Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
LGBQT imeharamishwa na katiba ya Tanzania, kula hadharani wakati wowote hakujaharamishwa na katiba au sheria yoyote.Mfahamu hapa inatumika hekima ya tamaduni sio dini.
Mfano kule ulaya kuna tamaduni matamasha ya LGBT jee hapa Tanzania wakisema waje wafanye mtakubali kwa tamaduni zenu?.
Kwani hao wanaoukala hadharani wewe wanakuwasha nini wewe ambaye huli?? Si uendelee na mambo yako au unatamani na kumezea mate ukiona mtu anakula hadharani.Zanzibar ina utaratibu wake iliyojiwekea kwakuwa asilimia kubwa ya wakazi wa kule waislamu,,,,haitakiwi kula hadharani period.
Je tunashindwa kuheshimu hilo kwa mwezi mmoja tu? Tatizo letu sisi tunaingiza udini hapa ukristo vs uislamu.
Lakini tukitoa hiyo kutu akilini kwetu tutaona kwamba hiyo sheria na lazima ifuatwe period.
Tuache kila siku kulialia Zanzibar zanzibar pumbavu!
Na ukifuatilia hizi thread zinazoashiria udini udini zikianzishwa utaona zinapata wachangiaji wengi haraka sana kuliko zile thread zinazohusu wizi wa mali za Nchi au kuhusu maendeleo ya Nchi hii !Ndio maana nimesema kama mtatazama kwa mlengo huo mtalialia kila siku
Kisiwa cha Zanzibar si cha WaarabuTii sheria bila shuruti huwezi baki kwenu tanganyika
Itanielekeza kula kama kawaida ambavyo huwa nakula siku zote.busara kwa kawaida itakuelekeza nini
Usitufanye wajinga
fuatilia mjadala ulipoanzia, usiwe unakurupuka kujibu kama mpumbavuWacha porojo tii sheria bila shuruti huwezi baki kwenu tanganyika
Serikali ya Zanzibar na kadhi na balaza lake wanawahadaa waisilamu wajinga wasio jitambua hili wadhani serikali yao ni ya kidini kumbe uongo mtupu ndio maana baadhi ya watu hata wakimfahamu jirani yao anapika na kula mchana nyumbani kwake wanapiga simu hali yakuwa hakuna katazo hilo kwenye dini bali ni siasa tuJeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja linawashikilia watu kumi na mbili kwa tuhuma za kukutwa wakila mchana hadharani kipindi hiki cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan ambao wanaifanya kuwa idadi ya watu waliokamatwa kwa tuhuma za kutenda makosa mbalimbali kufikia sitini na mbili
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini magharibi Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Abubakar Khamis Ally amesema kufuatia video iliyosambaa mitandaoni ikiwaonesha baadhi ya watu katika eneo la viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar wakila hadharani wakati wa mchana wa Ramadhani, Jeshi hilo lilifanya msako na kuwakamata watu wapatao kumi na mbili wakiwa na vielelezo ambapo amesema wanaendelea na taratibu nyengine ili kuwafikisha Mahakamani.
Aidha ameyataja makosa mengine ni pamoja na unyang’anyi, Madawa ya kulevya na makosa mengine ambapo watuhumiwa wanashikiliwa na Polisi na wengine tayari wameshahukumiwa Mahakamani.
Hicho kijamaa kijinga sana kinaonekana hakijielewiacha ujinga wewe, kwani tanganyika haina waislam, iweje chakula kiliwe mchana kweupe kwenye migahawa iliyopo misikitini na walaji hawakamatwi? Zanzibar ina udini mwingi sana inapaswa kukemewa kwa hilo
Amri ni Sheria? Hiyo siyo nchi ya kifalme kwamba asemalo Rais limeshapita,either wekeni hiyo Sheria Kwenye maandishi au kaeni kimya..jifunze kutofautisha kati ya sheria za dini na sheria za kiserikali.
hilo swala limekuwepo tokea utawala wa karume,
je karume alipitisha amri hiyo akiwa kama kiongozi wa kiislamu au kama kiongozi wa serikali ya mapinduzi.
Mjinga kama wewe unatakiwa ujiulize swali kama hilo
Adhana inamaana kubwa sana chief,,, ukiacha kuwaita watu Katika swala lkn ni ulingano ambao unamlingani mwanadamu amtambue Mola wake
Inatangaza ukubwa wa Mwenyezi Mungu, inatangaza hakuna mola mwingine apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mungu mmoja tu wa kweli, hapa hakuna baba, mwana wala roho
Na inamtangaza Mtume ambaye ni wa mwisho na hatokuja mwingine naye ni muhammad, ambaye Mimi na wewe tunatakiwa kumfuata iii tuongoke.
Kwahiyo adhana ni ibada
Subiri tutakapogeuza znz kuwa wilaya ya mkoa wa Pwani, sheria zote za kijinga kama hiyo zitayeyuka, wala hatuhangaiki kufutaNjoo uzifute
Kwani dhambi inayofanyika Zanzibar ni kula mchana wa ramadhani tu hizi nyingine wanamuachia nani?riba pombe uzinzi ushoga ufisadi?kama wameamua kama serikali imeamua kusimamia dini isichague dhambi zinazo tendwa na wanyonge tukwa zanzibari wacheni walinde mila na desturi zao.
kinachotakiwa hapo ni kuheshimu utaratibu wao walio jiwekea ktk kipindi hiki cha mwezi mtukufu, kama unajiona huwezi kufuata utaratibu wao usiend au ondoka kwa muda huu.
28 March 2024
Zanzibar
Na kamanda ayataja majina yao na kabila zao waliokamtatwa wakila mchana hadharani :
View: https://m.youtube.com/watch?v=l4mmqjdRX3o