Waziri Jafo abadili gia angani, afuta maamuzi yote ya wasimamizi wa uchaguzi kuwaengua wagombea. Wagombea wote ruksa kushiriki uchaguzi

Hakuna mpinzani wa kweli atakaye weza kushiriki huo uchaguzi wa udanganyifu
 
Mtego wa panya, unawarudisha ili uwabane siku ya mwisho wakati wa kutangaza matokeo. Waziri Jafo anaugeuza uchaguzi kuwa wa hisani toka kwake na kauli za kibabe. Tukumbuke kuwa waziri wa Mambo ya Ndani kwenye kikao cha bunge alitoa maelekezo jeshi la polisi liwashughurikie waliojitoa! Hawa waziri aliwaita wanataka kusababisha uvunjifu wa amani.
Jafo alitakiwa aeleze sababu za kuwarejesha kinyume na sheria zilizosababisha wakose sifa! Swali, Jafo anayo mamlaka ya kutengua sheria?
 
Wapinzani wakishiriki uchaguzi huu wa kihuni, sitapiga kura tena mpaka nitakaporejea mavumbini.
Wapinzani wepi unawazungumzia? Dovutwa and company mbona washatangaza kuwa watashiriki maana kwao ni fursa. Walisema "anayesusa kashiba." Wao wanayo njaa, watashiriki ili washibe.
 
Wagombea wa upinzani waliondolewa kwa kushindwa kukidhi sheria za uchaguzi huo! Sasa waziri aliyesema kwa msisitizo kuwa sheria za uchaguzi lazima zifuatwe, leo anawarudisha kwenye uchaguzi kwa lugha za mitaani za kejeri za kuweka mpira kwapani! Na lazima kieleweke kitu. Haya mamlaka ya kutengua sheria ambayo iliwaondoa wagombea ameyapata wapi? Tuelezwe kabla ya kuwarudisha kwenye uchaguzi.
 

Hali tofauti ipi?

Maana hakuna mtu anaenda kwenye sanduku kama masharti mezani hayajafanywa kwa ukamilifu!

Opposition has the leverage here!

Halafu ni so scary kama dunia hii kuna watu hatari and dumb kama mawe wanaongoza nchi yeyote!
 
Hata Tunisia, Misri na Sudan kulianza hivyo.

Ee, Mungu iepushe Tanzania yetu kwa KUWAADHIBU NA KUWAFUTILIA MBALI WALE WOTE WENYE MIPANGO NA NIA OVU NA HII NCHI.
 
Kesho jiwe atamfukuza Jafo na kumkabidhi mikoba Mwigulu Nchemba. Atatoa kauli za kupooza pooza makali ili kujaribu kuonyesha naye amekereka.

Wait and see
TAMISEMI anakwenda kupewa Nape siyo Mwigulu.
 
Tarehe 24 wananchi wanachagua wagombea ....yaani ile asilimia 32.
badala ya kuwahamasisha wapige kampeni nyie mko mtandaoni
 
Nilishangaa sana watendaji hawafungui ofisi wiki nzima, jaffo yupo tu.Ningelikuwa jaffo wale watendaji wangefutwa kazi siku ileile.jaffo afukuzwe ofisini ameshindwa majukumu.
 
Haya.
Swali lisilo na kona wala milima mirefu, lakini kulijibu haiwezekani, kwa nini?

Kwa sababu serikali imejipa madaraka ya kutunga, kufuta na kutafsiri sheria yoyote kadri waonavyo wao inawapendeza. Hiyo ndio sababu..

Ni swali zuri sana na la kufikirisha.
 
Sawa serikali inayo kupitia bunge, naye Jafo anayo mamlaka hayo bila kupitia bunge?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…