaume aliyekataa mimba, ushoga unasababishwa na wanaume, either direct or indirect.

Msiwasingizie wanawakeee.
Na hakuna Mwanaume anae kataa Mimba bila sababu! Single Mama mjirekebishe ili wababa wa Watoto wenu wasiwakimbie!!
 
Acheni umbea kwenye nyumba za watu wewe mgeni sehemu zako ni 2 tu living room na dining room na kwa kuongezea public toilet

Vingine mwenye nyumba atake yeye kukuonyesha
Mkuu ugeni una madaraja,kuna wageni wengine mwisho wao ni siting room tu,na kuna wageni wengine hadi vyumbani wanafika!!
 
Mkuu ugeni una madaraja,kuna wageni wengine mwisho wao ni siting room tu,na kuna wageni wengine hadi vyumbani wanafika!!
Na kuna wageni wengine wao mwisho wao ni huko nje,hata siting room hawaingiii!!
 
Nenda kasome tafsiri ya neno "Udini" kwenye kamusi ya Kiswahili na utaeelewa namaanisha nini!!
Nasoma between the lines, na nnawafahamu sana kwa neno udini mnamaanisha nini.

Udini wangu mimi, wewe unakuwasha nini?
 
Kitendo cha kuhamia Dodoma kimetenganisha wazazi na kuchangia kushuka kwa maadili. Baba tuko Dom, mama anarudi usiku, housegirl ndo meneja wa familia. Watoto kama ni wa kiume utasikia mama na house girl wanapikezana "nitakuchapa", "nitamwambia babaako"
 
Dogo mmoja niko kwao nadiscuss kitu akaniambia shut up naangalia katuni.

Nikamwambia ntazima TV kama ndio inakupa jeuri akajibu "kwani siwezi kuwasha"

Nilichomoa adapter ya king'amuzi ukutani na hakuna aliyeniambia kitu
Hayo ndiyo mambo ya Kitanzania halafu tunajifanya tunajuwa.

Kwanza "sitting room" si pahala pa kuweka TV. Sitting room ni kwa ajili ya kukaa kuongea na wageni. Kuweka tv sitting room, watoto hapohapo, wageni hapohapo, ni kujikaribishia mmomonyoko wa maadili tu.

Ulivyoizima ulifanya la maana sana na ungewapa darsa, wasiweke tv chumba wanachokaribisha wageni.
 
Sasa Kama Nyumba ni ndogo na Ina sitting room moja tu TV iwekwe wapi unapendekeza!!?
 
Sasa Kama Nyumba ni ndogo na Ina sitting room moja tu TV iwekwe wapi unapendekeza!!?
Isiwashwe kabisa wanapokuja wageni au muda mnapokaa kuongea kama familia. Ni kujipangia utaratibu tu.
 
Niliwahi kufika kwenye nyumba Fulani dogo alikuja na sindano anataka kunichoma mama yake akasema usikwepe atalia Sitasahau nilisepa hapohapo [emoji16]
Hahha Mimi ningechapa Kofi kama ingenichoma hiyo sindano hahah
 
Isiwashwe kabisa wanapokuja wageni au muda mnapokaa kuongea kama familia. Ni kujipangia utaratibu tu.
Kumbe wwe huwajui kina Junior,wao wanapoona wageni ndiyo huwa Sasa Wanaanza vituko vyao, Mara watake kuaangalia tv, yaani mradi fujo tu hapo Sebuleni!!
 
Upo sahihi kabisa, vitoto vingi vya kizazi hiki havina adabu. Katoto hakakufahamu kanakurukiarukia kama ngedere, halafu unakuta kenyewe ni ka-kike. Malezi ya ki-zungu yanachangia kwa kasi sana kuporormosha misingi ya malezi mazuri. Huko mbeleni tutakosa taifa lenye maadili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…