Zanzibar ni dola la kiislam?
serikali ya Zanzibar inaongozwa na katiba ya kiraia au Quran?
mahakama zinashtaki waliokamatwa wanakula wakiwemo wakristo kwa sheria za kiislam?
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Zanzibar ACP Abubakar Khamis Ally amesema Jeshi hilo litaendelea kuwakamata wale wote wataoonekana au kukutwa wakila chakula mchana hadharani katika mwezi huu mtukufu kwa waislam ramadhani.
ACP Abubakar Khamis Ally amenukuliwa na AyoTV akisema โKwa mwezi huu kwa ramadhani kwa tamaduni ya Nchi hii hata sehemu za vyakula utakuta zimefungwa kwahiyo sio vyema wakakaa maeneo wakala hadharani hilo ni kosa na ndio maana tunawakamata na tutaendelea kuwakamata kwani inaleta kero kwa wengineโ
Hadi sasa ni Watu 12 wamekamatwa kwa kosa hilo
MY TAKE:
Suala la mfungo wa Ramadhan ni la kidini sio utamaduni, kusema kwamba kwavile Zanzibar imejaa waislam ni utamaduni au utaratibu wao hivyo kila mtu afuate hata wasio waislam sio sawa, huu ni ubaguzi wa kidini, hivi kwakuwa bara wamejaa wakristo tukisema adhana zipigwe marufuku kwavile sio utaratibu wetu, hiki ni nini kama sio udini ? kitekelezwe kwakuwa ni utamaduni / utaratibu ? NO !!
huu ni mwezi mtukufu wa Ramadan kwa waumini lakini kuna wasio waumini huu mwezi kwao ni wa kawaida waachwe waendelee na maisha yao ya kawaida
Tanzania (bara na visiwani) ni nchi huru kila mtu ana uhuru wa kufanya anachotaka maadam havunji sheria za nchi (sio za dini), kila mtanzania ana haki ya kula hadharani .