Wauzaji wa bidhaa za forever living mnaboa sana!

Wauzaji wa bidhaa za forever living mnaboa sana!

Hakuna biashara ngumu kama hiyo, kwanza unatakiwa kuwa muongo yaani kusema mafanikio makubwa uliyonayo au aliyonayo mwingine ili umvutie kujiunga. Marafiki zangu wote walinikwepa, kila nikikutana nao wanajua nawapa stori za forever. Nikaona huu upuuzi tu, nikaamua kuachana nayo na sitaki hata kuisikia.
Pole sana na hongera kwa kuwa mkweli
 
Sio kwa vicheko hivi, lazma unahusika na forever living
Mwenzangu mnanifurahisha asubuhi kwa nini nisicheke? Afu nafurahi kuona watu wanaiona kweli. ... kifungo cha fikra ni kibaya sana. ..all in all forever living owners ni wamarekani. ..I guess umeipata point yangu 'fikra kufunguka' have a blessed Saturday. ..
 
Mimi walinifuata kibo complex hapa tegeta wakanunua machips na kuku, nikapiga na bia zao jamaa wana story kibao. Nilivyochoka kusikiliza nikaondoka zangu.
 
hata umachinga ni deal sana kuliko forever pili hawa jamaa wajinga bei zao juu sana halafu huwezi nunua bidhaa hadi uwe member duuh hapo ndoo nachoka.
ila niliwahi mtongoza demu mmoja wa forever then biashara ndoo ikawa basi tena yani unakutana na demu mkali lazima ufanye application huwezi jua.
 
Wanaboa sana.Alafu usijiroge kuingia katika hiyo biashara.Itakula kwako tu.Hizo bidhaa haziuziki.Ni aghali mnoo alafu ubora wa kawaida tu.Wanaofaidika ni watu wachache tu amboa ni waasisi wa Forever hapa nchini.
 
Mimi walinifuata kibo complex hapa tegeta wakanunua machips na kuku, nikapiga na bia zao jamaa wana story kibao. Nilivyochoka kusikiliza nikaondoka zangu.
Wanagaramia hadi misosi ili tu uone bidhaa jinga sana, mie nlipewa ka fanta na vibagia nlivokua na hasira nkakanywa fasta tu gudugudugudu nkaweka chupa pembeni nikaendelea kununa
 
Hii mbinu ya kuwaita watu na kuwapa vinywaji na chakula watawapata wengi kumbe..
mimi siku zote nikiona kitu sikielewi elewi huweni kunishawishi

eti semina halafu hujui semina inahusu nini....na unaenda?


Hizi mbinu wanazopewa hizi kama mkeo yuko huko na akili za kushikiwa 'watamlamba hadi basi'
manake wauzaji wote wa bidhaa za mtandao wako so desperate kushindana kuleta member wapya
na kuuza bidhaa....
Kumlamba nini.?
 
hi michezo ya pyramid nilicheza 2009 kabla hata ya hizi za forever ilikua ya waitaliano ila nilijuta, walinipiga 500K ditaki hata kuwasikia hawa watu
 
We acha tu, mtu unakuwa muongo mpaka kwa wazazi, Mara ukijiunga utapata gari, utajenga nyumba, utazawadiwa safari ya kwenda marekani kumuona Mkurugenzi wa kampuni, utapewa tiketi ya ndege kwenda south nk yaan uongo mtupu
Halafu anayekuambia yote hayo hajawaki kuwa nayo au kuyafanya
 
Back
Top Bottom