Man filandu
JF-Expert Member
- Aug 31, 2023
- 412
- 402
Wewe issue sio kupitia station kadhaa kubwa za bongo, jibu mada hapo juu.Humjui Lilian Mwasha basi utakuwa hujawahi kusikiliza Radio maana amepita station kadhaa kubwa bongo
Asante sana ubarikiwe mama yangu.Ahsante Sana, pamoja na kuwa Niko safari mbali Sana na masaa yanatofautiana, Mungu alinipa Rehema za kuona. Kwa kweli hili jambo halina afya kabisaaa.
Pamoja na uchovu na usiku wote huo: nilihakikisha katika hatua za awali Nampata mhusika na kumwambia hili jambo ni baya, halifai na ni kinyume na sheria ya mtoto na huduma za ustawi. Aache mara moja. Aidha, nimeelekeza ofisi yangu washughulikie kwa stahiki zote zinazohusika na asitokee mwingine kufanya mambo haya hayafai.
Ahsante Sana.
Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Venue Sio sahihiSioni alichokosea
Ifike wakati wababa wawajibike na malezi
Hao wasichana wanahitaji upendo na malezi ya baba zao
Nakupenda Bure aiseeee, tungekua na mawaziri wanaojitambua Kama WEWE tungekua na Tanzania nzuri sana sana. MUNGU azidi kukubariki Mtumishi DorothyUko sahihi kabisa, hapa ni kuongezea tatizo. Hatua zitachukuliwa na za awali mimi nimechukua tayari
Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Elimu kweli inahitajika kwa utaratibu mzuri na siyo kila mtu aonavyo yy. Mtu akiona anacho kipaji cha kutoa elimu, na aje tumjenge vzr ili asije kuharibu. Maana akiharibu hata yy hao hao anaojaribu kuwasaidia watamgeuka wakiona anaweza kuwa mtaji wao.Namuunga mmono Lilian Mwasha.
Ujinga mwingi sana unafanyika majumbani na wanawake hawana pa kukimbilia wala pa kusemea kwa sababu hata hayo madawati yanahudumiwa na wengi wanaonyanyasa wanawake huko majumbani.
Dkt. Gwajima D naamini bado jamii inahitaji elimu ya familia kabla ya khinvia kwenye kuunda familia
Naomba sana sana pamoja na hili, naomba Kwa ustawi wa Watoto wetu ANGALIA suala la vipindi vya Radio na Tv vya watoto ambao wanashindanishwa kuimbishwa na kuchezeshwa nyimbo ambazo hazina maadili. Angalia TV hata jumapili au Jumamosi hii utashangaa Nia aina Gani ya kizazi tunachokilea. Asantee sana Dada DorothyAhsante Sana, pamoja na kuwa Niko safari mbali Sana na masaa yanatofautiana, Mungu alinipa Rehema za kuona. Kwa kweli hili jambo halina afya kabisaaa.
Pamoja na uchovu na usiku wote huo: nilihakikisha katika hatua za awali Nampata mhusika na kumwambia hili jambo ni baya, halifai na ni kinyume na sheria ya mtoto na huduma za ustawi. Aache mara moja. Aidha, nimeelekeza ofisi yangu washughulikie kwa stahiki zote zinazohusika na asitokee mwingine kufanya mambo haya hayafai.
Ahsante Sana.
Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
SawaHili suala nimewapa wataalamu walichambue, waje na mapendekezo ya hatua stahiki. Naomba tuvute subira. Ahsante Sana
Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Kwa mujibu wa waziri ngoja wajiridhishe kwanza yeye na jopo lakeHata onyo ni hatua za kisheria pia.
Sijui pia kama amevunja sheria gani.
Nashukuru kwa jibu zuri Mheshimiwa.Elimu kweli inahitajika kwa utaratibu mzuri na siyo kila mtu aonavyo yy. Mtu akiona anacho kipaji cha kutoa elimu, na aje tumjenge vzr ili asije kuharibu. Maana akiharibu hata yy hao hao anaojaribu kuwasaidia watamgeuka wakiona anaweza kuwa mtaji wao.
Hakika elimu kweli bado inahitajika kwa wingi na ndiyo maana sasa pamoja na huko kwenye jamii bado na redioni na mitandaoni humu tunafika mubashara kabisa. Mashuleni kuna miongozo ya madawati ya ulinzi pia, kuna namba za call center ikiwemo 116 kwa ajili ya watoto. Kifupi mifumo ipo sema Kila mmoja atimize wajibu tu. Ahsante kwa maoni juu ya umuhimu wa elimu.
Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Anatumia kipimo gani?Anawauliza watoto wanaochukiwa na baba zao. Je amewaandaa kisaikolojia? Mbona yaonekankama ni udhalilishaji kwa watoto na wazazi wao. Angalia clip hapa
Uko sahihi, mawazo yako yanajenga. Na utaona tukiyatumia, ubarikiweNashukuru kwa jibu zuri Mheshimiwa.
Nina hoja mbili za nyongeza.
Hawa waelimisha rika wa kujitegemea (wote) wanahitaji kupigwa msasa waendane na malengo ama utaratibu wa serikali kwenye kuelimisha. Empowering society bila kuzingatia parameters na ethics za sheria na kanuni ni kutengeneza tatizo jipya.
Kuna wataalam wa ushauri (Councelors) waliosomea na kuhitimu. Hawa watu eanafanya shughuli gani kwa sasa? Watu kama Lilian Mwasha wanaibuka na kuziba pengp lililopo la wataalam ambao tayari tunao.
Je unaonaje serikali ilipanua wigo wa kuelimisha jamii haswa kuanza kuwapiga msasa mara kwa mara wadau kama Lilian Mwasha?
Yaani Kila kitu kinautaratibu, nikifanya langu mm hapa, watakuja waseme waziri kakurupuka. Wote huwa tunafuata utaratibu huu huu, kuwa kwa haraka waziri huwa nasema hili baya au hili liko hivi, na nimesema hapo tayari. Sasa, kinachofuata ni kuwa, ataitwa na kamishna, atahojiwa ilikuwaje kafikaje huko alikofika, atasema, huenda wengine wataunganishwa maana uelewa utakuwa sasa mpana. Inaweza gusa huko shuleni alikokuwa lakini pia watoto watahitaji huduma na wazazi pia watahitaji huduma, yaani mfumo mzima uliguswa utahusika kwenye hatua mbalimbali Kila mmoja kwa nafasi yake kama ni kupata unasihi au kuwajibika. Na hapo baada ya huo uchambuzi ndiyo wizara itasema ikaja ikaenda ikawa hivi na Sasa kilichofanyika hiki. Halafu Sasa maoni yatatolewa je nn kimesahaulika au kimeachwa wapi Ili hatua zaidi ziendelee juu eneo hilo. Nadhani huu ni utaratibu mzuri kabisa, au vipi ndugu zangu?Kwa mujibu wa waziri ngoja wajiridhishe kwanza yeye na jopo lake
Ahsante Sana. Mambo mengi ya jamii yana dhamana ya wizara mbalimbali za kisekta, wizara yangu tunaendelea na uratibu wa wadau wa kisekta kama nilivyotamka tarehe 12 Sept 2023 tukiwa na BASATA, Cosota Bodi ya FILAMU wanaouhusika na udhibiti wa uzalishaji content.Naomba sana sana pamoja na hili, naomba Kwa ustawi wa Watoto wetu ANGALIA suala la vipindi vya Radio na Tv vya watoto ambao wanashindanishwa kuimbishwa na kuchezeshwa nyimbo ambazo hazina maadili. Angalia TV hata jumapili au Jumamosi hii utashangaa Nia aina Gani ya kizazi tunachokilea. Asantee sana Dada Dorothy
Udhalilishaji upo.Tunzeni watoto wenu, huo ni ukweli hakuna udhalilishaji hapo.
Kilichofanyika sio kukosea ni upumbavu tu, kwanza Lilian sio mwalimu wa hiyo shule kilichompeleka pale sijui ni nini? Huwezi hoji under age na kuwepa information public bila ridhaa ya mazizi, tuseme mama zao hao watoto ndo walimtuma? Anajua nini kimefuatia kwenye familia baada ya taarifa kuzagaa mitandaoni? Ifike sehemu watanzania akili zitukae sawaAmekosea sana aaiseee angekuwa na Nia ya kutibu angewaita praivate na kukutana na wazazi wao, Sasa mtoto anasema baba hanihudumii kwa chochote??? Anawatia moyo tuuu lakini hakuna msaada hapo
Ubarikiwe, tumshukuru Mungu, tuombeane tupate Rehema zake kwa ushirikiano zaidi, ushirika wa Rehema zake [emoji1431][emoji1666][emoji1241]Nakupenda Bure aiseeee, tungekua na mawaziri wanaojitambua Kama WEWE tungekua na Tanzania nzuri sana sana. MUNGU azidi kukubariki Mtumishi Dorothy
Mh Waziri, hili la Lilian halihitaji basata haimbi bongo flever wala pale alikuwa hanengui ni mdangaji tu wamitandaoni, sheria zipo na ziko wazi hatua zichukuliwe kwa mujibu wa sheria. Zipo shule kitendo cha mzazi kupiga selfie shuleni mtoto anaweza fukuzwa shule. Sheria faragha za watoto ipo.Ahsante Sana. Mambo mengi ya jamii yana dhamana ya wizara mbalimbali za kisekta, wizara yangu tunaendelea na uratibu wa wadau wa kisekta kama nilivyotamka tarehe 12 Sept 2023 tukiwa na BASATA, Cosota Bodi ya FILAMU wanaouhusika na udhibiti wa uzalishaji content.
Tunaendelea na ushirikiano na wenye dhamana ya hivi vyombo vya habari pia.... Shukrani kwa maoni yako.
Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Upuuzi ,utaongeleaje masuala ya deep ya familia ( na watoto) mbele ya kadamnasi ...mpumbavu sana!Anawauliza watoto wanaochukiwa na baba zao. Je amewaandaa kisaikolojia? Mbona yaonekankama ni udhalilishaji kwa watoto na wazazi wao. Angalia clip hapa
Ahsante waziri, umeongea kwa busara sana 🤜🤛Hili kakosea, hatua zitachukuliwa na wengine wasifuate huu utaratibu. Yako baadhi ya matatizo ikiwemo haya ya migogoro ya watoto na familia inabidi jamii wawape wataalamu wa ustawi wa jamii Ili waendelee kitaalamu.
Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app