Watu hawataki kutembeleana siku hizi, kila mmoja yuko bize kusaka shilingi

Kwa mzee mtu mzima si vizuri akakufuata wewe ulipo
 
Individualism ni nzuri sana katika kuleta maendeleo collectivism ya kiafrika ina upumbavu mwingi ambao ni unnecessary kama huu wa kutaka Kujuana juana.

Inshort sipendi mazoea ya hovyo hovyo na mtu katika maisha yangu binafsi regardless huyo mtu ni ndugu yangu wa damu au laaah!.
 
Hii iko vizuri kama itatekelezwa; ingawa umbali wa kijiografia unaweza kuwa tatizo kwa baadhi ya maeneo
 
Kwa hali hiyo, kuna dalili zozote itakuja kutokea tukaishi kama zamani?
 
Inasaidia kupunguza conflicts za kipumbavu , tabia ya unafiki na umbea wa Kitanzania ni kero sana , Individualism ndio solution ,kila mtu apambane na hali yake.
Watz sio watu wa kuintertain kabisa ,unalikaribisha jitu kwako kesho linaenda kumwaga umbea ,Majungu na chuki + unafiki tu .
 
Si hivyo tu siku hizi adui hatoki mbali.

Unamkaribisha mtu kwako kumbe kaja kuchunguza unaishi vipi akakutangaze.

Kila mtu akae kwake tutakutana kwenye matukio, harusi au misiba
Kitu kipi kilichosababisha uadui uongezeke? Je maisha ya unayoishi sasa yanakupa furaha?
 
Labda ukiwa hoi kitandani (hospitali) kwa muda wa miezi mitatu, utapenda watu wangapi waje kukujulia hali?
 
Biblia imesema nyakati za mwisho upendo wa watu utapoa na inaonekana katika hili kuna mazingira mengi yanayoweza kuchangia hali hii. Mimi niliwahi kuwa na hali fulani ya maisha ya kawaida tu ya mkate na chai nikapambana sana na ndugu na jamaa kila aliyekuja Mkoani hapa alifikia kwangu sasa baadae mambo yaka yumba kidogo nakwambia huko kijijini hakuna ambaye hakuwa na taarifa hizo mbaya zaidi hawa ambao mimi niliwapokea na kuwapa mwongozo wa maisha wakageuka kuwa mwiba kwangu tena, sasa mazingira kama haya pia yanapunguza upendo na ukaribu kama mtu huna moyo mkuu huwezi endelea vizuri na ndugu, jamaa na marafiki.
 
Kwa hali hiyo, kuna dalili zozote itakuja kutokea tukaishi kama zamani?
Haitatokea aise.
Maana hata siku za utafutaji zimeongezeka. Watu hadi siku za wikiend wanahangaika kwenye mishemishe, wengine ndiyo muda wa kwenda bar kunywa, kuangalia mpira na michepuko (usasa ni mwingi).
Unaweza kufika kwa ndugu yako, akakuambia twende huku, kumbe bar. Ukitoka hapo saa 4 usiku, unalala, kesho ndugu yako kwenye mishemishe, unabaki wewe mwenyewe.
Unaweza kujikuta hapo nyumbani kwa ndugu yako umebaki wewe tu.
Mama yupo na kibanda chake cha nyanya anarudi usiku, watoto shule, wakirudi ni misele mpk usiku, ndugu yako anarudi saa 4 usiku. Haina maana.
Kibaya zaidi pesa hakuna halafu mahitaji ni mengi
 
Ni kweli wapo wanaokatisha tamaa; swali ni kwanini wao wamebadilika na kuwa maadui?
 
Kwa mazingira hayo, wengi hatufurahii maisha kwa sababu muda mwingi tuko bize kwenye kutafuta shilingi, mwingine jumatatu mpaka jumapili muda wote ni bize; katika hali hii tukisema maisha ni utumwa tutakuwa tumekosea?​
Ndiyo ni utumwa.
Kama sehemu yenye changamoto ya usafiri kama dar (Foleni)
Mtu anaamka saa 10 usiku anawahi usafiri anafika kazini saa 2 asubuhi.
Anarudi saa 6 usiku asubuhi saa 10 tena anaamka.
Maisha kwasasa ni utumwa halafu kibaya zaidi pesa haionekani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…