Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Ni kweli atamgeuka kama alivyomgeuka Irene Isaka wakati wa.. kikokotoo cha mafaoJafo anageuka supu kesho. Mwigulu ndani. Jiwe atajisafisha na kushangaa yaliyotokea na kumtupia lawama zote Jafo.
Mchezo utamalizwa kwenye kutangaza washindi. CCM itashinda kwa asilimia 100.
Jafo ni waziri wa nchi. Mwenye wizara yake anafuatilia kwa ukaribuKesho jiwe atamfukuza Jafo na kumkabidhi mikoba Mwigulu Nchemba. Atatoa kauli za kupooza pooza makali ili kujaribu kuonyesha naye amekereka.
Wait and see
Hahaha ccm sio wakubwa kiivyo, labda useme unene wa ugonjwa.[emoji30][emoji30][emoji30] View attachment 1259773
Katika mazinira haya kauli ya "kupita bila kupingwa' haina mashiko. Kwa kigezo gani? Ambapo wasimamizi ni haohao waliotufikisha hapa?Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ametangaza kuwaruhusu wagombea wote waliochukuwa fomu na kuzirejesha kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini Tanzania Novemba 24, 2019 wanaruhusiwa kushiriki uchaguzi huo na amefuta maamuzi yote yaliyofanywa na wasimamizi wa uchaguzi Nchini kote ya kuwaengua wagombea wa vyama mbalimbali. Waziri Jafo ametoa uamuzi huu jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na wanahabari leo.
Chanzo: Ukurasa wa OR-Tamisemi Facebook
Hata hivyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa nchini Tanzania (Tamisemi), Selemani Jafo ametangaza wenyeviti wa vijiji 6,248, wa mitaa 1169 na vitongoji 37,505 wanaotokana na CCM wamepita bila kupingwa baada ya kutojitokeza kwa wagombea kutoka vyama vya upinzani.
“Kwa upande wa vitongoji Chama cha Mapinduzi kimepita bila kupingwa katika vitongoji 37,505 kati ya vitongoji 64,384 sawa na asilimia 58,”
Amesema katika wajumbe wa kundi la wanawake jumla ya wajumbe 64,085 wamepita bila kupingwa na wajumbe kundi la mchanganyiko jumla ya wajumbe 75,560 wamepita bila kupingwa.
Waziri kapwaya Sana kwenye hili na msingi wake ni chama chake kimehodhi shughuli nzima ya uchaguzi Kwa hiyo uwazi unakuwa sifuri.
Acha janja janja umeruhusiwa kugombea pamoja na ukilaza wako wa kushindwa kujaza fomu tuone kama utapata hata mtaa mmoja!
Kurudi tena ni kushiriki unajisi. Wahenga walisema akumulikaye mchana usiku atakuchoma. Ccm washaonesha wanachotaka kufanya na hawatogeuka nyuma hata kama CHADEMA, ACT, na NCCR watarudi kushiriki. Hivyo kushiriki ni kuhalalisha unajisi unaotaka kufanyika.