Watu 'Powerful' 12 ni akina nani hadi waachiwe kuharibu Bonde la Ihefu?

Hakuna kitu kama ubongo wa Taifa. Kila kitu kinaanza na kuisha na raia walio wengi wenyewe. Kama raia mlio wengi hamna akili hata mngepewa CIA au Mossad wawaendeshe mtabaki mafukara tu.
Tatizo unafikiri huo ubongo utabeba mawazo ya wachache! Ulinzi na usalama ni wa raia wote lakini mipango na mbinu si kazi ya raia wote!
 
ccm watupu hapo, mchwa wa taifa hili wapo kazini kama kawaida yao!
Hongera sana kamanda Balile, uwe makini hawa watu kumwaga damu ni asili yao.
 
Kikwete aliwafunga mawaziri wastaafu, vigogo wa polisi, Magufuli amemfunga nani kwa ufisadi? Sugu na madiwani wa Chadema?
Magufuli tena kaingiaje mbona mimi sijamtaja? Mie nimesema tu Kikwete alitambulika kuwa ni rais dhaifu basi.
 
Walikuwepo before JPM na wapo after JPM Mnazani Magu aliweza kumgusa kila mwizi TZ kuna royal families ambazo hazigusiki
Hayo aliyoweza kuyagusa tu imekuwa balaa imemfanya achukiwe na mwishowe ikaonekana kafa kwa sababu hakuwa mtu mzuri kwa maana wazuri hawafi.
 
Nimemsikiliza ndugu yangu Balile! Kwa aliyosema ni mambo mazito yanayofanya kama Taifa tujiulize mamlaka zetu hasa za usalama wanamuogopa nani kwenye ulinzi wa rasilimali zetu?

Balile binafsi nimekupa heshima ya pekee kwa hili.
Hatuna viongozi ila tuna midoli tu iko pale imekaa
 
Hakuwa na lolote yule jamaa , mdogo wa Rostam Aziz alipodakwa na Makontena ya meno ya tembo pamoja na mibunduki kadhaa ya kivita , Jiwe alikubali Rushwa ya Channel 10 ili yaishe.

Umesahau hili ?
Bora hata huyo aliwakamata!

Vipi hawa mirenda wa sasa hivi umeona hata wamekamata mtu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…