DOKEZO Waziri Gwajima, hii anayofanya Lillian Mwasha kwa watoto siyo sawa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu, niambie kosa la huyo Dada. Hao watoto wamejieleza wazi sababu za wao kuona wanachukiwa na Baba zao.

Au kwa mtazamo wako ulitaka aseme na ambao wanachukiwa na mama zao watoke mbele?
Mkuu nakukubali sana na post zako.

Vipi unamtetea huyo demu kwa alivyowatoa hao madogo kueleza hisia zao?
 
Kwanza nakushukuru kwa Sala na maombi yako 🙏🏽.

Aidha, mimi siko hivyo kuwa mtu atakaa kule apange lake ovu aje ausumbue moyo wangu. Hataweza. Huko nilishavuka kiumri na kimajukumu na kwa msaada wa Mungu. Hutokea tu automatic ukishaijua Dunia hii na mambo ya watu wake. Nifuatilie zaidi ya humu JF.

Sina namna nzuri ya kukuelezea. Maana nisipojitokeza kusema na wale ambao inabidi tabia zao tuwasaidie kuzirekebishe, maana nitakuwa nakimbia na majukumu yangu kwa nafasi yangu na umri wangu kama bibi sasa. Lazima niwape neno langu liwasaidie.

Atakayesikia haya asiyesikia naye shauri yake.

Ila wanaponirushia mishale yao mara ingine bila hata hatia, wakumbuke kuwa, wenye haya maJukwaa nao Wana kanuni zao za maisha ya humu jukwaani.

Ubarikiwe 🤝🙏🏽
 
Mhe hulali?
Nawe huwa unakesha kama miye ninayebukua mastaz yangu?
Btw good morning [emoji274]
[emoji28][emoji28][emoji28] yaani mm naona wakati nasoma PCB A level nililala kuliko huku kwenye uwanja wa jamii. Yaani lazima uongezee tu nguvu maana unaguswa na mambo na mimi sipendagi jambo lichelewe chelewe wakati kuna uwezekano wa kuongeza kasi....

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Kila huduma ina mwongozo wake na hizi huduma za ustawi nazo ni taaluma. Nia njema isipoenda na itifaki yake, inaweza kugeuka changamoto halafu tena tukaja kuulizana maswali.

Tujengane tu vizuri Ili umoja wetu uwe na tija nzuri kabisa
Tuliosomea Pyongyang tumekuelewa vizuri sana. Kifupi umesema huyo bi Dada kakurupuka na kakosea kuingilia kazi za watu. Asante Dr Gwaji girl.
 
Sijarejea BASATA kwamba yeye anahusika huko..hapana..nilikuwa najibu kuhusu hoja nyingine iliyotolewa kuwa kwenye vyombo vya habari..... Kunarushwa mambo fulani... Ndiyo nikatoa kinachoendelea. Tafadhali soma vzr utaona connection. Shukrani

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Maoni yamepokelewa, shukrani

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Haya maelekezo kashapewa tayari katika hatua za awali. Moyo wake tu ndiyo tunausubiri. Mengine yanaendelea sambamba na kujumuisha maoni yenu wote humu. Ndiyo maana napita kusoma Kila mchangiaji kasemaje. Kwangu mm hii ni teleconference ya kijamii kuona jamii inasemaje kwenye hizi changamoto mbalimbali za kijamii.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Shukrani nimepokea

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Ubarikiwe,

Kama mama wa familia, kwanza namshukuru Mungu kwa kunipa Mume mwema Advocate Gwajima ambaye, katika kila hatua ya mapito ananitia moyo Ili kazi niliyoaminiwa nayo Sasa na Mhe Rais basi iwabariki wengine na nimwakilishe vema yeye aliyenituma.

Hata hivyo, nadhani nimezoea kwani tangu nikiwa natibu hospitalini simu yangu pia ilikuwa wazi miaka yote na siku zote familia kwa kujua mapenzi yangu kwa huduma niliyonayo, hawajachoka kunitia moyo.

Hata nilipokuwa nimeondoka kwenye kuongoza hospitali nikawa wizarani nilifanya hivi na mkumbuke, bado wale wa inbox ambao Kila siku nawajibu sms, Mungu ndiye anajua. Na nitafanya hivi hadi mwisho wa utumishi wangu kwa kuwa Inabariki moyoni kubariki wengine, wakati ni sasa tukiwa hai.

Ndugu zangu wapendwa, kubwa katika yote ni upendo na uaminifu miongoni mwa wanafamilia na Mungu kati yenu, hapana mzigo mzito kwenye kuwabariki wengine. Kuwabariki wengine ni fursa adimu. Mtu akiipata na aitumie kwa faida yake, jamii yake na Mungu wake. Amina.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…