Mh. Dr Gwajima D, kwa jinsi unavyoijali kazi yako, nimekuvulia kofia[emoji122][emoji122][emoji122][emoji120]
Ninakufananisha na kuku wa kienyeji anayeyaatamia mayai yake kwa ajili ya kuvitotoa vifaranga. Huwa wako tayari kushinda ndani bila kula ili tu kuhakikisha mayai wanayoyaatamia hayahatiribiki kwa kupigwa na ubaridi.
Mchango wako wa mwisho kwenye huu uzi uliutoa saa Jana saa 2237, na huu wa sasa (leo) ni wa saa 0447.
Inafahamika kuwa mbali na kuwa Kiongozi wa Serikali, wewe pia ni mke na mama! Kwa hiyo hata ukitoka kazini bado una majukumu ya kifamilia n.k.
Ndiyo maana najiuliza, "huyu mama anapata muda wa kutosha kupumzika?"
Inawezekana alilala kwenye saa Sita au Saba za Usiku, lakini bado amemudu kuamka mapema na kuanza majukumu yake hata kabla hajaenda ofisini!
Dr, hakika unanihamasisha sana kwa uchapaji kazi wako! Hongera sana mama[emoji120][emoji120][emoji120]