Waziri Gwajima atangaza kumchukulia hatua za kisheria Masha Love na wanaochochea kuharibu maadili

Waziri Gwajima atangaza kumchukulia hatua za kisheria Masha Love na wanaochochea kuharibu maadili

Binafsi mimi hawa Ustawi niliwauliza hili Swali

Na mpaka sasa zaidi ya wiki sijapatiwa jibu

Hayo mengine nadhani Serikali na Sheria zetu zinaweza kuyahimili, (na wengine wanaweza kusema kwenda sana huko ni kuwa na a Police State)
 
Nonsense,cheap popularity,Dkt. Gwajima D una mambo mengi ya kufanya na watanzania tuna shida nyingi sana kuliko huu upuuzi ,mfatilie pia yule mkuu wa mkoa aliye Binti wa chuo kikuu sauti ,ukimalizana na Nawanda

Ukifanya haya nitajua uko siriazi na kazi yako

IQ yako iko chini sana..!!
 
Na hoja ya kuna mengi ya kufanya, uko sahihi, ni kweli yapo mengi na katika hayo mengi ni likiwemo na hili la kusimamia maadili, labda kama hufahamu tu majukumu ya wizara hii. Siyo vibaya kutofahamu kwani unaweza kurejea tu taarifa zetu ziko online, upi ni wajibu wetu kwenye maadili ambayo, ulikuwa mjadala wa nchi tarehe 17 Mei 2024 bungeni, labda kama mwenzetu huwa hufuatilii chochote kingine zaidi ya nikiingia kwenye ajenda hizi tu. Jitahidi basi kuwa unafuatilia mambo mengi mengi pia.

Ahsante Sana kwa kuendelea kuinua sauti ya kazi za wizara hii.
Waziri mimi nakuunga mkono,hawa wasanii wapuuzi wengi sana isiishie kwa huyo tu nenda mpaka kwa wale wanaoshabikia ushoga mfano WCB wana mashoga wengi mule kwa kigezo cha ubunifu.

Uchafu wanaofanya unaharibu sana kizazi kuonekana ushoga ni kitu cha kawaida au ndo sanaa,mfikishie na waziri wa sanaa haya.
 
Mkuu ukimalizana na Masha Love mtafute na Zuchu mwambie zile tabia zake anazozifanyaga kila anapokua jukwaani apunguze au aache maana anatuharibia watoto huku mikoani
 
Nakubaliana na wewe. Kwani tunapigana mishale tu hata hatusogei kisa wengine hata hawajui siyo muundo wa serikali, siyo Sheria na siyo majukumu ya wizara na miundo mingine ya nchi.

Yaani unakuta yule anayejitoa afanyie kazi mambo sugu yaliyoshamiri kinyume na sheria ndiye anayeshambuliwa kisa tu watu baadhi walizoea tofauti wakadhani mazoea ndiyo kawaida. Ukiacha kufanya wengine wakuhoji tena, usipokuwa na msimamo uyumbe yumbe.

Kumbe hapa ni elimu ya uraia... Ngoja nitafute wadau waje watoe elimu watu wajue, vinginevyo Sheria hizi tunazitaka Sana ila kutakuwa hakuna utekelezaji, na miundo hii tutaunda na bila majukumu kufahamika itakuwa hakuna ushirikiano, ukweli usemwe Ili twende sawa pamoja ndugu katika 🇹🇿

Ahsante Sana
Dunia kwa Sasa ni kama Kijiji,kuna Mambo tunafanya huku uraiani hatujui kuwa ni kosa, Mfano:Mtu mzima anamtuma mtoto kununua sigara na pombe,Kisa ni mtoto wake,ni mengi kubeba mnyama kichwa chini miguu juu,nk .
 
Hivi Masha kafanyaje?? Nilikua nimefungwa ndo nimeachiwa huru leo...
"alisikika kijana mmoja wa hovyo huko instagram😄😄😄"
Haalafu huwezi kuamini! Binafsi nimesoma kuanzia page ya 1-3! Sijaelewa huyo Mashalove ni nani, na amefanya nini kiasi cha mtoa mda kumjia juu Mh. Waziri! Na kila anayeonekana kuwa upande wa Waziri kuonekana ni CHAWA!!

Nadhani kama kuna mtu mwenye ABC ya huu mtafaruku, angetuwekea humu jukwaani sisi tusio na access ya mitandao mingine nje ya jamii forums!
 
Mbona ameshafuta na mambo yote huko online ambayo ameshajua yalikuwa hayafai. Unajua watu wengi hawajui lipi ni kosa, na Sheria ni ipi. Pale unapomwambia hili ni kosa, akajua akajuta akaondoa, una Sababu gani kwa mfano ya kutomkanya? Mabadiliko yanahitaji hatua nyingi Sana na mojawapo muhimu, ni mtu kutambua na kujutia kosa lake. Alikuwepo babu wa TikTok, alijua na akajutia na akabadilika.
Mh. , shida ni kwamba matukio ni yaleyale kila wakati. Onyo kwao lishakuwa sugu, hamna budi kutazama njia nyingine. Kwa nini wafanye vitu ambavyo wanajua kabisa sio sahihi? Nanyi mtakuwa na kazi hiyo hiyo ya kuonya kila wakati? Dkt. Gwajima D
 
Cheap popularity sasa Mimi inipeleke wapi kwa mfano? Yaani inisadie nini hasa wewe unavyodhani. Si usinipe tu hiyo popularity yaishe😀

Mimi nasimamia Yale ambayo nyie watanzania mmeyawekea Sheria ambazo zinatakiwa kusimamiwa kwa ajili ya kujenga maadili na kuwalinda watoto wenu. Ni hilo tu. Sheria ya mtandao kifungu cha 14 kasome Kiko online. Hii habari ya kuuliza serikali ina mkakati gani na mpango gani na Sheria ziko wapi, muwe mnakumbuka kuwa vyote vipi, na tukianza kusimamia tupeane ushirikiano rafiki.
Unachonifurahisha huwa haujui kumvungia mtu unampa kavu lake live.
 
Haalafu huwezi kuamini! Binafsi nimesoma kuanzia page ya 1-3! Sijaelewa huyo Mashalove ni nani, na amefanya nini kiasi cha mtoa mda kumjia juu Mh. Waziri! Na kila anayeonekana kuwa upande wa Waziri kuonekana ni CHAWA!!

Nadhani kama kuna mtu mwenye ABC ya huu mtafaruku, angetuwekea humu jukwaani sisi tusio na access ya mitandao mingine nje ya jamii forums!
Aliewekwa maiki huyu wa pembeni yake michezo yake ya jukwaani inatuharibia watoto huku mikoani
maxresdefault-1701469445.jpg
 
Cheap popularity sasa Mimi inipeleke wapi kwa mfano? Yaani inisadie nini hasa wewe unavyodhani. Si usinipe tu hiyo popularity yaishe😀

Mimi nasimamia Yale ambayo nyie watanzania mmeyawekea Sheria ambazo zinatakiwa kusimamiwa kwa ajili ya kujenga maadili na kuwalinda watoto wenu. Ni hilo tu. Sheria ya mtandao kifungu cha 14 kasome Kiko online. Hii habari ya kuuliza serikali ina mkakati gani na mpango gani na Sheria ziko wapi, muwe mnakumbuka kuwa vyote vipi, na tukianza kusimamia tupeane ushirikiano rafiki.
Tupo pamoja na wewe mhe. Gwajima Maadili yanavunjwa kwa speed ya radi
Huyo masha mchukulie hatua kabisa.

Pia kuna nyimbo za ovyo sana
Kama
Mtoto kautaka na nyingine nyingi ni matusi matupu wanaimba bila muktadha
 
Haalafu huwezi kuamini! Binafsi nimesoma kuanzia page ya 1-3! Sijaelewa huyo Mashalove ni nani, na amefanya nini kiasi cha mtoa mda kumjia juu Mh. Waziri! Na kila anayeonekana kuwa upande wa Waziri kuonekana ni CHAWA!!

Nadhani kama kuna mtu mwenye ABC ya huu mtafaruku, angetuwekea humu jukwaani sisi tusio na access ya mitandao mingine nje ya jamii forums!
Kwakweli hata mm kwa hili limenipita kushoto sijapata udaku huu 😃😃😃
 
Bila kumsahau Afande aliyeamuru Binti wa Yombo Dovya abakwe. Fuatilia hao kwanza ambao wengi tunashanga mbinu zenu za kupindisha sheria.. Mko double standard sana Mungu anawaona!!!
Kila kiongozi anayo mipaka yake ya wizara yake, hilo hebu toa ombi lako kule wizara ya Katiba na Sheria tafadhali. Tuache kuwa tunapindisha utaratibu
 
Ni kweli kabisa mkuu,nimekumbushia hoja hii Dkt. Gwajima D kaniletea chawa wake wote na yeye mwenyewe kunishambulia vibaya sana kama vile siruhisiwi kutoa hoja humu jukwaani.
Sishambuliagi mtu mimi, Bali huwa naelimisha watu utaratibu na kuwaambia ukweli wa wazi wazi. Ila kwa Sababu baadhi kama wewe hivi labda wamezoea kuambiwa mambo kwenye braketi hivi, ndiyo maana labda wanaona wanashambuliwa. Mimi Mwalimu mzuri sana kwanza nipongeze tafadhali 🥳
 
Waziri mimi nakuunga mkono,hawa wasanii wapuuzi wengi sana isiishie kwa huyo tu nenda mpaka kwa wale wanaoshabikia ushoga mfano WCB wana mashoga wengi mule kwa kigezo cha ubunifu.

Uchafu wanaofanya unaharibu sana kizazi kuonekana ushoga ni kitu cha kawaida au ndo sanaa,mfikishie na waziri wa sanaa haya.
Dabiliyusiibi na ushoga pdidy papa grammy awards aaha
 
Back
Top Bottom