Watu 12 wakamatwa kwa kula hadharani mchana Zanzibar
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja linawashikilia watu kumi na mbili kwa tuhuma za kukutwa wakila mchana hadharani kipindi hiki cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan ambao wanaifanya kuwa idadi ya watu waliokamatwa kwa tuhuma za kutenda makosa mbalimbali kufikia sitini na mbili

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini magharibi Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Abubakar Khamis Ally amesema kufuatia video iliyosambaa mitandaoni ikiwaonesha baadhi ya watu katika eneo la viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar wakila hadharani wakati wa mchana wa Ramadhani, Jeshi hilo lilifanya msako na kuwakamata watu wapatao kumi na mbili wakiwa na vielelezo ambapo amesema wanaendelea na taratibu nyengine ili kuwafikisha Mahakamani.

Aidha ameyataja makosa mengine ni pamoja na unyang’anyi, Madawa ya kulevya na makosa mengine ambapo watuhumiwa wanashikiliwa na Polisi na wengine tayari wameshahukumiwa Mahakamani.
Hizi dini shurutishi hapana.
 
Zanzibar ina utaratibu wake iliyojiwekea kwakuwa asilimia kubwa ya wakazi wa kule waislamu,,,,haitakiwi kula hadharani period.

Je tunashindwa kuheshimu hilo kwa mwezi mmoja tu? Tatizo letu sisi tunaingiza udini hapa ukristo vs uislamu.

Lakini tukitoa hiyo kutu akilini kwetu tutaona kwamba hiyo sheria na lazima ifuatwe period.

Tuache kila siku kulialia Zanzibar zanzibar pumbavu!
yani afunge muhisilam mimi inanihusu mini? et mwezi mtukufu shenziiii
 
Zanzibar ni dola la kiislam?

serikali ya Zanzibar inaongozwa na katiba ya kiraia au Quran?

mahakama zinashtaki waliokamatwa wanakula wakiwemo wakristo kwa sheria za kiislam?

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Zanzibar ACP Abubakar Khamis Ally amesema Jeshi hilo litaendelea kuwakamata wale wote wataoonekana au kukutwa wakila chakula mchana hadharani katika mwezi huu mtukufu kwa waislam ramadhani.

ACP Abubakar Khamis Ally amenukuliwa na AyoTV akisema “Kwa mwezi huu kwa ramadhani kwa tamaduni ya Nchi hii hata sehemu za vyakula utakuta zimefungwa kwahiyo sio vyema wakakaa maeneo wakala hadharani hilo ni kosa na ndio maana tunawakamata na tutaendelea kuwakamata kwani inaleta kero kwa wengine”

Hadi sasa ni Watu 12 wamekamatwa kwa kosa hilo

MY TAKE:

Suala la mfungo wa Ramadhan ni la kidini sio utamaduni, kusema kwamba kwavile Zanzibar imejaa waislam ni utamaduni au utaratibu wao hivyo kila mtu afuate hata wasio waislam sio sawa, huu ni ubaguzi wa kidini, hivi kwakuwa bara wamejaa wakristo tukisema adhana zipigwe marufuku kwavile sio utaratibu wetu, hiki ni nini kama sio udini ? kitekelezwe kwakuwa ni utamaduni / utaratibu ? NO !!

huu ni mwezi mtukufu wa Ramadan kwa waumini lakini kuna wasio waumini huu mwezi kwao ni wa kawaida waachwe waendelee na maisha yao ya kawaida

Tanzania (bara na visiwani) ni nchi huru kila mtu ana uhuru wa kufanya anachotaka maadam havunji sheria za nchi (sio za dini), kila mtanzania ana haki ya kula hadharani
Wazanzibar hatuendani nao bora tupeane talaka tokomea....🙂
 
Mfahamu hapa inatumika hekima ya tamaduni sio dini.

Mfano kule ulaya kuna tamaduni matamasha ya LGBT jee hapa Tanzania wakisema waje wafanye mtakubali kwa tamaduni zenu?.
Wee jamaa ujue umejibu ki genius sana japo wewe mwenyewe unaona kawaida tu...🤔🤔🤔🤔
 
Zanzibar ni upuuzi mwingi sana,kuna mtu wangu wa Karibu yupo kule, Jumapili iliyopita,walienda Kanisani kuwaambia wapunguze music wamefunga,wakati wao maspika Usiku tarawei,pia wengi wao wanashinda njaa tuu.Hawa jamaa bara wako huru ila kwao wanaroho mbaya sana, Jumapili pale michenzani waligoma kuniuzia maji,eti tumefunga,pumbavu kabisa
 
Umeanza vizuri tuu ila huku mwisho sasa umepuyanga puyanga 😂😂😂😂😂
 
Zanzibar being predominantly Muslim, during Ramadan, everyone is expected to adhere to the Islamic teachings of fasting from dawn to dusk, at least in public. It is not against the law to eat publicly rather considered polite.

Hiki ndicho google inasema.

Lakini sidhani kama kuna sheria ya dini inasema hivyo ni mihemko ya watu kama asemavyo member M Z A N Z I B A R I
Hapana bwana! Ni kwamba ule lakini kwa staha na siyo hadharani ovyo ovyo tu. Ujue watu wengi wanafanya sifa katika kula wewe mwenyewe shahidi watu kutafuna ovyo tu masokoni na na barabarani
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja linawashikilia watu kumi na mbili kwa tuhuma za kukutwa wakila mchana hadharani kipindi hiki cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan ambao wanaifanya kuwa idadi ya watu waliokamatwa kwa tuhuma za kutenda makosa mbalimbali kufikia sitini na mbili

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini magharibi Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Abubakar Khamis Ally amesema kufuatia video iliyosambaa mitandaoni ikiwaonesha baadhi ya watu katika eneo la viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar wakila hadharani wakati wa mchana wa Ramadhani, Jeshi hilo lilifanya msako na kuwakamata watu wapatao kumi na mbili wakiwa na vielelezo ambapo amesema wanaendelea na taratibu nyengine ili kuwafikisha Mahakamani.

Aidha ameyataja makosa mengine ni pamoja na unyang’anyi, Madawa ya kulevya na makosa mengine ambapo watuhumiwa wanashikiliwa na Polisi na wengine tayari wameshahukumiwa Mahakamani.
Kujiona Dini yao muhimu kuliko imani za wengine ni ukosefu wa busara
 
Back
Top Bottom