Waziri Jafo abadili gia angani, afuta maamuzi yote ya wasimamizi wa uchaguzi kuwaengua wagombea. Wagombea wote ruksa kushiriki uchaguzi

Waziri Jafo abadili gia angani, afuta maamuzi yote ya wasimamizi wa uchaguzi kuwaengua wagombea. Wagombea wote ruksa kushiriki uchaguzi

Jafo anageuka supu kesho. Mwigulu ndani. Jiwe atajisafisha na kushangaa yaliyotokea na kumtupia lawama zote Jafo.

Mchezo utamalizwa kwenye kutangaza washindi. CCM itashinda kwa asilimia 100.
Ni kweli atamgeuka kama alivyomgeuka Irene Isaka wakati wa.. kikokotoo cha mafao
 
Nimesoma kuwa Mhe. Waziri wa TAMISEMI amelegeza kamba kwa wagombea hata wale waliowekewa pingamizi. Je Vyama vya upinzani sasa vitarudi ulingoini?
 
Maendeleo hayana Chama....!!! Hii ni kauli ya kinafikiiii kuliko Unafikii wowote unao ufahamu duniani
 
Kesho jiwe atamfukuza Jafo na kumkabidhi mikoba Mwigulu Nchemba. Atatoa kauli za kupooza pooza makali ili kujaribu kuonyesha naye amekereka.

Wait and see
Jafo ni waziri wa nchi. Mwenye wizara yake anafuatilia kwa ukaribu
 
Kwa kauliii hiii inamaana Utaratibu haukufuatwaaa walifanya kwa Maagizo kutoka Juuuu....!!! Sasa alicho kisema Lipumba kinanikaa akilini...!!!
 
John Mnyika kasema atampelekea waziri Jafo barua ya kuwakataza kutumia nembo ya CHADEMA kwenye uchaguzi kwa sababu CHADEMA imeshajitoa.

Lakini angemkumbusha tu kwamba hakuna mgombea huru Tanzania.

Wagombea wote ni mali ya vyama vinavyoshiriki uchaguzi, na kama chama kimejitoa, hakuna haja kukiweka kwenye ballot paper.

Na ikiwa Tamisemi watashikilia msimamo wao CHADEMA wawatangazie wananchama wao tena kwamba wasishiriki kampeni na uchaguzi serikali za mitaa 24/11/2019, kwa sababu chama kimeshajitoa.
 
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ametangaza kuwaruhusu wagombea wote waliochukuwa fomu na kuzirejesha kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini Tanzania Novemba 24, 2019 wanaruhusiwa kushiriki uchaguzi huo na amefuta maamuzi yote yaliyofanywa na wasimamizi wa uchaguzi Nchini kote ya kuwaengua wagombea wa vyama mbalimbali. Waziri Jafo ametoa uamuzi huu jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na wanahabari leo.

Chanzo: Ukurasa wa OR-Tamisemi Facebook


Hata hivyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa nchini Tanzania (Tamisemi), Selemani Jafo ametangaza wenyeviti wa vijiji 6,248, wa mitaa 1169 na vitongoji 37,505 wanaotokana na CCM wamepita bila kupingwa baada ya kutojitokeza kwa wagombea kutoka vyama vya upinzani.


“Kwa upande wa vitongoji Chama cha Mapinduzi kimepita bila kupingwa katika vitongoji 37,505 kati ya vitongoji 64,384 sawa na asilimia 58,”

Amesema katika wajumbe wa kundi la wanawake jumla ya wajumbe 64,085 wamepita bila kupingwa na wajumbe kundi la mchanganyiko jumla ya wajumbe 75,560 wamepita bila kupingwa.
Katika mazinira haya kauli ya "kupita bila kupingwa' haina mashiko. Kwa kigezo gani? Ambapo wasimamizi ni haohao waliotufikisha hapa?
 
Watu walishapanda basi kuelekea November 24.
Halafu jamaa "wamechomoa betri"
Hakuna "gari" lingine!
Safari ipo hapo?
Abiria wengi wameshashuka.
Lakini dereva kang'ang'ania usukani anasema gari itawaka tu!
Kumbe dereva hana leseni!
Tafuteni dereva mwingine safari ijayo.
 
Kurudi tena ni kushiriki unajisi. Wahenga walisema akumulikaye mchana usiku atakuchoma. Ccm washaonesha wanachotaka kufanya na hawatogeuka nyuma hata kama CHADEMA, ACT, na NCCR watarudi kushiriki. Hivyo kushiriki ni kuhalalisha unajisi unaotaka kufanyika.
 
Kiongozi huyu Jafo ana mawazo sana ukimuangalia usoni ni mtu ambaye amechanganyikiwa

Hajui mustakabali wake, Huyo Jafo anaweza fanywa mbuzi wa kafara

Waziri kapwaya Sana kwenye hili na msingi wake ni chama chake kimehodhi shughuli nzima ya uchaguzi Kwa hiyo uwazi unakuwa sifuri.
 
Wazungu wana msemo wao usemao "gabbage in gabbage out", ukipanda uvundo utavuna uvundo. Ni wazi serikali ya CCM na Watendaji Kata wake wameonesha nia ovu ya kuhakikisha Wapinzani hata kama watashinda, hawatapewa ushindi wowote.

Baada ya kubanwa, Waziri Mhusika ameamua kutengua maamuzi ya Wasimamizi wa uchaguzi yaliyoengua maelfu ya wagombea wa Upinzani na kuwataka waendelee na uchaguzi.

Lakini ikizingatiwa tayari wasimamizi wameonesha nia ovu (malice aforethought), tutarajie haki kutendeka kama hawa Wapinzani watarejea kwenye uchaguzi?
 
Sasa ccm ilichotaka si ushindi,jamaa wameshakula kona,ijitangazie ushindi then Mkulu apongezwe kwa kufanikisha ushindi wa kishindo 100%,basi.
Kurudi tena ni kushiriki unajisi. Wahenga walisema akumulikaye mchana usiku atakuchoma. Ccm washaonesha wanachotaka kufanya na hawatogeuka nyuma hata kama CHADEMA, ACT, na NCCR watarudi kushiriki. Hivyo kushiriki ni kuhalalisha unajisi unaotaka kufanyika.
 
Hakuna kitu kama hicho,labda watoto wadogo wa chekechea ndio watakaohadahika .
Washalikologa bwembela wacha walinywe wenyewe.
 
Nia yao ovu itabati palepale .wanachotaka vyama vishiriki kuuhalalisha ushindi wa wizi.
Hapatwi mpinzani hapa.wapepatwa wenyewe CCM na utawala wao wa kibwege na kimla.
 
Back
Top Bottom