Waziri Jafo abadili gia angani, afuta maamuzi yote ya wasimamizi wa uchaguzi kuwaengua wagombea. Wagombea wote ruksa kushiriki uchaguzi

Jafo
Tume
CCM
Serikali

Kila hoja wanayotoa kuhalalisha mazonge yao inakosa mashiko na ndio watu wanazidi kuiona hila yao

Yani hizi wiki tatu zimekua Ni za aibu kuu kwa gvt

Pole Sana jafo ivumayo haidumu.
MANCHESTER CITY matokeo yenu tunayo
 
Namuonea huruma kwa jinsi alivyotumika duh magufuli siku ukimsikia itakuwa ni siku ya uteuzi.
 
Nimeipenda hii kauli ya Msimamizi mkuu wa uchaguzi wa serikali za mitaa Waziri Jaffo.

" Hakuna Kukimbiana Lazima Kieleweke"

Chadema msiweke mpira kwapani rudini uwanjani refa anawaita.

Maendeleo hayana vyama!

cc: Daudi Mchambuzi


..REFA mwenyewe mkereketwa wa CCM.

..Jafo hakutakiwa kuongea kishabiki namna hiyo.
 
kuna game zingine refarii unashindwa kuwa neutro Kama game ya Leo MAN CITY VS LIVERPOOL
Mkuu utawafanya watu wanune.....

Umekosa mfano mwingine wowote, Bali utoe mfano wa mechi kati ya Liverpool VS Man City
 
Kile kikao cha ikulu kile cha watendaji, niseme
Asante Mungu majibu yamewahi mno kutoka.
Ni 1 ya kikao ambacho mi sijui kilichojadiliwa ni nini! Chaguzi zote awamu hii tu ndo wagombea wakosee kujaza form?
Mtendaji anaenda chooni siku nzima?
Kwenye hii sarakasi ya huu uchaguzi mdogo, nishauri tu katiba mpya idaiwe na tume huru ya uchaguzi bila kusahau shughuli za kisiasa kwa vya vyote zitambulike na mihimili isiingiliane!
 
CCM tuitishe maandamano kumpinga Jafo. Amepora ushindi wetu wa wazi na kuwarudisha waliopewa RED CARD uwanjani.

CCM hatukubali. Tutang'oa viti vyote na kuchomoa betri.
 
Mkuu utawafanya watu wanune.....

Umekosa mfano mwingine wowote, Bali utoe mfano wa mechi kati ya Liverpool VS Man City

Liverpool kabebwa na mwamuzi hadi aibu.
Hawana tofauti na CCM.
 
Kwenye mechi ya simba na yanga......unamweka Haji Manara ndio referee unategemea nini......
 
Halafu wasimamizi ni wale wale, huyu mtu anatuona sisi wote wajinga.
 
Hahahaaaaa......!

Umenikumbusha Mchungaji Erasto: Jaffo mnamuonea bure hana sifa ya Jaji

Maendeleo hayana vyama!
Kama hana sifa ya Jaji kwanini ajifanye kuwa na kutekeleza jukumu la Jaji kwa hiari hata kwa shinikizo? Ona sasa anakejeliwa na kudharauliwa yeye huku aliyemwagiza anaendelea na kazi anayopenda ya kuteua Jumapili akiachana na kanisa maana amegundua anawa-bore waumini wengine. Ashukuru tu katika uteuzi hakutenguliwa yeyote maana angekuwa mmoja wao kwani ni wa pwani lakini hata hivyo akae chonjo maana hatma yake itategemea hatua watakayochukua wapinzani kutokana na gia aliyobadili angani. Yes, yes kila wakati bila kupima na kuhoji mantiki yake huwa na madhara makubwa. Tuendelee kusubiri lakini wapinzani wasigeuke nyuma watakuwa jiwe la chumvi siyo lile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…