leveroi
JF-Expert Member
- Sep 23, 2016
- 374
- 322
Kukubali kwa wapinzani kuingia tena kwenye uchaguzi huu watakuwa wenyewe hawajitambui. Ila natambua wapinzani ( au kwa lugha nzuri "vyama mbadala"), ni watu wenye uelewa mpevu pengine hata kuliko hawa watu wa serikali na chama chao. Hapo Jafo anawakilisha tu maamuzi geugeu toka kwa bosi wake. Yote ya kijinga yalofanyika ya kuwaengua wagombea wa upinzani haikuwa jambo la bahati mbaya bali liliratibiwa toka juu.( wewe unayetaka udhibitisho wake endelea kuganda hapo ukisubiri).
Kwa mfano hai (ingawa sitataja Nina wahusika ila ni ndani ya Babati mjini) hao wanaoitwa wasimamizi wadogo ambao ni watendaji wa mitaa(tambua hiyo ni serikali), kuna mmoja alifuatwa usiku wa SAA sita baada ya muda wa pingamizi kupita akalazimishwa kusaini barua ya pingamizi, tena hata waloweka mapingamizi wenyewe hawakuwa na habari kwani ni majina yao tu yaliwekwa bila wao kuhusishwa.
Kwa mantiki hiyo Jafo anapokuja na kete ya kufuta utenguzi wa kijinga ulofanywa, ni janja tu ili ulimwengu uone kwamba kuna chaguzi za vyama vingi nchini. Ila tukumbuke ile kauli au niseme amri walowahi kupewa wakurugenzi...mshahara nikulipe mimi,....halafu usimame utangaze mpinzani kashinda, utakuwa na akili kweli wewe!!! Hapohapo tusisahau watendaji wote wa kata waliitwa madhabahuni na kuhimizwa na kuagizwa waloagizwa, ambao hao wote ndo wenye dhamana ya kutangaza matokeo ya chaguzi zetu.
Kwa maana hiyo endapo mamlaka ikifanikiwa kushawishi wapinzani kurejea, hakika hiyo kete ya mwisho ya kutangaza matokeo itakula kwao tu.