Watu 12 wakamatwa kwa kula hadharani mchana Zanzibar
Ishu ni kwamba zanzibar si nchi ya kiislam, kama vipi basi iwe ya kiislam, iwe kama Nigeria kaskazini palipo na sharia za kiislam. Sehemu hiyo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iwe na sharia za kiislam na ijulikane hivyo kuliko kujifanya ni nchi ya kisekula huku inakumbatia udini/uislam. Udini ulikemewa sana Tanzania na hautakiwi kumea na kukua katika nchi isiyoongozwa kwa itikadi za kidini
Hapo hakuna Udini bali kuna siasa za kuwaadaa waisilamu wasio jitambua serikali gani ya kidini inayo kopa kwa riba na kukopesha kwa riba serikali gani ya kidini kiongozi wake anayepatikana kwa sanduku la kura serikali gani ya kidini ambayo kuna mchanganyiko wa wanawake na wanaume kwenye uongozi serikali gani ya kidini inayo kumbatia ufisadi na ukabila upemba na uunguja na ubara hapo hakuna dini bali wametunga sheria hiyo kuwadanganya waisilamu wasio jitambua
 
Kwani mtu Kula chakula mchani kipindi cha mfungo ni uvunjifu wa katiba ya nchi?
Watu wajinga wajinga ndo wapo very attached kwenye mambo ya dini.
 
Hiyo sheria ipo kabla wewe hujazaliwa tii sheria bila shuruti huwezi baki kwenu tanganyika
Hiyo sasa ni sheria au ni upuuzi! Mnalazimisha watu kufunga ili iweje sasa!! Hopeless kabisa nyinyi.

Halafu unafikiri mimi na akili zangu timamu naweza kuishi eneo lenye watu wenye vichwa flat!!
 
Kwahiyo ni lini Serikali ya Mapinduzi itaanza kuwafunga Watu ambao hawaswali hawaendi Makka kuhiji hawatoi Zaka na Ibada nyingine za Kiislamu mbona inakomalia kwa Watu wanaokula mchana kwenye Ramazani?
 
Kwahiyo ni lini Serikali ya Mapinduzi itaanza kuwafunga Watu ambao hawaswali hawaendi Makka kuhiji hawatoi Zaka na Ibada nyingine za Kiislamu mbona inakomalia kwa Watu wanaokula mchana kwenye Ramazani?
Hilo nalo neno !😅
😂😂
 
Mbona Waisilamu wa Bara hawalazumishwi na Serikali kufunga na wanafunga wengine hawafungi kila Mtu anakuwa Huru kuijamulia mambo yake.

Kwa hiyo Waisilamu wa Zanzibar hawamuamini Allah mpaka watishiwe kufungwa Jela ndio wafunge?
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja linawashikilia watu kumi na mbili kwa tuhuma za kukutwa wakila mchana hadharani kipindi hiki cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan ambao wanaifanya kuwa idadi ya watu waliokamatwa kwa tuhuma za kutenda makosa mbalimbali kufikia sitini na mbili

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini magharibi Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Abubakar Khamis Ally amesema kufuatia video iliyosambaa mitandaoni ikiwaonesha baadhi ya watu katika eneo la viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar wakila hadharani wakati wa mchana wa Ramadhani, Jeshi hilo lilifanya msako na kuwakamata watu wapatao kumi na mbili wakiwa na vielelezo ambapo amesema wanaendelea na taratibu nyengine ili kuwafikisha Mahakamani.

Aidha ameyataja makosa mengine ni pamoja na unyang’anyi, Madawa ya kulevya na makosa mengine ambapo watuhumiwa wanashikiliwa na Polisi na wengine tayari wameshahukumiwa Mahakamani.
Mambo ya hovyo kabisa
 
Mkuu unatetea basi tu. Hili ni tatizo, niambie na hawa walikuwa wanakula hadharani?


Sio kila kinachoandikwa kwenye mitandao ni cha kuamini
 
Zanzibar being predominantly Muslim, during Ramadan, everyone is expected to adhere to the Islamic teachings of fasting from dawn to dusk, at least in public. It is not against the law to eat publicly rather considered polite.

Hiki ndicho google inasema.

Lakini sidhani kama kuna sheria ya dini inasema hivyo ni mihemko ya watu kama asemavyo member M Z A N Z I B A R I
Kwani mfungo huwa ni lazima ?
 
Sasa kula hadharani linakuwaje kosa wakati kufunga ni suala binafsi la muamini husika ?
Wakulaumiwa ni serikali kwa kuendelea kuisimamia amri hiyo hata baada ya mapinduzi kwa kujificha kwenye hoja ya utamaduni.

Napingana na wanaosema sheria hiyo ipo kwenye uislamu, mtume aliishi na jamii tofauti za watu, sijawahi kuona andiko linalounga mkono matendo hayo kwenye uislamu

Hii hapa taarifa ya mwaka 2017, naibu waziri akijibu swali la mwakilishi wa PAJE.

Ni wapi kataja sheria ya kiislamu hapo,
Screenshot_20240329-123605_Chrome.jpg
 
Wakulaumiwa ni serikali kwa kuendelea kuisimamia amri hiyo hata baada ya mapinduzi kwa kujificha kwenye hoja ya utamaduni.

Napingana na wanaosema sheria hiyo ipo kwenye uislamu, mtume aliishi na jamii tofauti za watu, sijawahi kuona andiko linalounga mkono matendo hayo kwenye uislamu

Hii hapa taarifa ya mwaka 2017, naibu waziri akijibu swali la mwakilishi wa PAJE.

Ni wapi kataja sheria ya kiislamu hapo,
View attachment 2948045
Ni kweli uislam hauna tatizo mimi nimekulia kwenye jamii ya waislamu, nashirikiana na waislamu kwenye nyakati zote hata za mfungo akikuta kwako unakula atakaa pembeni wewe utaendelea kula.

Hii sheria serikali haipaswi kuitekeleza kwa sababu inajenga chembechembe za ubaguzi kwa watu wasio waislam na wale ambao hawajafunga tu kwa hiari zao.
 
Lakini kwanini ule hadharani mwezi wa ramadhsni? Kila nchi ina by-laws zake kama huwezi kuzitii ondoka hilo eneo neenda pale unapo ona kuna usalama kwako.
By
Nakumbuka 2020 nimekamatwa pale CCM bar- Michenzani kisa nakula kipindi cha Corona. Niliteswa sana na Askari Police wa Kizanzibar. Wakinena maneno ya Wewe Mbara acha kuzingua

Zanzibar ni dola la kiislam?

serikali ya Zanzibar inaongozwa na katiba ya kiraia au Quran?

mahakama zinashtaki waliokamatwa wanakula wakiwemo wakristo kwa sheria za kiislam?


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Zanzibar ACP Abubakar Khamis Ally amesema Jeshi hilo litaendelea kuwakamata wale wote wataoonekana au kukutwa wakila chakula mchana hadharani katika mwezi huu mtukufu kwa waislam ramadhani.

ACP Abubakar Khamis Ally amenukuliwa na AyoTV akisema “Kwa mwezi huu kwa ramadhani kwa tamaduni ya Nchi hii hata sehemu za vyakula utakuta zimefungwa kwahiyo sio vyema wakakaa maeneo wakala hadharani hilo ni kosa na ndio maana tunawakamata na tutaendelea kuwakamata kwani inaleta kero kwa wengine”

Hadi sasa ni Watu 12 wamekamatwa kwa kosa hilo

MY TAKE:

Mfungo wa ramadhani ni suala la Dini sio utamaduni, kusema kwamba kwavile Zanzibar imejaa waislam ni utamaduni au utaratibu wao hivyo kila mtu afuate hata wasio waislam sio sawa, huu ni ubaguzi wa kidini.

huu ni mwezi mtukufu wa Ramadan kwa waumini tu, wasio waumini waachwe waendelee na maisha yao ya kawaida, jambo lisilo la wote lisilazimishwe kuonekana ni la wote kiasi cha kutumia mpaka polisi.

Tanzania (bara na visiwani) ni nchi huru kila mtu ana uhuru wa kufanya anachotaka maadam havunji sheria za nchi (sio za dini), kila mtanzania ana haki ya kula hadharani
waitangazie umma kwamba wao ni dola ya kiislamu
 
Wacha porojo hizo sheria zipo kabla wewe hujazaliwa tena hilo kosa hukumu yake ni mwaka mmoja jela na viboko 12 sita ukiingia na sita ukitoka tii sheria bila shuruti huwezi baki kwenu tanganyika
Huu ni upunguani, au iliandikwa kipindi bado mpo utumwani na sultani anawacharaza viboko huku mnatumikishwa kwenye mashamba ya karafuu

Kweli utumwa uliwaathiri sana sasa endeleeni kukumbatia desturi za mabwana zenu wa kiarabu
 
Back
Top Bottom