Waziri Jafo abadili gia angani, afuta maamuzi yote ya wasimamizi wa uchaguzi kuwaengua wagombea. Wagombea wote ruksa kushiriki uchaguzi

Ingekuwa mimi mpinzani wangu kajitoa ningefurahi maana siku zote nimemfanyia figisu ila anajitahidi ananishinda. Sasa kajitoa ningejitutumua
 
Kwa siasa za Tanzania, ukishindwa kujiuzulu nafasi ya kuteuliwa, basi kubali kusimamia kila kitu hata Yale usioyaamini.
 
Kama walikosea kisheria...kwanini wasemehewe kirahisi hvyo bila kukagua fomu zao...kama kuna qliyejaza matusi je?? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Kashikwa pabaya sana.
 
Mimi naamini kabisa kwamba Polepole kwa sasa anasimamia mambo mengi asioyaamini. Nafsi yake inamsumbua Sana na asipopata mke kwa kumbwambia relax, by the time anaacha hiyo nafasi atakuwa hayupo sawa kisaikolojia.
 
Hahaha kwani shule alikuwa anayosoma haya yanayotokea leo?!

Yule mwalimu, wangemrudisha akafundishe Kama taaluma ina-matter.
 
Uchaguzi au uchafuzi (kama baadhi wanavyouita), umeisha kwa asilimia kubwa baada ya Wana Ccm "kupita bila kupingwa"! Lakini Leo hii Waziri mwenye dhamana " ametengua" matokeo hayo!

Swali, je CCM wanaweza kumshtaki Waziri kwa "kuwapora" ushindi wao? Je Waziri ana uwezo wa kutengua matokeo ya Uchaguzi?

Naomba kujuzwa
 
Kama vyama vya upinzani vimeshatangaza kujitoa, shida ya nini tena. hizi pesa tunazoharibu kufanya sarakasi za uchafuzi ni bora tungeongeza barabara hata za changarawe. kuna hii barabara ya makongo imejaa madimbwi ya maji hata samaki wameanza kuzaliana humo.
 
Nimesikia kuna mtu amefura jumba jeupe hataki ata kula ; Anadai kwanini hao wapinzani na alishatoa amri wafutwe wote ?

Anasema yeye hapingwi na ngoja uchaguzi uishe kama Unajua ujajiandika kupiga kura utasakwa popote ulipo na utaona chamtemakuni.
Poleni waTanzania watu ambao hawakua tayari mkawasukumia kitu kigumu sasa anawatesa kwanini mlimsukumia.
 
Chaguzi zijazo au uchaguzi huu wa tarehe 24 Novemba 2019?? Zimebaki siku ngapi?? Wazo lako zuri sana ila muda hauko vizuri upande wa Jafo. Kuhusu mgombea binafsi tungetamani ila labda uchaguzi mkuu 2020 kuondoa mchanganyiko huu. Hata kama Jafo akiamua kwa nguvu zake kuweka majina hayo yaliyokuwa yameenguliwa nadhani atakuwa ana-force matumizi ya vyama vyao kwani vyama vishajiondoa. Kama chama kimejiengua, inamaana hakina mgombea. Lakini tumeona wakihalalisha wabunge kuendelea kuingia bungeni bila chama. Hao nao watagombea bila hiari ya chama. Mbowe anasema "Kukibaka chama" mchana peupeeee
 
Mwenyekiti wetu kasema hatutashiriki .
Na HATUTASHIRIKI.

Shindeni nyie. Ushindi wa kishindo.
Tumekubali yaishe.
 
Uwezo na akili za ndugu Jafo....unazionaje au unamuelewaje?

Utakavyoelewa huenda mnafana akili....Hongera.

Kushindwa kujaza fomu na kuzirejesha kwa kuchelewa; Uzembe.

Watanzania hatupaswi kufanya majaribio ya Uongozi kwa wazembe kama hawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…