DOKEZO Waziri Gwajima, hii anayofanya Lillian Mwasha kwa watoto siyo sawa

DOKEZO Waziri Gwajima, hii anayofanya Lillian Mwasha kwa watoto siyo sawa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu, niambie kosa la huyo Dada. Hao watoto wamejieleza wazi sababu za wao kuona wanachukiwa na Baba zao.

Au kwa mtazamo wako ulitaka aseme na ambao wanachukiwa na mama zao watoke mbele?
Mkuu nakukubali sana na post zako.

Vipi unamtetea huyo demu kwa alivyowatoa hao madogo kueleza hisia zao?
 
Umejiunganisha na uwepo wa MUNGU kweli au ni hisia ndio zimekupelekea uongee hivyo mkuu?

Mana MUNGU hachelewi wala hawai kutupiga matukio sisi viumbe wake ili kutupima imani zetu..Haswa nyinyi Mama zetu anawapiga matukio sana ili kupima imani zenu.

MUNGU akuongoze kweli kweli na asikutoe kwenye reli yako.

Hapo sikunpangia MUNGU kazi ila nimemuomba akuongoze na kizazi chako.
Kwanza nakushukuru kwa Sala na maombi yako 🙏🏽.

Aidha, mimi siko hivyo kuwa mtu atakaa kule apange lake ovu aje ausumbue moyo wangu. Hataweza. Huko nilishavuka kiumri na kimajukumu na kwa msaada wa Mungu. Hutokea tu automatic ukishaijua Dunia hii na mambo ya watu wake. Nifuatilie zaidi ya humu JF.

Sina namna nzuri ya kukuelezea. Maana nisipojitokeza kusema na wale ambao inabidi tabia zao tuwasaidie kuzirekebishe, maana nitakuwa nakimbia na majukumu yangu kwa nafasi yangu na umri wangu kama bibi sasa. Lazima niwape neno langu liwasaidie.

Atakayesikia haya asiyesikia naye shauri yake.

Ila wanaponirushia mishale yao mara ingine bila hata hatia, wakumbuke kuwa, wenye haya maJukwaa nao Wana kanuni zao za maisha ya humu jukwaani.

Ubarikiwe 🤝🙏🏽
 
Mhe hulali?
Nawe huwa unakesha kama miye ninayebukua mastaz yangu?
Btw good morning [emoji274]
[emoji28][emoji28][emoji28] yaani mm naona wakati nasoma PCB A level nililala kuliko huku kwenye uwanja wa jamii. Yaani lazima uongezee tu nguvu maana unaguswa na mambo na mimi sipendagi jambo lichelewe chelewe wakati kuna uwezekano wa kuongeza kasi....

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Kila huduma ina mwongozo wake na hizi huduma za ustawi nazo ni taaluma. Nia njema isipoenda na itifaki yake, inaweza kugeuka changamoto halafu tena tukaja kuulizana maswali.

Tujengane tu vizuri Ili umoja wetu uwe na tija nzuri kabisa
Tuliosomea Pyongyang tumekuelewa vizuri sana. Kifupi umesema huyo bi Dada kakurupuka na kakosea kuingilia kazi za watu. Asante Dr Gwaji girl.
 
Mh Waziri, hili la Lilian halihitaji basata haimbi bongo flever wala pale alikuwa hanengui ni mdangaji tu wamitandaoni, sheria zipo na ziko wazi hatua zichukuliwe kwa mujibu wa sheria. Zipo shule kitendo cha mzazi kupiga selfie shuleni mtoto anaweza fukuzwa shule. Sheria faragha za watoto ipo.
Sijarejea BASATA kwamba yeye anahusika huko..hapana..nilikuwa najibu kuhusu hoja nyingine iliyotolewa kuwa kwenye vyombo vya habari..... Kunarushwa mambo fulani... Ndiyo nikatoa kinachoendelea. Tafadhali soma vzr utaona connection. Shukrani

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Absolutly i salute now you are talking as a professional Doctor, kwa taaluma yako unajua hatua za makuzi ya watoto, huyu Lilian ni ignorant kwa kile alichokuwa akifanya.

Mh, napendekeza ukae na waziri wa elimu muweke mwongozo wa maudhui ya watoto mashuleni, uwepo uratibu wa shughuli kama hizi na kama kuna haja ya kuwa puplic basi serikali ihusishwe na ibariki
Maoni yamepokelewa, shukrani

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Mhe. Kuomba radhi iwe ni miongoni mwa hatua zitakazochukuliwa, muhusika aombe radhi hadharani kama alivyodhalilisha hao watoto pamoja na familia zao kupitia mitandao aombe radhi pia na ikiwezekana arudi shuleni kuomba radhi na ajutie kosa lake.
Alichokifanya kitawaathiri hao watoto hapo shuleni.
Haya maelekezo kashapewa tayari katika hatua za awali. Moyo wake tu ndiyo tunausubiri. Mengine yanaendelea sambamba na kujumuisha maoni yenu wote humu. Ndiyo maana napita kusoma Kila mchangiaji kasemaje. Kwangu mm hii ni teleconference ya kijamii kuona jamii inasemaje kwenye hizi changamoto mbalimbali za kijamii.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Kudos Mheshimiwa, suala la wazazi kutelekeza watoto ni suala moja, Alilolifanya Lilian ni suala lingine kabisa ambalo ndilo lengo la hii thread.

Umeelewa kwa usahihi mheshimiwa, na umechukua hatua sahihi.

By the way, kuna miongozo ya kufanya kazi na watoto (working with children), ili kutokusababisha Vulnerability na harm. Hili litiliwe mkazo, sio kila mtu anapaswa kupewa access na watoto tena wa sensitive issues kama hizi.
Shukrani nimepokea

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Mh. Dr Gwajima D, kwa jinsi unavyoijali kazi yako, nimekuvulia kofia[emoji122][emoji122][emoji122][emoji120]

Ninakufananisha na kuku wa kienyeji anayeyaatamia mayai yake kwa ajili ya kuvitotoa vifaranga. Huwa wako tayari kushinda ndani bila kula ili tu kuhakikisha mayai wanayoyaatamia hayahatiribiki kwa kupigwa na ubaridi.

Mchango wako wa mwisho kwenye huu uzi uliutoa saa Jana saa 2237, na huu wa sasa (leo) ni wa saa 0447.

Inafahamika kuwa mbali na kuwa Kiongozi wa Serikali, wewe pia ni mke na mama! Kwa hiyo hata ukitoka kazini bado una majukumu ya kifamilia n.k.

Ndiyo maana najiuliza, "huyu mama anapata muda wa kutosha kupumzika?"

Inawezekana alilala kwenye saa Sita au Saba za Usiku, lakini bado amemudu kuamka mapema na kuanza majukumu yake hata kabla hajaenda ofisini!

Dr, hakika unanihamasisha sana kwa uchapaji kazi wako! Hongera sana mama[emoji120][emoji120][emoji120]
Ubarikiwe,

Kama mama wa familia, kwanza namshukuru Mungu kwa kunipa Mume mwema Advocate Gwajima ambaye, katika kila hatua ya mapito ananitia moyo Ili kazi niliyoaminiwa nayo Sasa na Mhe Rais basi iwabariki wengine na nimwakilishe vema yeye aliyenituma.

Hata hivyo, nadhani nimezoea kwani tangu nikiwa natibu hospitalini simu yangu pia ilikuwa wazi miaka yote na siku zote familia kwa kujua mapenzi yangu kwa huduma niliyonayo, hawajachoka kunitia moyo.

Hata nilipokuwa nimeondoka kwenye kuongoza hospitali nikawa wizarani nilifanya hivi na mkumbuke, bado wale wa inbox ambao Kila siku nawajibu sms, Mungu ndiye anajua. Na nitafanya hivi hadi mwisho wa utumishi wangu kwa kuwa Inabariki moyoni kubariki wengine, wakati ni sasa tukiwa hai.

Ndugu zangu wapendwa, kubwa katika yote ni upendo na uaminifu miongoni mwa wanafamilia na Mungu kati yenu, hapana mzigo mzito kwenye kuwabariki wengine. Kuwabariki wengine ni fursa adimu. Mtu akiipata na aitumie kwa faida yake, jamii yake na Mungu wake. Amina.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom